Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Naibu Waziri mteule wa Madini, Francis Kumba Ndulane ashindwa kusoma kiapo kwa ufasaha, uteuzi wake watenguliwa

Hii imetokea leo ambapo naibu waziri Fransis Ndulano alishindwa kusoma vizuri hati ya kiapo akapewa nafasi ya kurudia bado akawa anakwamakwama hadi akaambiwa akakae kwenye kiti chake. Sijui ataapa siku yingine au ndio kibarua kimeota nyasi. Sasa sijui ni uoga au wamemroga.
Fundisho:
Tuwafundishe watoto wetu kujiamini pamoja na elimu walizo nazo confidence ni muhimu.
Mkuu mi mwenyewe na tatizo hilo la kuloose confidence na niko mwaka wa mwisho NINA PRESENTATION na miaka ya nyuma nilikuwa na kimbia presentation.Sasa wakuu nawezakufanyaje?
 
Labda viongozi wa dini hawaelewi kwa nini huwa wanaalikwa kwenye shughuli muhimu za serikali.

Ngoja niwakumbushe;

Nyie viongozi wa dini uwepo wenu unamaanisha utakaso wa kiroho na mwili katika eneo husika na kwamba shetani hatapata nafasi ya kumdhuru yoyote.
Inapotokea nguvu za shetani zikapenya na kutia dosari shughuli husika maana yake viongozi wa kiroho mliokuwepo imani zenu ni haba kiasi cha kumruhusu shetani kufanya atakavyo.

Nimeshangaa leo Naibu waziri " anapagawa" kwenye kula kiapo viongozi wa dini yangu ya Kristo Yesu badala ya kukemea wao wakawa wanacheka.

Next time watu wa itifaki mnapoalika viongozi wa dini basi leteni walawi kweli siyo hawa wenye harufu ya siasa.

Mungu wa mbinguni awabariki nyote.

Maendeleo hayana vyama!
Umetumia parameta gani kuamini kulikuwana ndumbanangai kwenye kile kiapo?

Kila mtu ana kiwango chake cha mchecheto.

Wewe ukiona sketi hata kama ulikuwa unatapika unasitisha kwanza mpaka ipite
 
Hii sasa ni kali.

Awali Naibu waziri wa fedha ilibidi arudie kula kiapo zaidi ya mara 5 kwa sababu sehemu iliyoandikwa "Baraza la Mawaziri" yeye alitamka " Baraza la Mapinduzi"

Kali ya mwaka ni huyu Naibu waziri wa madini Trancis Ndulane ambaye amekuwa akisoma kiapo huku akitetemeka na hivyo kuwekwa pembeni ili waapishwe wengine.

Wakati wa hotuba yake Rais Magufuli amesema atateua Naibu waziri mwingine wa madini baada ya Francis kufeli kula kiapo.

Sijajua manaibu waziri hawa wana mchecheto gani!

Maendeleo hayana vyama!
Sifa tu za JPM kwan yeye mara ngapi amegurugusa akiongea kiingereza., ile inatokezea yule ni binadamu yawezekana tension mbele za watu pale ndio shida
 
Naunga mkono hawa viongozi wa dini ni waganga njaa tu,hawana Mungu wa kweli. Haiwezekani ndumba ipenyeze mahala walipofanya sala.
Hamna ndumba iliyo penya kaka,jamaa alikuwa na kitete,
Tuseme ukwe ata humu mpo wengi ambao ingewatokea .
 
Ukijaribu kufanya utafiti utagundua kwamba wapo watu wengi sana, wakubwa kwa wadogo, wenye elimu za ngazi kuanzia msingi mpaka chuo kikuu ambao hawawezi kusoma kwa mtiririko wa moja kwa moja.
Pili, ni muhimu kujua kwamba, kuwa na vyeti ni jambo moja, kukariri jingine na mwisho kuwa hata wajinga hupewa vyeo kutegemea utaratibu na siasa (hapa simaanishi kuwa aliyeshindwa kuapa ni mjinga).
 
