Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama hujui jambo bora kukaa kimya na kujifunza kuliko kuonesha ujinga mbele ya watu. Shida ya Watanzania kama. jambo hulijui unahisi halipo.?Acha uongo wewe,kama wewe ulidanganywa,acha kuwadanganya wengine
Bundi (bibi wa jf) alishalia june au july 2023 🤣🤣🤣🤣🤣🤣Ni njia ya kisiasa ya kummaliza waziri mkuu bila kuvunja serikali.
Nawasalimu Waungwana wa JF,JE KATIBA INASEMAJE KUHUSU CHEO HIKI?
Cheo Cha kimkakati zaidi.Ni cheo cha kutongozea kura kanda ya ziwa au kumpiga pin Kasimu
Anajua hatuwezi kuhojiNa pesa pia
Sawa mzee wa TECSababu mgalatia mwenzio na msukuma,angekuwa muislam hapo mlivyo na chuki kkenge nyie
Samia kiboko, naona kaamua kuondoa uchafu wa magufuli
Mabadiliko haya ni kuongeza ufanisi au kuelekea 2025?
Kweli Draft ,ni kama liko wazi hv ,na kama unaeza changanya cards vzr hili baraza lina mtu atakayekuja shika kijitiHii warmup ya 2025, draft liko wazi sana.
Kweli Draft ,ni kama liko wazi hv ,na kama unaeza changanya cards vzr hili baraza lina mtu atakayekuja shika kijiti
We ndo umejibu Jibu LILILO SAHIHI SANA kwani kaonekana hatoshi kwenye nafasi yake ila kumtengua kutasababisha sintofahamu Nyingi ikiwemo kuvunjwa kwa baraza zima la mawaziri na serkali yote kwa ujumla hio ikiendana sawa sawa kabisa na kuwajibisha Tume ya uteuzi wa waziri mkuu kuteua Waziri asiyetosha na hii itamtia doaNi njia ya kisiasa ya kummaliza waziri mkuu bila kuvunja serikali.
Majukumu hayatajwi kwenye kitabaJamani hili Taifa letu tunaendaje? Vyeo vinakuwa vingi Sana. Ina maana ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa kubwa sana mpaka utendaji unakuwa Mdogo na kuamua kuiongeza nguvu kumpa msaidizi vipi? Vipi wizara zilizo chini yake?
Ningependa kujua majukumu ya Naibu Waziri Mkuu yatakuwa yapi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri na Muungano wa Tanzania.
---
hivi nyie vijana mbona mnaakili mgando hivi? hata historia ya nchi hamuijui? harafu kutwa kucha kupiga kelele humu.Hapa staki kuongea sana kwa sabu sielewi mambo ya Kisheria
Naongelea hii nafasi aliyopewa na kuteuliwa mh Dotto Biteko kuwa Naibu waziri mkuu, sjawahi kuisikia na wala kuona tangu nchi yangu ipate uhuru
Hii inamaana gani? Ni mh Rais kuogopa kulivunja bunge kwa kutokumtengua waziri mkuu?
Au lipo kikatiba?
Tafadharini Waheshimiwa sana viongozi wetu meza kuu Maadimin wetu Jf
Msiunganishe huu uzi
Majaliwa anapwayaMpaka leo hii, hiki cheo kiliwahi kushikiliwa na watu 2 tuu tena kwa sababu maalumu sana na nyeti, na zenye maslahi mapana kwa taifa.
1. Dr. Salim Ahmed Salim.
Salim alipewa cheo hiki 1986 mpaka 1990, kwasababu aliwahi kuwa Waziri Mkuu kwa mwaka mmoja enzi za Mwalimu Nyerere (Baada ya Kifo cha Sokoine), hivyo baada ya Rais Mwinyi kuingia akaona ni Busara Waziri Mkuu wake aliyemteua Joseph Sinde Warioba awe na Naibu ambaye ni Salim.
2. Augustino Lyatonga Mrema
Akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Augustino Mrema alitumia ujuzi wake kama KACHERO WA USALAMA WA TAIFA, kudadisi na kukamata wezi na wala rushwa katika kila wizara ya Serikali aliyogundua mambo si shwari.
Hali hiyo ikawaudhi baadhi ya mawaziri wenzake serikalini. Wakamwambia "MREMA USIVUKE MIPAKA YAKO, Wewe ni waziri kama sisi na huwezi kuingilia mambo ya ndani kwenye wizara zetu bila kujadiliana nasi kwanza." Mrema anasema alikomaa nao, na ndipo Rais Mwinyi akagundua dhamira yake njema.
Rais Mwinyi mnamo mwaka 1992 akamuongezea cheo kipya Mrema. Akamteua kuwa NAIBU WAZIRI MKUU.
1993, Mrema alipopewa Unaibu Waziri Mkuu anasema "wenzangu walianza kuniogopa na kuniheshimu. Hata kama wanaenda sehemu walikuwa wanalazimika kusimama kwanza ili kupisha msafara wenye ving'ora wa Naibu Waziri Mkuu."
Akiwa Waziri wa Mambo ya ndani na Naibu Waziri Mkuu alishughulika na kila aina ya ubadhirifu, wizi na magendo kwa kadri alivyopata taarifa. Akawa waziri maarufu sana kwa wananchi mijini na Vijijini.
"Rais Mwinyi kila akirudi kutoka mikoani alikua akiniita na kuniambia Mrema nimetoka kwenye ziara, wananchi wanakusalimia sana. Unafanya kazi nzuri," alinisimulia Mzee Mrema katika mahojiano hayo ya MSUMARI WA MOTO.
Miongoni mwa mambo yaliyompa umaarufu Mrema zama hizo za uwaziri wake wa mambo ya ndani na Naibu Waziri mkuu ilikua ni kuhamasisha ujenzi wa vituo vya polisi kwa nguvu za wananchi ili kuimarisha ulinzi lakini pia "Tajirika na Mrema" - UTOAJI WA ZAWADI KWA WATU WANAOFICHUA WAHALIFU.
Nani angekubali kukaa na taarifa za mwizi au muhalifu wakati ana uhakika akimfichua atapewa zawadi?
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Swali ni je, Biteko kateuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu kwa merits alizonazo, ama ameteuliwa kwa sababu Majaliwa ameonekana anapwaya kwenye u Waziri Mkuu?
Na hii ndio sababu kubwa ambayo watu hawajui.hii political movie haina uhusiano na Majaliwa kabisa.Naibu waziri mkuu kaja kubalance influence ya kanda ya Ziwa!! Lissu na Mbowe wameivuruga lake zone mbaya kabisa CCM inapumulia mashine!!
Biteko amesoma na hajaunga unga katika elimu yako hawezi Fanya mambo ya hovyi kama ya makonda.Kuna dalili Biteko atakuwa na nguvu kama Makonda zama zile
Hii nchi katiba inavunjwa hakuna wa kuhoji, hicho cheo hakipo kikatiba ndiyo maana hata Jaji Mkuu muda wake ulishapita lakini yupo kwa kuvunja katiba