Nailaumu CHADEMA kuwa hawajui wanataka nini

Rafiki sasa tunyenyekee kwenye haki yetu?!
Kwa nini tumgeuze kama Tz ni mali ya mtu mmoja
Wanaonyenyekea ni kwa faida yao binafsi sio wananchi
I see nimeumia mno kusoma statement yako 'Eti tumsifie Magufuli' are you serious??!
Basi safari bado ni ndefu
Mbowe did not bow alituma ujumbe
Bro think twice I see
 
Hizo ni hisia tu muundo wa Chadema umekaa kitasisi zaidi huwezi linganisha na hivyo vyama vingine ulivyovitaja viongozi pamoja na kamti kuu ni wasomi na wanavision wanajua walipotoka hali iliopo sasa na nani anayetufaa kutuongoza ukiona kelele za wasimu zinakuwa nyingi basi ujue tupo kwenye right truck
 
Nashangaa ww mkabila wa Kisukuma muunga mkono ukanda na ukabila wa ajabu ajabu! Na ww miaka hii minne umeonekana ni adui wa CHADEMA, hivi kweli adui unaweza kutuchagulia silaha ya kukupiga nayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mayalla nilikua nakufuatilia na kusoma sana mabandiko yako....lakini tangu ulipobadirika nikakuweka kando...sijawahi kuona umeandika kuhusu kuzuiwa mikutano ya siasa...leo unasema CHADEMA inahitaji mtu mpya na sio Mbowe...umejisahaurisha kua vyama lazima vijinadi kupitia mikutano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Ceftriaxon karibu mitaa hii

P
 
Pascal Mayalla ni kweli chadema inahitaji fresh blood ila sio Mwambe,CHADEMA inahitaji fresh blood kama Tundu Lisu ila walichokifanya sio kibaya ni maandalizi ya Tundu lisu kuongoza jahazi
Mkuu JME, naheshimu mawazo yako, kwa vile Chadema toka kuasisiwa kimekuwa ni chama cha uanaharakati, Lissu ni mwanaharakati tena extremist wa siasa za confrontation type, Chadema kunahitaji kufanya transformations kutoka chama cha kiharakati kugeuka chama tawala in waiting, hivyo sasa kinahitaji moderate politicians wenye vichwa vilivyo tulia ambao sio wapayukaji bali wapanga mikakati.

Mwambe nimekaa nae chini pale Bungeni Dodoma,;jamaa yuko vizuri upstairs atabadili Chadema kutika siasa za pinga pinga na kuonyesha siasa mbadala. Serikali kivuli itaingia kazini throughou a year sio sasa serikali kivuli ni kipindi cha Bunge tuu.

P
.
 
Pascal Mayalla,
Inawezekana CHADEMA wakawa hawajitambui lakini jee wale waliozuia mikutano ya vyama mbadala wanajitambua?
Mkuu Mwanamageuko, kwanza asante kwa hoja hii ya mikutano na huku ndiko kutojitambua kwenyewe ninakokuzungmzia.

Katiba imeruhusu mikutano, rais ameapa kuilinda katiba, anezuia mikutano kinyume cha katiba
Katiba hiyo hiyo imeweka utaratibu wa nini cha kufanywa pale katiba inapovunjwa au kukiukwa,

Ni kutokana na Chadema kutokujitambua badala ya kufuata sheria, taratibu na kanuni kulishughulikia hili,,Chadema wao wakataka kuandamana maandamano ya UKUTA. Uvunjwaji wa katiba haupingwi kwa press conference, kelele, mikutano au maandamano.

Kwenye hili nilishauri

P
 
Pascal wewe cdm hukufukuzwa bali uliamua kumfuata pot wako sasa yanini kuendelea kufuatilia mambo ya CHADEMA? Pascal Mayalla,
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Mmawia, kiukweli wengi humu tunajuana kupitia jf tuu lakini hatujuani in reality, mimi ni very real, sijawahi kuwa CCM, hata wakati nikimpigia debe EL, sikuwahi kuwa CCM wala sijawahi kuwa Team Lowassa, na hata Lowassa alipohamia Chadema, sikuwahi kuwa Chadema, na sasa ni kweli poti wangu ndio yuko kunako, bado sijawahi kuwa CCM, ila tunanokwenda...
P
 
Huyu Bwana Pascal Mayalla ni Janga kweli, bado anaamini kuwa Rais atamfikiria kama wakina Mtatiro, lakini ndiyo hivyo ni kama Fisi anangojea Mkono wa Binadamu Udondoke.
Jamii ya Kujipendekeza na Kusifu tu! Hovyo kabisa.
Mayala wewe ndie hujitambui na ndio maana unavyotafuta kwa 'mkuu wa kaya' hujakumbukwa kwani hueleweki, wenzio wote wa 'kanda pendwa' wameshakumbukwa umebaki wewe unajitekenya kila uchwao.
Wakuu Nikwega na Pilipili Kichaa, ama kweli nyie vichaa kweli, hivyo kwa mtu mwenye uwezo wa kusoma tuu, kwa kusoma mabandiko yangu humu jf, unaamini mimi ni mtu ninayetafuta uteuzi?.
P
 
Toka lini akaipenda chadema? Acha aweweseke tu,mambo ya chadema yanaamuliwa na wanachadema wenyewe.
Ni kweli, mambo ya vyama yanapaswa kuamuliwa na vyama vyenyewe, ndio maana nimependekeza hivi
Ruzuku ikiishafutwa mkakiendesha chama kwa fedha zenu na sio kwa kodi zetu, then mtakuwa huru kujifanyia mnavyotaka, hata mkiamua kuteua mfalme, sultani au Mangi, tena umenikumbusha enzi za Mangi, Mangi akimtamani tuu mkeo, siku hiyo unampelekea na kumsubiria apate baraka za Mangi, hivyo kwa mapenzi yenu na viongozi wenu rukhsa hata kuwapenda kama Mangi na kuwapelekea...
P
 
Ili CHADEMA iendelee kuwepo wamuchague Mwambe!!? Uache masihara.
Pamoja na mapungufu ya Mbowe, bado ni mtu sahihi wa kuingoza Chadema kwa sasa.
Vinginevyo wewe Paskali utakuwa ni malaika kuzimu. Tunakukataa, ushindwe na ulegee!
Amen, endelezeni tuu mambo yenu chaguaneni kwa mazoea, baada ya uchaguzi wa 2020, tutakuja kukumbushana!.
P
 
Ndugu Pascal, hapo hukuuliza swali,
Brother it is very hard to believe huna chama.
Ndugu i still love reading your articles
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Mkirindi, amini usiamini sina chama ila sasa najiandaa kustaafu uandishi na kuwa mtumishi wa watu, kwa mujibu wa katiba yetu ili kuwa mtumishi wa watu ni lazima ujiunge na chama cha siasa kwa lazima, utake usitake!.
Hili nimelilalamikia sana
Thanks for reading me.
P
 
Mkuu Fuso, usiishie kunisoma tuu humu jf, karibu unisikilize kabisa in person sikiliza hoja zangu!.
P
 
Mkuu Chakaza, ulijuaje?. Mimi naandikia makala magazeti kadhaa na gazeti la habari leo ni moja ya magazeti ninayoyaandikia na hizi ni baadhi ya makala zangu
P
 
Mkuu Masiya, kila nikishauri, sio tuu huwa natoa sababu, bali pia huwawekea mifano na kuwaambia the consequenses za uamuzi wao.
Kama ushauri kwenye bandiko hili its the choice between life and death, live and let die!.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…