Hii sasa ni kali.

Awali Naibu waziri wa fedha ilibidi arudie kula kiapo zaidi ya mara 5 kwa sababu sehemu iliyoandikwa "Baraza la Mawaziri" yeye alitamka " Baraza la Mapinduzi"

Kali ya mwaka ni huyu Naibu waziri wa madini Trancis Ndulane ambaye amekuwa akisoma kiapo huku akitetemeka na hivyo kuwekwa pembeni ili waapishwe wengine.

Wakati wa hotuba yake Rais Magufuli amesema atateua Naibu waziri mwingine wa madini baada ya Francis kufeli kula kiapo.

Sijajua manaibu waziri hawa wana mchecheto gani!

Maendeleo hayana vyama!
Haya ndiyo madhara ya kupata wabunge kwa mtutu wa bunduki na maji ya washawasha
 
Kilwa bana sijui kuna nini Mara kulikua na Mbunge sijui ana jina la utani Bwege aisee tunguli hizi hazipendi maendeleo yao
 
Mtu hajawahi hata kukaimu ukuu wa idara, ghafra bin vuu unampa cheo ambacho hakutarajia. Uzoefu ni muhimu hata ukiwa msomi. Si aibu kwa mshindwa kuapa tu, hata kwa mteuzi.
Umeambiwa jamaa alikuwa DED wa Ifakara!
 
hao viongozi wwnyewe wa dini wanamuhubiri kristo huku wakitegemea hirizi ya shetani kufanya fake miracles case study hapa ni yule mfuga misukule aliyempora Halima ubunge
 
Mkuu mi mwenyewe na tatizo hilo la kuloose confidence na niko mwaka wa mwisho NINA PRESENTATION na miaka ya nyuma nilikuwa na kimbia presentation.Sasa wakuu nawezakufanyaje?
Hii inaathiriwa na makuzi pamoja na mazingira ni ngumu kuibadilisha kwa haraka.
Hakikisha siku ya presentation usiwaangalie machoni bali waangalie kwenye nywele yaani juu ya vichwa hii itasaidia kidogo
 
Ningepata nafasi ya kumuona Rais leo hii ningemshauri asimtumbue NW Madini, mtu mzima yule tena msomi hawezi kushindwa kusoma sentensi mbili hizo.
Kuna tatizo sehemu, waswahili tuna mambo ya kijinga sana.
Afu jiwe amesahau yy mwenyewe "alizimika" Lindi huko!
 
Huwezi tengeneza tukio kama hili,hii ni fedheha kubwa sana kwa taifa letu. Tukio kama hili huwa linatazamwa dunia nzima.
Nadhani dunia nzima inamshangaa Maalim kwenda kuapa wakati wenzake/mashabiki wake bado hata hospitali hawajatoka au kupona majeraha yale ya risasi.
Tukio la waziri kushindwa kusoma sio zito kama la Maalimu kuapishwa. Mezani yako naonani mbovu
 
Mimi najiuliza sana!

Hivi selikali huwa wanatengeneza vimatukio ili kutusahaulisha mambo flani flani?

Hebu ona mjadala wote wa ACT na Maalimu Seif umekufa kabisa.
Haya ni matumizi sahihi ya jicho la tatu. Hongera kwamatumizi sahihi ya ubongo.
 
Kumbuka alishaapa bungeni, pili aliwahi kuwa Mhasibu wa Tanroads Lindi, tatu alikuwa mkurugenzi wa Wilaya.

Hii ni "ndumba dot com" period.
Tabia za watawala
(1) myime mtu / watu elimu washindwe kuzitambua haki zao. (2) tengeneza tatizo kisha litatue.
(3) matukio. (Jana ilikua siku ya uhuru yapo mengi yaliyopaswa kufanyika, huwezi zungumza habari za uhuru ukaacha uchaguzi huru.)
 
Back
Top Bottom