Wakuu, TEC wapo serious si kidogo
Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania-TEC limetoa Limetoa mwongozo mpya kuwakumbusha Waamini taratibu na kanuni kwenye Ibada kanisani ambao unapiga marufuku wageni kuzungumza kanisani isipokuwa paroko/padri kama tukio ni la Kiparokia, Askofu wa Jimbo kama tukio ni la Kijimbo, Rais wa Baraza la Maaskofu-TEC kama tukio la kitaifa.
Viongozi hao katika ibada husika watatambua kwa ufupi uwepo wa wageni wa kidini, kiserikali na waalikwa wengine bila ya kuwapa nafasi ya kuongea, kutoa hotuba wala kusalimia. Zaidi Padri Chesco Msaga ambae ni Naibu Katibu Mkuu Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania anasema hata angekuja kingozi kutoka wapi, hataruhusiwa kuzungumza wakati wa ibaada.
Pia soma
Kanisa Katoliki limepiga Marufuku Viongozi wa Serikali/Wanasiasa kuhutubia/kusimama mbele ya madhabahu na kutoa neno
View attachment 3377707