Tanzania viongozi wa dini wote wanao alikwa kwenye shughuli za kiserikali basi huwa ni "WATAPIA TUMBO na MARAFIKI WA SHETANI", huwezi kukuta "SHEIKH PONDA au ASKOFU MWAMAKULA au ASKOFU BAGONZA" amealikwa kwenye hafla za serikali maana muda wowote kwenye hio hafla wanaweza "KUCHOMOA BETRI"
Pili, baada ya Jiwe kuona ametereza kumchagua huyo Naibu Waziri Wa Madini na amepata wazo jingine la kumteua mwingine kwenye hio nafasi, ila majina ndio yamesha tangazwa kwa wananchi, huyo Naibu Waziri Wa Madini akafanyiwa "MAKUSUDI" form yake kuwekwa maandishi madogo sana yaliyo vurugwa vurugwa pamoja na kuchanganyiwa "HERUFI ZA KICHINA" ili ashindwe kusoma halafu mabadiliko yafanyike.
Haiingii akilini DED ashindwe kusoma "PARAGRAPH MBILI" za kiswahili, wakati "MBUNGE MSUKUMA" mwenye elimu ya "DARASA LA SABA (FAILURE)" anaweza kusoma Bajeti Za Serikali na Sheria huko bungeni vizuri na akazielewa.
Watu wanamcheka na kumkebehi kwa kushindwa kusoma kiapo, ila sio jambo jema kabisa, yule bwana ataathirika kisaikolojia, anapaswa kupewa moyo na counselling. Sio kumcheka au kudhihaki. YULE NI BINAADAMU PIA."