Naibu Waziri wa Afya amuondolea madaraka Mkuu wa Idara Paul Koroso, aliyemjibu “Sijali lolote hata nikifukuzwa kazi”

Naibu Waziri wa Afya amuondolea madaraka Mkuu wa Idara Paul Koroso, aliyemjibu “Sijali lolote hata nikifukuzwa kazi”

Kwenye miradi ya serikali usipokula na wanasiasa tegemea hujuma na majungu. Ila wazalendo na wataalamu wenye misimamo huwa hawafiki mbali.
Uzalendo kwa kununua toilet paper holder kwa laki 5?? Tuache utani
 
Huyu jamaa sura yake ilivyokaa kaa tu anaonekana na disorder flan sijui unaibu waziri kaupataje
Hili jamaa nalifahamu tangu A level Minaki halikuwa na ushirikiano na watu na lilikuwa lichafu balaa na limeaoma likiwa lizee tu
 
Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel ameagiza kuondolewa madarakani kwa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa wizara hiyo, Paul Koroso kutokana na mgogoro ulioibuka katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh2.9 bilioni.

Dk Mollel pia ameagiza Koroso aswekwe mahabusu akidai amemtolea majibu na lugha ya kijeuri kuwa “hajali lolote hata akifukuzwa kazi”.

Dk Mollel ametoa maagizo hayo Julai 5 akiwa mjini Nansio Ukerewe alipofika kutatua mgogoro uliobuka kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi hospitali ya Rufaa ya mkoa katika kisiwa hicho ndani ya Ziwa Victoria.

"Kutokana na changamoto zilizojitokeza kwenye mradi huu, Koroso utakoma kuwa mkuu wa Idara ya Ujenzi Wizara ya Afya. Katibu mkuu atamteua mkuu mpya wa idara ambaye atakuja kusimamia mradi wa Ukerewe," alitangaza Dk Mollel.

Pamoja na viongozi na wataalamu wa Wizara, mkoa na wilaya, kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi wa CCM, halmashauri na mkandarasi Suma JKT.

Miongozi mwa malalamiko yaliyotolewa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe dhidi ya Koroso ni kutowashirikisha viongozi wa wilaya na halmashauri katika utekelezaji wa mradi huo.

"Ofisi ya DC, halmashauri na CCM Wilaya ya Ukerewe hawakushikishwa katika utekelezaji wa mradi huu," Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Denis Mwila alimweleza Dk Mollel.

Muda mfupi kabla ya amri ya kuswekwa mahabusu, Koroso alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa Serikali ingeokoa kati ya Sh180 milioni hadi Sh260 milioni iwapo ungetekeleza mradi huo kwa mtindo wa Force account (kutumia nguvu za wananchi) badala ya ukandarasi.

Kiwango kilichotajwa na Koroso kilitofautiana na kiwango cha Sh600 milioni kilichotajwa na mhandisi wa mkoa wa Mwanza, Chagu Nghoma.

Kutokana na tofauti hiyo, Dk Mollel akamtaka Koroso kutoa ufafanuzi, ndipo akasisitiza kuwa hesabu zake ndizo sahihi kwa mujibu wa kanuni na msingi wa kitaaluma na kwamba yuko tayari kuchukullwa hatua yoyote.

"Mheshimiwa Naibu Waziri, kiwango nilichotaja kimezingatia kanuni, vigezo na hesabu za kitaaluma; nitaendelea kusisitiza hilo hata kama ukinifukuza kazi sitajali," alisema Koroso.

Kutokana na kauli hiyo, Koroso aliyeketi jirani na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Ukerewe akajikuta anawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa mahabusu.

Chanzo: Mwananchi

Upumbavu mtupu
Kwa sheria ipi ana nguvu hiyo?
 
Ifike wakati sasa wanataaluma wajitambue kama alivyo Eng Paul Korosso

Wanasiasa wakishalambaga asali wanakuwaga wajinga sana, tusiwavumilie tuwape za uso

Dr Mollel hata kung'oa mtu jino hawezi japo ndio fani yake
Kong'oa mtu jino unadhani ni kazi nyepesi.
 
