Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Hakuna uchawi hapo,jamaa kitete na uoga vimezidi sasa anatafuta visingizio.
 
Hao nao hawana wakovu ni wanasiasa was Chadema.
 
Na Ndo mana mwarabu mmoja alikuwa na uwezo wa kuswaga kundi la mbanga 300 kutoka tabora mpaka bagamoyo zikiwa ndani ya minyororo.
Tena kwa Unaa unakuta njiani zinajipendekeza kwasasbu "Maandiko" ndivo yalivowafundisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upendo una nguvu ambazo chuki haikupi.

Mfano kwa kuwachukia hao wala keki yako kumebadilika nini mpaka leo.

Msamalia mwema alimpomsaidia majeruhi barabarani hakujiuliza kama huyu ni class gani, mla keki au la.

Jaribu kuwa na compassion na kusamehe watu hata wanaokuumiza, utashangaa sana matokeo.

Achana na hiyo mifano ya wafungwa 300.
 
Hakuna aliyeumbuka. Kwani wewe hukosei? Mbona akina Mathawe wanaongea kwa kithethe au akina Mura wanaoweka ra kwenye kila la bila kusahau akina Rwadai wanaosifika kwa kuweka la kwenye ra. Acheni mambo ya kijinga. Waziri hakuteuliwa kusoma habari bali kuongoza wizara. Mbona kukosea ni suala la kibinadamu.

Hapa aliyeumbuka hakuna kama yupo ni wale wanaoshupalia makosa ya kawaida kama haya. Kwanza, mhusika hakushindwa kula kiapo bali alikosea maneno machache. Pia hii si kasoro ya kujadiliwa kiasi hiki zaidi ya wivu na chuki za kawaida hasa kwa wale wasiompenda Magufuli
 
Uchawi unapenya hata makanisani na misikitini kwahyo usishangae hapo ,usione watu wamekaa na suti zao,wanatunguli zao mfukoni zinapumua tu.
 
Unathibitisha vipi kama ni nguvu za giza mkuu?
Huyu siyo wa kwanza kutoka Lindi anafanyiwa ndumba za namna hii.

Yupo dada mwingine aliukosa ubunge wa viti maalumu hivi hivi kwa kukabwa koromeo wakati anajieleza!
 
Hili zengwe, kapigwa kipapai, hukuona yule mgombea udiwani wa posta alikiwa anashindwa kutamka maneno yake, mapka akasema hii uchawi
Na naona sasa hivi ndio imekuwa habari ya mjini vipapai vya aina hii.
 
If there. Is anyone to blame on this saga basi ni jiwe la kisukuma la chato, hakutumikia akili ku- handle hii issue
 
Kati ya wote waliokuwepo pale wangapi hawatumii nguvu za giza tuanzie hapo?
 
Labda viongozi wa dini hawaelewi kwa nini huwa wanaalikwa kwenye shughuli muhimu za serikali.

Ngoja niwakumbushe;

Nyie viongozi wa dini uwepo wenu unamaanisha utakaso wa kiroho na mwili katika eneo husika na kwamba shetani hatapata nafasi ya kumdhuru yoyote.
Inapotokea nguvu za shetani zikapenya na kutia dosari shughuli husika maana yake viongozi wa kiroho mliokuwepo imani zenu ni haba kiasi cha kumruhusu shetani kufanya atakavyo.

Nimeshangaa leo Naibu waziri " anapagawa" kwenye kula kiapo viongozi wa dini yangu ya Kristo Yesu badala ya kukemea wao wakawa wanacheka.

Next time watu wa itifaki mnapoalika viongozi wa dini basi leteni walawi kweli siyo hawa wenye harufu ya siasa.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote.

Maendeleo hayana vyama!
Unajuaje ni nguvu za giza na si mtu ana matatizo ya macho anahitaji miwani tu?
 
Haya ndo madhara ya kutokuwepo mchujo wa kupata wabunge,watu wamepita bila kupingwa hawajapitishwa hata kwenye moto ilitupate watu pure for public tasks.
 
Labda viongozi wa dini hawaelewi kwa nini huwa wanaalikwa kwenye shughuli muhimu za serikali.

Ngoja niwakumbushe;

Nyie viongozi wa dini uwepo wenu unamaanisha utakaso wa kiroho na mwili katika eneo husika na kwamba shetani hatapata nafasi ya kumdhuru yoyote.
Inapotokea nguvu za shetani zikapenya na kutia dosari shughuli husika maana yake viongozi wa kiroho mliokuwepo imani zenu ni haba kiasi cha kumruhusu shetani kufanya atakavyo.

Nimeshangaa leo Naibu waziri " anapagawa" kwenye kula kiapo viongozi wa dini yangu ya Kristo Yesu badala ya kukemea wao wakawa wanacheka.

Next time watu wa itifaki mnapoalika viongozi wa dini basi leteni walawi kweli siyo hawa wenye harufu ya siasa.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote.

Maendeleo hayana vyama!
Hapa kazi tu... pale nguvu ya pombe inapotumika kuliangamiza taifa kwa kisingizio cha maendeleo hewa
 
Back
Top Bottom