Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Kwa walio lima mwishoni alizeti ikiwa bado ndogo inaathirika mkuu
Lakini kama wakati mvua inakata alizeti ilikua imekua itaenda fresh tu athari kidogo sana

Ila mvua ikirudi mapema ikamwaga maji ya kutosha itapona
We ulipanda tar ngap mkuu,
 
Mvua naona kama zinasuasua mkuu,jua ni kali..vip haliwezi kuathiri Alizet kwa sasa?
Alizeti kama mtu ukipanda mapema na shamba likiwa limelimwa vizuri kwa trekta. Alizeti inawezekana kuvumilia jua. Hasa ikisha fika kina cha magoti au kiunoni. Halafu ile hali ya trekta kupita huwa kunafanya udongo utunze maji.

Alizeti ikipigwa jua ikiwa changa ndio inakufa au kwa shamba ambalo halijalimwa kwa trekta.

Kilimo kinahitaji usimamizi wako kwa 100%. Maana watu wengi wanapigwa hela zao na wasimamizi na watu wanaowaamini .
 
MREJESHO WA GHARAMA so far

Kukodi Shamba ekari 20
20 x 30,00 = 600,00
Shamba lilikua safii

Kulima
20 x 40,000 = 800,000

Mbegu (ASA)
80 x 5,000 = 400,000

Kupanda
20 x 30,000 = 600,000

Palizi
20 x 50,000 = 1,000,000

Mengineyo
1,000,000

Jumla kuu kama 4,500,000

Mpaka sasa nimelaza 4.5M
Bado kuvuna, kupeta, na hifadhi
Makadirio gharama yote isizidi 6M

Mawazo makuu yanayo vuruga kichwa changu kwa sasa ni JE NITAPATA WASTANI WA GUNIA NGAPI KWA EKARI?
Ndugu yangu Ukwaju sijui ni mrejesho gani unao utaka zaidi ya huu nilioutoa (nimeu quote hapo juu)

Alizeti inapalizi moja tu.......kama ulilipia palizi zaidi ya moja basi jua ULIPIGWA mkuu

Hizo ndio gharama nilizo tumia so far...... nimeweka hadi gharama za mademu niliomega huko 😂😂😂😂
 
Ndugu yangu Ukwaju sijui ni mrejesho gani unao utaka zaidi ya huu nilioutoa (nimeu quote hapo juu)

Alizeti inapalizi moja tu.......kama ulilipia palizi zaidi ya moja basi jua ULIPIGWA mkuu

Hizo ndio gharama nilizo tumia so far...... nimeweka hadi gharama za mademu niliomega huko [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kukodi shamba ekari ni elfu tatu? Au.umekosea?
 
Ndugu yangu Ukwaju sijui ni mrejesho gani unao utaka zaidi ya huu nilioutoa (nimeu quote hapo juu)

Alizeti inapalizi moja tu.......kama ulilipia palizi zaidi ya moja basi jua ULIPIGWA mkuu

Hizo ndio gharama nilizo tumia so far...... nimeweka hadi gharama za mademu niliomega huko [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwa wanaolima alizeti mwezi Disemba, lazima wapalilie mara 2
 
MREJESHO WA GHARAMA so far

Kukodi Shamba ekari 20
20 x 30,00 = 600,00
Shamba lilikua safii

Kulima
20 x 40,000 = 800,000

Mbegu (ASA)
80 x 5,000 = 400,000

Kupanda
20 x 30,000 = 600,000

Palizi
20 x 50,000 = 1,000,000

Mengineyo
1,000,000

Jumla kuu kama 4,500,000

Mpaka sasa nimelaza 4.5M
Bado kuvuna, kupeta, na hifadhi
Makadirio gharama yote isizidi 6M

Mawazo makuu yanayo vuruga kichwa changu kwa sasa ni JE NITAPATA WASTANI WA GUNIA NGAPI KWA EKARI?
A cha ubishi sniper92
 
Mwaka Jana nililima Hysan Eka 10 nikapata gunia 35 ambazo zilitoa mafuta dumu 47.
Mwaka huu nimelima ASA eka 15 ,Ila ASA inavutia zaidi ukiangalia jinsi inavyoota na inavyokua Ila mwaka huu mvua imekuwa uchawi mkuu
Kwa kiwango cha magunia kea Hysan utakuwa ulifeli sana sema kwenye mafuta kidogo ilikuinua.