Kuna ubabe gani kwenye majibu? Huyu naibu waziri kilaza anaamrisha mtu awekwe ndani kwa kosa gani? Jaribu kutumia akili hata kidogo.

Kwani Korosso angesema tu kwa taaluma yangu au hesabu nilizo nazi ninhivi na hivi bila kuongeza "hata ukinifukuza kazi" angepungukiwa na nini?

Wakati mwingine ni hekima tu ndio tunakosa.

Waziri amekosea ila pia Korosso amekosea. Kutakiwa kujieleza haimaanishi ndio umeshahukumiwa. Ange handle tu professional
 
Hana hata mamlaka ya kumfuta cheo. Kama ana hayo mamlaka basi anaweza kumpandisha cheo mtumishi yeyote wa umma. Mwenye mamlaka hayo ni Katibu Mkuu wake ambae ndie Mtendaji Mkuu wa Wizara. Na uamuzi wake unaweza kukatiwa rufaa katika Tume ya Utumishi. Watu hua hawakati rufaa kwa sababu mabadiliko hayo ya wadhfa yalikuwa hayaathiri mishahara yao. Lakini sasa kwa hii sheria ya Mwigulu, watu watakata tu rufaa.

Mawaziri sio watendaji katika wizara. Wao jukumu lao ni kusimamia sera za wizara.

Amandla...
Kama unajua mawaziri wanasimamia Sera, mamlaka za Makatibu wakuu kutekeleza Sera zinatokea wapi? Ukisoma hiyo taarifa ya Mwananchi imesema Wazir ameagiza Katibu Mkuu atekeleze jambo kwa maslahi aliyoyataja hapo, maana yake kuna mgogoro ambao umepelekea kusuasua kwa kazi.
Miongoni mwa vitu watendaji wanatakiwa kufanya ni kuepuka migogoro kwa kuwashirikisha wananchi hasa kwenye matumizi ya fedha na sio kwenye utaalamu.
Issue ya Korosso sio utaalamu ila ni matumizi ya fedha tu. Yeye na engineer wa mkoa wanatofautiana pakubwa mno wakat wote ni wataalamu. Kinidhamu alitakiwa kuomba kukaa na mwenzake waweke sawa ila sio kujipiga kifua kuwa yeye ndio yuko sahihi na sio mwingine yule.
 
kabla ya kusona habari yote nilijua huyu jamaa kamjibu waziri vibaya lakini baada ya kusoma wala sioni kosa lake,kwa sababu yeye amesema yupo tayari kufukuzwa kazi kwa sababu ana uhakika na usahihi wa maelezo aliyotoa,Shida ni kwamba hii serikali ya CCM haipendi watu wanaojiamini,wanataka watu wa ndio mzee
Unless kuna taarifa hazijaandikwa lakini ukisoma hiyo habari nashindwa kuelewa kilichomfanya Koroso kuingiza hayo maneno "sijali hata ukinifukuza kazi" katika maelezo yake. Kama issue ilikuwa kujadili tofauti ya figure ambayo ingeokolewa kati yake na Engineer wa Mkoa yeye angestick kwenye maelezo yake ya kitaaluma tu. Sijaelewa ya kufukuzana kazi yaliingiaje pale.
 
"Kutokana na kauli hiyo, Koroso aliyeketi jirani na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Ukerewe akajikuta anawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa mahabusu. "

🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓
Jamaa alijifanya mbabe bila kutambua kuwa ameketi sehemu na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya matokeo anawekwa chini ya ulinzi!
Hili jambo siyo la kushabikia

Governance nzuri haishabikii haya

Serikali yetu ina namna nzuri sana ya kudeal na hizi issues

Actually hiyo situation could have been avoided kirahisi sana
 
Huyu jamaa sura yake ilivyokaa kaa tu anaonekana na disorder flan sijui unaibu waziri kaupataje
UCHAWI upo.

