Uzalendo kwa kununua toilet paper holder kwa laki 5?? Tuache utaniKwenye miradi ya serikali usipokula na wanasiasa tegemea hujuma na majungu. Ila wazalendo na wataalamu wenye misimamo huwa hawafiki mbali.
Kuna wakati ni bora usimamie ukweli na uhalisia kuliko kulamba miguu ya watawala wasiojua chochoteJAMAA YUKO PERFECT... HESHIMA KWAKE.
Hili jamaa nalifahamu tangu A level Minaki halikuwa na ushirikiano na watu na lilikuwa lichafu balaa na limeaoma likiwa lizee tuHuyu jamaa sura yake ilivyokaa kaa tu anaonekana na disorder flan sijui unaibu waziri kaupataje
HakunaHii nchi tunatengeneza miungu watu na sio viongozi, hapo kuna kosa gani la kumfukuza mtu na kumsweka rumande?
Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel ameagiza kuondolewa madarakani kwa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa wizara hiyo, Paul Koroso kutokana na mgogoro ulioibuka katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh2.9 bilioni.
Dk Mollel pia ameagiza Koroso aswekwe mahabusu akidai amemtolea majibu na lugha ya kijeuri kuwa “hajali lolote hata akifukuzwa kazi”.
Dk Mollel ametoa maagizo hayo Julai 5 akiwa mjini Nansio Ukerewe alipofika kutatua mgogoro uliobuka kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi hospitali ya Rufaa ya mkoa katika kisiwa hicho ndani ya Ziwa Victoria.
"Kutokana na changamoto zilizojitokeza kwenye mradi huu, Koroso utakoma kuwa mkuu wa Idara ya Ujenzi Wizara ya Afya. Katibu mkuu atamteua mkuu mpya wa idara ambaye atakuja kusimamia mradi wa Ukerewe," alitangaza Dk Mollel.
Pamoja na viongozi na wataalamu wa Wizara, mkoa na wilaya, kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi wa CCM, halmashauri na mkandarasi Suma JKT.
Miongozi mwa malalamiko yaliyotolewa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe dhidi ya Koroso ni kutowashirikisha viongozi wa wilaya na halmashauri katika utekelezaji wa mradi huo.
"Ofisi ya DC, halmashauri na CCM Wilaya ya Ukerewe hawakushikishwa katika utekelezaji wa mradi huu," Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Denis Mwila alimweleza Dk Mollel.
Muda mfupi kabla ya amri ya kuswekwa mahabusu, Koroso alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa Serikali ingeokoa kati ya Sh180 milioni hadi Sh260 milioni iwapo ungetekeleza mradi huo kwa mtindo wa Force account (kutumia nguvu za wananchi) badala ya ukandarasi.
Kiwango kilichotajwa na Koroso kilitofautiana na kiwango cha Sh600 milioni kilichotajwa na mhandisi wa mkoa wa Mwanza, Chagu Nghoma.
Kutokana na tofauti hiyo, Dk Mollel akamtaka Koroso kutoa ufafanuzi, ndipo akasisitiza kuwa hesabu zake ndizo sahihi kwa mujibu wa kanuni na msingi wa kitaaluma na kwamba yuko tayari kuchukullwa hatua yoyote.
"Mheshimiwa Naibu Waziri, kiwango nilichotaja kimezingatia kanuni, vigezo na hesabu za kitaaluma; nitaendelea kusisitiza hilo hata kama ukinifukuza kazi sitajali," alisema Koroso.
Kutokana na kauli hiyo, Koroso aliyeketi jirani na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Ukerewe akajikuta anawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa mahabusu.
Chanzo: Mwananchi
Hana kosa, acheni kuonea watu.Hana nidhamu hata kidogo...
Kong'oa mtu jino unadhani ni kazi nyepesi.Ifike wakati sasa wanataaluma wajitambue kama alivyo Eng Paul Korosso
Wanasiasa wakishalambaga asali wanakuwaga wajinga sana, tusiwavumilie tuwape za uso
Dr Mollel hata kung'oa mtu jino hawezi japo ndio fani yake
Kuna ubabe gani kwenye majibu? Huyu naibu waziri kilaza anaamrisha mtu awekwe ndani kwa kosa gani? Jaribu kutumia akili hata kidogo.
Wewe ungeanza kutumia akili zako tu ungeona tatizo la huyo KorosoKuna ubabe gani kwenye majibu? Huyu naibu waziri kilaza anaamrisha mtu awekwe ndani kwa kosa gani? Jaribu kutumia akili hata kidogo.
Kama unajua mawaziri wanasimamia Sera, mamlaka za Makatibu wakuu kutekeleza Sera zinatokea wapi? Ukisoma hiyo taarifa ya Mwananchi imesema Wazir ameagiza Katibu Mkuu atekeleze jambo kwa maslahi aliyoyataja hapo, maana yake kuna mgogoro ambao umepelekea kusuasua kwa kazi.Hana hata mamlaka ya kumfuta cheo. Kama ana hayo mamlaka basi anaweza kumpandisha cheo mtumishi yeyote wa umma. Mwenye mamlaka hayo ni Katibu Mkuu wake ambae ndie Mtendaji Mkuu wa Wizara. Na uamuzi wake unaweza kukatiwa rufaa katika Tume ya Utumishi. Watu hua hawakati rufaa kwa sababu mabadiliko hayo ya wadhfa yalikuwa hayaathiri mishahara yao. Lakini sasa kwa hii sheria ya Mwigulu, watu watakata tu rufaa.
