Chukulia mfano wa cement, cement mfuko Bei yake unajulikana mfano 42.5 ni 20000, alafu umenunuliwa kwa 30000. Hapo inahitaji uwe mtaalamu kujua kuwa Kuna wizi?
Aweso alienda kukagua bwawa lililojengwa kwa mil 200, hivi ilihitaji awe na uwezo wa kusoma BOQ kujua kuwa Kuna wizi umefanyika pale?
Tatizo kubwa tulilonalo waafrica wengi ni hili la kuona suala la kupiga ni kawaida. Ndio maana Hadi leo tupo hivi.
Ni cement ya wapi? Imenunuliwa wapi? Hivi unategemea mkandarasi anunue simenti bila kuweka faida yake, gharama ya kusafirisha n.k.? Na kwenye BoQ hamna kitu kama bei ya mfuko kwenye rates. Kinacholipiwa ni zege au tofali lililotumika kwenye mradi.
Gharama ya mradi inategemea quotation ya mkandarasi. Mkandarasi anaweka kiasi anachotaka alipwe kutokana na kazi hiyo na ni uamuzi wa mshitiri kumkubalia au kumkatalia. Gharama za utekelezaji za mkandarasi zinajengwa na vitu vingi, overheads zake, gharama ya kuleta vitendea kazi, hali ya eneo, ulinzi wa eneo, ujenzi wa stoo na ofisi yake na ya msimamizi, upatikanaji wa wafanyakazi ( kuna maeneo hupati kibarua baada ya mavuno na hivyo mkandarasi anatakiwa awalete kutoka sehemu nyingine), mahitaji ya mkataba ( advance payment bond, performance bond, bima, kupima vifaa, usafirishaji wa vifaa, uharibikaji wa vifaa wakati wa usafirishaji n.k.), ushindani ( ni makandarasi wangapi wa daraja linalotakiwa ambao wako tayari kuifanya kazi hiyo), gharama ya kuleta wasimamizi wa wake ( site agents, foremen n.k) n.k. Aidha, uhakika wa malipo ( serikali ina sifa ya kutolipa kwa wakati kwa hiyo mkandarasi makini ataweka pia gharama za overdraft zitakazomwezesha kukopa pesa ili atekeleze mradi). Sasa waziri atazijuaje zote hizi mpaka aseme kuna wizi umetokea? Na wizi uko wapi kama wewe ulikubali kumlipa kwa hiari yako? Hivi ukienda Shoppers Plaza ukanunua embe kwa shilingi 10000 halafu kesho yake ukakuta maembe yanauzwa shilingi 1000 Tandale, utawaita Shoppers wezi?
Hayo mambo ya bei ya mfuko wa simenti yanatokea kwenye Force Account au mikataba ambapo mshitiri anachukua jukumu la kutoa vifaa vyote vya ujenzi. Huko ndiko unaweza kulinganisha bei ya simenti ya kwa Mangi na ile iliyonunuliwa na Mwalimu Mkuu ambae mara nyingi hana experience ya ujenzi.
Hii tabia ya kujiona unajua kila kitu na kuendekeza unafik inatutia hasara kupita kiasi. Na kama mshitiri haridhiki na utendaji kazi katika mradi, mkataba umeweka wazi hatua anazopaswa kuchukua. Kumtupa jela sio mojawapo.
Amandla...