Mollel naibu Waziri Afya.

Halafu Ndugulile anatumbuliwa kila akiwekwa.
 
Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel ameagiza kuondolewa madarakani kwa Mkuu wa Idara ya Ujenzi wa wizara hiyo, Paul Koroso kutokana na mgogoro ulioibuka katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe unaotekelezwa kwa gharama ya zaidi ya Sh2.9 bilioni.

Dk Mollel pia ameagiza Koroso aswekwe mahabusu akidai amemtolea majibu na lugha ya kijeuri kuwa “hajali lolote hata akifukuzwa kazi”.

Dk Mollel ametoa maagizo hayo Julai 5 akiwa mjini Nansio Ukerewe alipofika kutatua mgogoro uliobuka kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi hospitali ya Rufaa ya mkoa katika kisiwa hicho ndani ya Ziwa Victoria.

"Kutokana na changamoto zilizojitokeza kwenye mradi huu, Koroso utakoma kuwa mkuu wa Idara ya Ujenzi Wizara ya Afya. Katibu mkuu atamteua mkuu mpya wa idara ambaye atakuja kusimamia mradi wa Ukerewe," alitangaza Dk Mollel.

Pamoja na viongozi na wataalamu wa Wizara, mkoa na wilaya, kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi wa CCM, halmashauri na mkandarasi Suma JKT.

Miongozi mwa malalamiko yaliyotolewa na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe dhidi ya Koroso ni kutowashirikisha viongozi wa wilaya na halmashauri katika utekelezaji wa mradi huo.

"Ofisi ya DC, halmashauri na CCM Wilaya ya Ukerewe hawakushikishwa katika utekelezaji wa mradi huu," Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Kanali Denis Mwila alimweleza Dk Mollel.

Muda mfupi kabla ya amri ya kuswekwa mahabusu, Koroso alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa Serikali ingeokoa kati ya Sh180 milioni hadi Sh260 milioni iwapo ungetekeleza mradi huo kwa mtindo wa Force account (kutumia nguvu za wananchi) badala ya ukandarasi.

Kiwango kilichotajwa na Koroso kilitofautiana na kiwango cha Sh600 milioni kilichotajwa na mhandisi wa mkoa wa Mwanza, Chagu Nghoma.

Kutokana na tofauti hiyo, Dk Mollel akamtaka Koroso kutoa ufafanuzi, ndipo akasisitiza kuwa hesabu zake ndizo sahihi kwa mujibu wa kanuni na msingi wa kitaaluma na kwamba yuko tayari kuchukullwa hatua yoyote.

"Mheshimiwa Naibu Waziri, kiwango nilichotaja kimezingatia kanuni, vigezo na hesabu za kitaaluma; nitaendelea kusisitiza hilo hata kama ukinifukuza kazi sitajali," alisema Koroso.

Kutokana na kauli hiyo, Koroso aliyeketi jirani na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi Wilaya ya Ukerewe akajikuta anawekwa chini ya ulinzi na kupelekwa mahabusu.

Chanzo: Mwananchi
Milion 260 na milion 600 zimemfanya Koroso kupangiwa kazi nyingine.
 
Kuna watu humu Wana matatizo ya akili. Mm napingana na serikali kwenye vitu vingi, lakini unawezaje kupinga Jambo Kama hili? Toilet paper holder kwa laki 5?? Alafu huyo mhandisi bado anajibu jeuri
Mnatuchanganya. Ubishi ulikuwa kuhusu tofauti ya fedha ambazo zingeokolewa kwa kutumia Force Account kati ya Koroso na Engineer wa Mkoa; au ulikuwa ni kuhusu bei ya toilet paper holder?
 
Engineer kaonewaa, yeye sio mtu wa Evaluation yeye anasimamia kazi tuu suala la rate sio lake,
Inashangaza kuanza kumlaumu Mhandisi tena wakati mkandarasi kashaanza kazi
 
Back
Top Bottom