Naibu Waziri Adamu Malima aibiwa kila kitu hotelini Morogoro!

Sakata la Mh. Adam Malima maswali mengi bila majibu.

Hivi katika hali ya kawaida, mtu anawezaje kumiliki silaha zote hizo, yaani bastola(pistol) na bunduki kwa ajili ya kujihami na maadui na bado anashindwa kugundua kua tayari hapo alipo ameshazingirwa na maadui(ama ni vibaka ama majambazi) na wanafanikiwa kumuibia mali zake pasipo yeye mwenyewe kushtuka mpaka shughuli nzima ina kamilika pamoja na masilaha yote aliyokua nayo.

Binafsi huu ni udhaifu wa hali ya juu, kua huyu kiongozi anashindwa kumiliki silaha lakini pia anashindwa kujilinda yeye binafsi na hivyo kuhatarisha maisha yake pamoja na maisha ya watu wengine.

Kwa msingi huo napendekeza mara baada ya uchunguzi kukamilika juu ya mazingira ya uvamizi huo na kuthibitika kua kulikua na uzembe kwake yeye binafsi huyu kiongozi anyang'anywe silaha, na aajiri walinzi binafsi na hii ni kwa faida yake mwenyewe sababu hawa wavamizi pia wangeweza kuchagua ama kumuibia hizo silaha ama kumdhuru yeye mwenyewe binafsi ama vyote kwa pamoja.

Lakini pia si vibaya tukajiuliza swali hili, Kwa hoteli ya hadhi ya namna hiyo inawezekana vp kufanyika wizi wa namna hiyo pasipo walinzi wa hoteli hiyo kushtuka mpaka kunakucha pasipo kuacha alama isiyo na mashaka kua hapa kweli wizi ama uvamizi ulifanyika?

Mi nadhani kuna taarifa ambazo bado tumenyimwa juu ya mazingira ya uvamizi huo.

Hatahivyo ni swala la muda tu kabla ya ukweli wote kujulikana.

Pole Mh. Adam Malima kwa hayo yaliyo kukuta
 
hahahhahahahaha hii kali asee
 

Mkuu soma habari vizuri kwenye gazeti la mwananchi maelezo ya waziri mwenyewe,anasema komeo la dirisha lilifunguliwa na si kuvunjwa kama unavyodai wewe,na kwa akili ya kawaida sana tu,ilo dirisha komeo lake litabenjuliwa liwaje kwa ndani kama huyo mtu hakuwa ndani ya chumba?maana kama ingekua kwa nje na dirisha lilifungwa basi ilo dirisha lazima lingevunjwa ndio mwizi aingie!
 
Naona Huyu Waziri anawaharibia Jina / Biashara wenye Hoteli!! Ni bora wakawa wazi na kuelezea Kisa Kizima ili Watu wajue na sio Kuiweka Hoteli kwenye Mazingira ya kuonekana ni Kichaka cha Uhalifu!! Ila pia Nadhani hii Hoteli Inamilikiwa Kifisadi kwani kwenye Tukio Kama hili Utaona itakuwa Vigumu sana kwa Mmiliki Kujitokeza Hadharani na Kueleza Ukweli ili Kulinda Biashara Yake!!
 
this is shame 4the minister like Adam, always Mungu akiamua kumpa adhabu mtu, hachagui wadhifa wake na ninajaribu kuamini haya kutokana na mazingira aliyoibiwa, najua kwa CCM ili litapita kimya2 kama la posho za ma-MB
 
Kaibiwa na chamgu doa, haiwezekani hotel kama hiyo mtu aingie bila kuwa noticed!!

Waziri anatemebea na SMG! JK bana...
 