Mawaziri sio watendaji katika wizara. Wao jukumu lao ni kusimamia sera za wizara.
Amandla...
Unless kuna taarifa hazijaandikwa lakini ukisoma hiyo habari nashindwa kuelewa kilichomfanya Koroso kuingiza hayo maneno "sijali hata ukinifukuza kazi" katika maelezo yake. Kama issue ilikuwa kujadili tofauti ya figure ambayo ingeokolewa kati yake na Engineer wa Mkoa yeye angestick kwenye maelezo yake ya kitaaluma tu. Sijaelewa ya kufukuzana kazi yaliingiaje pale.kabla ya kusona habari yote nilijua huyu jamaa kamjibu waziri vibaya lakini baada ya kusoma wala sioni kosa lake,kwa sababu yeye amesema yupo tayari kufukuzwa kazi kwa sababu ana uhakika na usahihi wa maelezo aliyotoa,Shida ni kwamba hii serikali ya CCM haipendi watu wanaojiamini,wanataka watu wa ndio mzee
Hili jambo siyo la kushabikia"Kutokana na kauli hiyo, Koroso aliyeketi jirani na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Ukerewe akajikuta anawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa mahabusu. "
🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓
Jamaa alijifanya mbabe bila kutambua kuwa ameketi sehemu na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya matokeo anawekwa chini ya ulinzi!
UCHAWI upo.Huyu jamaa sura yake ilivyokaa kaa tu anaonekana na disorder flan sijui unaibu waziri kaupataje
Milion 260 na milion 600 zimemfanya Koroso kupangiwa kazi nyingine.Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel ameagiza kuondolewa madarakani kwa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa wizara hiyo, Paul Koroso kutokana na mgogoro ulioibuka katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh2.9 bilioni.
Dk Mollel pia ameagiza Koroso aswekwe mahabusu akidai amemtolea majibu na lugha ya kijeuri kuwa “hajali lolote hata akifukuzwa kazi”.
Dk Mollel ametoa maagizo hayo Julai 5 akiwa mjini Nansio Ukerewe alipofika kutatua mgogoro uliobuka kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi hospitali ya Rufaa ya mkoa katika kisiwa hicho ndani ya Ziwa Victoria.
"Kutokana na changamoto zilizojitokeza kwenye mradi huu, Koroso utakoma kuwa mkuu wa Idara ya Ujenzi Wizara ya Afya. Katibu mkuu atamteua mkuu mpya wa idara ambaye atakuja kusimamia mradi wa Ukerewe," alitangaza Dk Mollel.
Pamoja na viongozi na wataalamu wa Wizara, mkoa na wilaya, kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi wa CCM, halmashauri na mkandarasi Suma JKT.
Miongozi mwa malalamiko yaliyotolewa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe dhidi ya Koroso ni kutowashirikisha viongozi wa wilaya na halmashauri katika utekelezaji wa mradi huo.
"Ofisi ya DC, halmashauri na CCM Wilaya ya Ukerewe hawakushikishwa katika utekelezaji wa mradi huu," Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Denis Mwila alimweleza Dk Mollel.
Muda mfupi kabla ya amri ya kuswekwa mahabusu, Koroso alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa Serikali ingeokoa kati ya Sh180 milioni hadi Sh260 milioni iwapo ungetekeleza mradi huo kwa mtindo wa Force account (kutumia nguvu za wananchi) badala ya ukandarasi.
Kiwango kilichotajwa na Koroso kilitofautiana na kiwango cha Sh600 milioni kilichotajwa na mhandisi wa mkoa wa Mwanza, Chagu Nghoma.
Kutokana na tofauti hiyo, Dk Mollel akamtaka Koroso kutoa ufafanuzi, ndipo akasisitiza kuwa hesabu zake ndizo sahihi kwa mujibu wa kanuni na msingi wa kitaaluma na kwamba yuko tayari kuchukullwa hatua yoyote.
"Mheshimiwa Naibu Waziri, kiwango nilichotaja kimezingatia kanuni, vigezo na hesabu za kitaaluma; nitaendelea kusisitiza hilo hata kama ukinifukuza kazi sitajali," alisema Koroso.
Kutokana na kauli hiyo, Koroso aliyeketi jirani na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Ukerewe akajikuta anawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa mahabusu.
Chanzo: Mwananchi
Mnatuchanganya. Ubishi ulikuwa kuhusu tofauti ya fedha ambazo zingeokolewa kwa kutumia Force Account kati ya Koroso na Engineer wa Mkoa; au ulikuwa ni kuhusu bei ya toilet paper holder?Kuna watu humu Wana matatizo ya akili. Mm napingana na serikali kwenye vitu vingi, lakini unawezaje kupinga Jambo Kama hili? Toilet paper holder kwa laki 5?? Alafu huyo mhandisi bado anajibu jeuri
Unataka kusema Ana mtindio wa ubongo (usonji)Huyu jamaa sura yake ilivyokaa kaa tu anaonekana na disorder flan sijui unaibu waziri kaupataje