Wabongo bhana. Umejaribu hata kufatilia kwa nini TFF wamesogeza mbele usiku wa tuzo? Wala hakuna cha ajabu kwenye hilo ni swala la TFF tu kujitafuta ili kuziboresha. Mbona hamshangai CAF mashindano yanaisha mwezi wa sita au saba ila tuzo zinatolewa December au January? TFF wanahoja zifuatazao
1. Tuzo za TFF sio kwa ajili ya ligi kuu bara pekee yake, TFF inasimamia mashindano mengine mengi lakini ikiwemo timu ya taifa. Kwa sasa TFF imetafuta muda mzuri ambapo wataziunganisha tuzo na mashindano mengine kama vile ligi ya wanawake, under20 nk. Lakini kwa sasa kalenda ya CAF na FIFA wachezaji wa timu za taifa wapo kwenye timu zao na hata hao utopolo na azam soon wakicheza finali Zenji wanaondoka kwenda kwa timu zao za taifa. Kwahiyo timing mnayoitaka nyie haitaweza kufanya kazi. Kuweni na subira.
2. Utoaji wa tuzo ndio target angle ya TFF kujitafutia udhamini bora na mnono na ikiwemo kujitangaza ili wapate udhamini so inabidi waje na kitu bora bila kulipualipua. Hapa naamnisha ili sherehe zifane inabidi wachezaji muhimu wote wawemo kwenye kupokea tuzo zao. Hii inamaanisha TFF na wachezaji pamoja na timu zipate muda wa kutosha kujiandaa kushiriki kwenye tuzo hizo hata kama watakuwa katika timu nyingine. Kumbukeni msimu uliopita Mayele ambaye alikuwa ni muhimu kwenye zile tuzo hakuwepo sababu tu alikuwa kwenye majukumu ya timu yake ya taifa.
3. Hao CAF na FIFA wanapitisha hata miezi mitatu mpaka kuja kutoa tuzo unajua kwanini? Wanataka wapate muda wa kujiandaa vizuri ili waje na kitu bora, na huwa tunaenjoy kweli kweli kufatilia hayo ma ballondor au mchezaji bora wa Africa, sasa wazee wa zima moto hatutaki kujifunza kwao, tunaendeshwa na mihemko.
4. Huyo Karia mnayemuona hawapendi utopolo ndio amewasamehee hao utopolo makosa yao mengi ya kuvunja kanuni ili tu kuisaidia utopolo ijipate maana ingekuwa aibu Simba kuchukua kombe mara nane mfululizo. Juzi tuu amepotezea uwapokonya point12 kwa kumchezesha pacome ambaya hakustahili.
5. Uto wenye akili muongezeke ongezeke basi mfike walau hata watano. Huyo injinia ni swala muda tuu ataanza kuwashika nyeti.