Nilipokuwa JKT Mgulani miaka ya 70, tulikuwa tunapelekwa kulinda 'guard' sehemu nyeti, na tulikuwa tunapewa AK-47 au MP5 kufanyia ulinzi. Mara nyingi nilikuwa na wasiwasi kuwa tulikuwa target ya majambazi ambao wangeweza kutuvamia na kutunyan'ganya silaha. Katika hali hiyo ilibidi niwe macho sana hata kama muda wa zamu yangu ya ulinzi ulikuwa umekwisha. Hapa tahadhari ni kuwa usipokuwa muangalifu, silaha yako hiyohiyo inaweza kuwa chanzo cha madhara kwako na watu wengine pia.
 
Ngono tu...laptop tatu za nini na bunduki?afungue kesi na hotel itashinda coz vitu vya thaman kubwa huifadhiwa na hotel...lakn mizgo ukiingia nayo ni 'abiria chunga mzgo wako'.aseme ukwel 2msaidie aache kulewa kias cha kuvuliwa pete na watu kubomoa dirisha bila ya kuskia,si mmeskia kasema alikuwa kalala sebuleni?bonya hapa utamwelewa Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
 
Wizi wa Morogoro wataipata hachukuwi zaidi ya saa 24, alikisia tu, hakujuwa kuwa alipopindukia ni wrong number.

Nadhan Hii aibu Ni ya mwaka!! Kuanzia kwa Mwenye Hotel na Mwiibiwaji!! Sasa wewe Waziri Unatembea na Laptop 2 ili uonekane Unafanya Kazi sana au? Mimi Haingii akilini!! Haya kwenye sheria za kimataifa Kutembea na Hard Cash ni kitu ambacho kinashauriwa kiache Hata Huyu waziri Hajui Hilo? Pia Kuwa na Hela za Kigeni katika ziara za ndani ya Nchi ni za Sababu Gani? Vitu Vingi Hapa nchini wanataja kwa Dola ila with Equivalent Conversion Sasa yeye alikuwa na full dola ili aonekane Ni Expatriate? Duh Aibu!! Naona kama mwendo wenyewe ndio Huu; Huyu Waziri Hana Msaada wowote Kwenye Wizara!!
 
Dah hawa vibaka wa ajabu sana.............mie nlikuwa najua kuwa kibaka anakuwa kibaka kwa kuwa amekosa nyezo za kumfanya awe jambazi kamili. Sasa hawa wamewekewa bastola hapo wakaamua kuacha?? Kwamba wao hawataki kugraduate to Jambaziz?? Hata kama hajui kuitumia, inatosha kutishia tu kuliko kubeba yake majipanga makuuuuubwa!

Pole Muheshimiwa............. siku nyingine wasilisha mali zako reception.
 
Kwani alikwenda Morogoro kufanya nini? Au ndo alienda kula hicho kitimoto kilicho muibia?
 

Gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa alikuwa na Bunduki aina ya SMG. Hivi pamoja na sheria kuruhusu umiliki wa silaha, je raia ana haki ya kumiliki silaha za kivita kama SMG?
 

MwanajamiiOne. Hii ya vibaka yote ni cover up. Kitu kibaya zaidi ni pale unaposoma taarifa na kushindwa kuunganisha dots.


Kitu ambacho kinaleta maswali mengi zaidi ni
  1. Iweje mwizi aache bastola na SMG?, na je SMG inaruhusiwa kumilikiwa na raia?, I mean silaha ya kijeshi imilikiwe na raia?
  2. Naibu waziri Malima anasema alikuwa akiongea na mkewe na watu wengine kibarazani kwa simu, hii ina maana kuwa alikuwa na simu pale sebuleni ambayo nayo iliibiwa kabla ya kuingia ndani kwenda kuoga. Halafu Iweje chumba executive cha TZS 400,000 kwa usiku kikose Television ndani na kumfanya aende sebuleni kuangalia TV?, ina maana atakuwa alilala chumba cha low price ambacho hakina TV na kuomba risiti ya Executive room (huu ni ufisadi).
  3. Dirisha lilivunjwa, ila mbona picha zinaonesha dirisha lipo salama tu?, au hakulifunga?, na je nani ambaye alijua kuwa chumba hicho ni Naibu waziri akavamie?, je kuna wageni wengine nao waliibiwa?