Alizeti huwa haitaki mvua; mimi nimepanda mpaka tarehe 4 mwezi huu na nina imani nitavuna.

ASA usisahau kutuletea matokeo ya ASA tafadhali
 
umeishia mbali saha UPDATE zako hujaweka kupalilia ni mara ngapi umefanya.
Wenyeji wanaokodisha mashamba ni wabaya sana, wanakuuzia , wana kusafishia shamba, watalima na kupanda wenyewe, kwa tamaa zao watafanya wenyewe bila vibarua hivyo unatakiwa uwepo.
Ukichelwa kwenda wataomba hela ya palizi ya kwanza hadi ya 2 ukizubaa ya 3 na hawafanyi ukifika wakati watasema mvua nyingi weka palizi ya 3
nimeshtuka shamba lilishachoka kwa kulimwa miaka mingi Alizeti nikamwambia jamaa hawa wnasema utapata gunia 18 mpaka 20 kwa eka ni uongo mwisho ni gunia 7 au 8
Leo wanasema jua kali na ndege
huenda wamemkata nasubiri eka zilizo baki nitaweka mrejesho na hizo UPDATES zako tutapata jumisho km Alizeti ni zao la kumtoa mtu
Mlipigwa sana tena sana; alizeti palizi ni moja tu.

Alizeti huwa inakuwa taratibu ndani ya wiki 3 baada ya wiki tatu ndipo mabadiliko na Kazi ya ukuaji inaongezeka na hki ndicho kipindi kizuri cha palizi. Baada ya hapo unasubiri kuvuna tu
 
Mm mwenyewe nimejitosa heka 5,nipo nasikikizia mlio tu
 
MREJESHO WA GHARAMA so far

Kukodi Shamba ekari 20
20 x 30,00 = 600,00
Shamba lilikua safii

Kulima
20 x 40,000 = 800,000

Mbegu (ASA)
80 x 5,000 = 400,000

Kupanda
20 x 30,000 = 600,000

Palizi
20 x 50,000 = 1,000,000

Mengineyo
1,000,000

Jumla kuu kama 4,500,000

Mpaka sasa nimelaza 4.5M
Bado kuvuna, kupeta, na hifadhi
Makadirio gharama yote isizidi 6M

Mawazo makuu yanayo vuruga kichwa changu kwa sasa ni JE NITAPATA WASTANI WA GUNIA NGAPI KWA EKARI?
Weka current picha ya shamba nikusaidie kukupa tathmini
 
Alizeti haihitaji kulimia shida. Ukilima alizeti Ili unufaike lazima uwe mvumilivu wa kusubiria bei tofauti na hapo lazima uongeze thamani mazao yako
Na mwaka huu ilivyotucharaza isipofika gunia laki mbili sijui!
 
Kwa wanaolima alizeti mwezi Disemba, lazima wapalilie mara 2
Wapi huko wanapalilia alizeti mara 2?

Alizeti palizi ni mara moja tu
Ukipalilia mara 2 kwa alizeti ya biashara hasara kwako inakua ni kama uji na mgonjwa

Alizeti inakua haraka sana baada tu ya kuipalilia, shamba likilimwa vizuri palizi iwe wiki ya pili au ya tatu toka imepandwa na ikikua majani yake yana kivuli sana kiasi kwamba nyasi zinakosa nguvu ya kukua chini yake
 
Tunaomba mirejesho tafadhali kwa mlio lima. Mimi napanga mwaka huu nikalime Songea, Insha Allah.

Kwa yeyote aliyewahi kulima hili zao Songea naomba anipe Uzoefu (Muda wa kupanda, mbegu bora, upatikanaji wa mashine za kukamua etc)
 
Ngoja tumuombe huyu akusaidie hints kidogo Ngome Kuu
 
Back
Top Bottom