Naibu Waziri Mkuu: Magari ya Serikali yafungwe mfumo wa gesi asilia

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko ameelekeza utaratibu wa kubadili mifumo ya magari kutumia gesi asilia uanze na magari ya serikali na kuwa vituo zaidi vijengwe ili kupunguza matumizi ya mafuta.

View attachment 2749046
Naomba kuuliza kwa yeyote mwenye uelewa..!! Hivi kubadili system ya gari kutoka ya mafuta na kuja ya gesi, ni kwa magari yote ya mafuta ya petroli na diesel au petroli pekee..!!??
 
Sawa ndugu naibu waziri mkuu. Lkn lengo lako ndugu naibu ni nn hasa?

**Kwamba tutumie gesi yetu? (Siyo yetu tena, Kikwete alimuuhzia machina).
**Ni nafuu kuliko petrol na diesel? (Kwa uhaba huu wa dola tulionao Sasa hivi bei ya gesi itakuwa sawa na ya petrol na diesel).
 
Mjomba wangu Maja kama hajastuka kwamba kapwaya kwenye hii "move" ya bimdashi basi atakuwa na kichwa kizito sana. Ankoli mama kaona unapwaya shtuka ankoli.
 
Hapa ndipo tutajua kuwa kweli huyu Mzee ni mwizi namba moja duniani kama hili dili litashindikana
 
Utashangaa wanayafunga kwa Bei za Ajabu alafu baada ya miezi kadhaa hayafanyi kazi au kuachana na mfumo huo na kurudi walipotoka....

Hii nchi haijawahi ku-lack good ideas; bali implementation ya hizo ideas is for their own benefit...., na kilichokusudiwa kumsaidia mwananchi kinaishia kwenye makabrasha....

Anyway Idea hii nilisha-suggest siku kadhaa zilizopita...
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko ameelekeza utaratibu wa kubadili mifumo ya magari kutumia gesi asilia uanze na magari ya serikali na kuwa vituo zaidi vijengwe ili kupunguza matumizi ya mafuta.

View attachment 2749046
Kwanini wasianze kwa utaratibu wa kuanza kuagiza magri yenye mfumo wa gas kila wanapoagiza magari mapya? Hii ya kufunga mfumo wa gas naiona ni mzigo mwingine mkubwa sana serikali inaenda kuuingia ambapo watafunga hadi magari ambayo ni almost expired.
Gari linafungwa mfumo wa gas leo, mwezi ujao linawekwa mnadani, halafu linaagizwa gari jipya, likifika linaenda kufungwa mfumo wa gas.
Hili dili linaenda kuwa EPA na Kagoda nyingine hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…