My take: Naibu waziri ameibiwa na mtu aliyekuwa nae karibu sana tena chumbani na alikuwa anajulikana na walinzi na wafanyakazi wote. Mwizi wa vitu vya waziri ni wa jinsia ya kike iliyokuwa na motive ya short economic gain, ndiyo maana hakuwa na sababu ya kuchukua silaha kwani taaluma yake si unyang'anyi bali uchuaji wa ujira wa mwiha (sleeping with strange men allowance). Iweje atumie simu nje kabla ya kuingia ndani kwenda kuoga na kuvutiwa na taarifa na habari baadae kupitiwa usingizi sebuleni then simu iwe imefika chumbani yenyewe na kuibiwa?

Halafu yeye ameibiwa laptop simu na kila kitu kwa mtu yeyote katika hali hiyo hatakuwa na muda wa kujua nini kimeongewa wapi kwani focus itakuwa ni kuhakikisha mwizi anapatikana haya mengine ya mtandao ya kijamii inasema nini angekuja kuyajua siku zifuatazo, sasa kukanusha kuwa yeye hakuwa na mwanamke ni wazi kuwa hii ni COVER UP strategy baada ya mtu mzima kuumbuka. Ni kweli kuwa mtu aliyemwibia alikuwa na taarifa nae kwani ndiye alikuwa nae chumbani.

Halafu kwa nini wasiruhusu waandishi wa habari kwenda eneo la tukio chumbani?, kuna faragha gani iliyokuwepo baada ya kuibiwa?. Mbona akina Dr Slaa na Tarab walipowekewa vinasa sauti Dodoma waandishi waliruhusiwa kuingia na kuchua picha?. Hi ni total COVER UP ndiyo maana hata mkuu wa mkoa na viongozi wengine wanajiweka kando kwa kusema wao si wasemaji, maana sooner or later ukweli halisi utajulikana na kuwaumbua zaidi.

Kwa COVER hii maana yake ni kumuharibia mwenye hotel biashara. Mwenye Hotel hiyo ajue kuwa kusingizia dirisha limevunjwa na vitu kuibiwa ni negative PR na ajiandae kukosa wateja wengi sana kwa ajili ya funikafunika ya maovu ya kiongozi mmoja. Hao walinzi wanawaonea bure kabisa na kwa kuwa wanataka kazi watatizhwa wakubali ili wasifukuzwe wakati Mwizi halisi wa vitu hivyo kaletwa na muheshimiwa mwenyewe na huenda walikuwa wakivinjari for the rest of the week. Mwenye hotel asikubali hii kitu itamcost sana kurudisha imani kwa wateja kuwa hotel hiyo ni salama.
 
Hii hata mimi sijaelewa, SMG ni silaha ya kivita...labda wanaojua sheria juu ya umilikaji wa silaha za moto watufafanulie, Vile vile sielewi kwanini naibu waziri atembee na silaha aina ya SMG......?? , kwa style hii tusije kushangaa labda wapo wengine wanatembea na zaidi ya SMG, Nazungumzia ile kitu inaitwa LMG (Light machine gun)

Gazeti la Mwananchi limeripoti kuwa alikuwa na Bunduki aina ya SMG. Hivi pamoja na sheria kuruhusu umiliki wa silaha, je raia ana haki ya kumiliki silaha za kivita kama SMG?
 

Simple Thinking Yaani Ina Maana Huyo Kibaka alikuwa anasali siku zote na Kuja na kukuta Muheshimiwa Kalala sebuleni? Duhh Pia hii ni Kali!! Naona wakudanganywa Hapa ni watoto wa Check na Kia!!
 
Naomba wataalamu wa mambo ya computer watupost picha ya ile clip ya video kwenye dakika 2:30 tutapata majibu yote ya hili jambo. Ukiangalia vizuri kwa jinsi lile dirisha lilivyovutwa inaonyesha dhahiri ya kuwa lilibenjuliwa kutoka ndani. Sisi tunaongalia CSI kila siku atudanganywi kirahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…