Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Sawa tumeopokea uzi tayr


Sasa mkuu tetema ile angepiga vitu ingekuwa balaa na nusu


Ujue mzigo wa K'vant ili-ukupe confidence inatakiwa muhusika uwe comfortable..
Comfortability unaipata ukishapiga shot mbil za kwanza.yaan mwepes..weng hyo wanatumia.hata wnaamuzik..sasa wao ndo huwa wnaaharib.wanatumia cocain au bang...sasa..bangi ndo yenyew yaan hulew ila unachangamka..na ndomana watu wanaotumia bang ni weng kuliko unavyofkiria na ni watu wazito kabisa ambao huwez wazania
 
Ulozi tu
Hii sasa ni kali.

Awali Naibu waziri wa fedha ilibidi arudie kula kiapo zaidi ya mara 5 kwa sababu sehemu iliyoandikwa "Baraza la Mawaziri" yeye alitamka " Baraza la Mapinduzi"

Kali ya mwaka ni huyu Naibu waziri wa madini Trancis Ndulane ambaye amekuwa akisoma kiapo huku akitetemeka na hivyo kuwekwa pembeni ili waapishwe wengine.

Wakati wa hotuba yake Rais Magufuli amesema atateua Naibu waziri mwingine wa madini baada ya Francis kufeli kula kiapo.

Sijajua manaibu waziri hawa wana mchecheto gani!

Maendeleo hayana vyama!
 
Boss wao ni mungu mtu wao ndo maana wanamuogopa sana akisimama mbele yao imebaki kumuabudu tu
 
Nimecheki mkuu tena ana Masters ya Finance hahahaa
Tena master ya Mzumbe..[emoji41]
Screenshot_20201210-075839_Drive.jpg
 
Yaani huyo jamaa amechemsha hadi akaambiwa akaketi!

Hivi vyeo vingine vya "kupewa" ndiyo matatizo yake
Mtu hajawahi hata kukaimu ukuu wa idara, ghafra bin vuu unampa cheo ambacho hakutarajia. Uzoefu ni muhimu hata ukiwa msomi. Si aibu kwa mshindwa kuapa tu, hata kwa mteuzi.
 
Labda viongozi wa dini hawaelewi kwa nini huwa wanaalikwa kwenye shughuli muhimu za serikali.

Ngoja niwakumbushe;

Nyie viongozi wa dini uwepo wenu unamaanisha utakaso wa kiroho na mwili katika eneo husika na kwamba shetani hatapata nafasi ya kumdhuru yoyote.
Inapotokea nguvu za shetani zikapenya na kutia dosari shughuli husika maana yake viongozi wa kiroho mliokuwepo imani zenu ni haba kiasi cha kumruhusu shetani kufanya atakavyo.

Nimeshangaa leo Naibu waziri " anapagawa" kwenye kula kiapo viongozi wa dini yangu ya Kristo Yesu badala ya kukemea wao wakawa wanacheka.

Next time watu wa itifaki mnapoalika viongozi wa dini basi leteni walawi kweli siyo hawa wenye harufu ya siasa.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote.

Maendeleo hayana vyama!
Sikuhizi viongozi wa dini ndio wabeba tunguli kwenye mazindiko, unategemea upako wa roho wa kweli utoke wapi?
 
Leaders are born not made. Kuna utofauti mkubwa sana kati ya kiongozi na mwanasiasa.

Viongozi halisi waliozaliwa kuongoza wapo wametulia wanafanya mambo yao mengine, wengi tunaowaita Viongozi ni wanasiasa tu.

Seminars za uongozi hazikufanyi kuwa kiongozi kama hukuzaliwa kuwa kiongozi.

Viongozi ni wachache sana na wanaelewa mipaka yao kuepusha kutumia uwezo wao vibaya.

Hata kwenye matahasisi huko maofisini kwenu, yupo mkurugenzi ambaye unaona kabisa huyu hii nafasi haimfai kabisa maana hana sifa za kuwa kiongozi ila ni vyeti tu.




Sent from my E2333 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom