Kuna kitu hapo hakiko sawa kwenye uteuzi wake, hofu yake inatokana na siri alizonazo mwenyewe! Inawezekana kuwa hakutarajia kupata uteuzi, lakini alikuwa na muda wa kujiandaa angalau kukariri kiapo alichotakiwa kuapa.
Kuwa ni msomi mzuri, hilo nalipinga kwani kuna kundi kubwa tu la watu wenye Degree zenye rakiri za dahahabu huko Serikalini, lakini wanasafiria nyota za watendaji wa chini yao, wakati wao wenye mamlaka hamna kitu.
Kuna baadhi ya Wizara ukizitembelea na kubahatika kupata mawili matatu na watendaji wakuu, unagundua kabisa kuwa watu wanalipwa mshahara wasioustahili. Hii ifike mwisho sasa ili nafasi zijazwe na wanaostahili iwe kwa elimu, uzoefu, uwezo, umahiri, uwajibikaji na unyenyekevu n.k.