Naitabiria Yanga mafanikio zaidi ya Simba msimu wa 2023-2024

Kuna dalili mbaya toka pre-season hadi jana kwenye Simba Day nimeshaaza kuziona zinazoashiria kuwa Simba inaenda kuwa na msimu mbaya sana.

1. Tukirudi nyuma mwishoni mwa msimu uliopita, kipa Aishi Manula aliumia na kwa sababu za kijinga kabisa Beno Kakolanya, kipa mwenye uwezo akawa anakaa benchi tena katika mechi kubwa na muhimu sana. Hili tumelizungumza sana na nadhani kuna uzi nilishawahi kuuleta. Cha ajabu zaidi, inaonyesha hakuna juhudi zilizokuwa zinafanyika kutafuta kipa mbadala ili kipindi cha usajili kikifika asajiliwe, matokeo yake tumekuja kuokota kipa wa KMC dakika za lala salama.

2. Pre-season baadhi ya wachezaji kucheleweshwa kupelekwa kambini bila sababu za msingi. Baadhi ya wachezaji wapya walikuwa wanazungushwa kwenye matukio hapo Dar wakati wenzao wako kambini na wengine kina Chama na Baleke walichelewa kupelekwa kambini bila sababu za kueleweka. Hapo hapo inasemekana kocha alienda kwenye kozi fupi kwao Brazil (na kama wiki moja kabla alikuwa huko huko Brazil). Kimsingi timu imefanya mazoezi ya pre-season ya pamoja ya labda wiki moja tu.

3. Kwanini timu imejaza mawinga na kuzembea kusajili kiungo mkabaji na beki wa kushoto mbadala wa Zimbwe? Msimu uliopita niliona Simba imefululiza kusajili wachezaji wafupi kwa mkupuo. Nilibaki najiuliza huyu anayefanya usajili ana nia gani, hili halioni au ni makusudi haya? Msimu huu tumebadili gia, tumejaza mawinga, unajiuliza nia ni nini? Ukiangalia mechi ya jana dhidi ya Power Dynamos, utaona shida ya toka msimu uliopita pale eneo la kati ipo pale pale na hili litaisumbua sana Simba. Kuna wakati nilishauri Israel Mwenda ajaribiwe beki wa kushoto na kweli Simba ikatembea na ushauri huo lakini ukiangalia zile mechi alizochezeshwa nafasi hiyo kama ile na Coastal Union bado hakuwa comfortable kucheza upande ule. Ni sawa kumtumia hivyo kwenye dharura ila kwenye dirisha la usajili kulikuwa na nafasi ya kusajili mtu ambaye anaweza kucheza hiyo nafasi kwa ufanisi.

4. Kuendelea kumkumbatia Bocco. Kama mpira ni burudani, mimi siburudiki nikimuona Bocco akiwa uwanjani anachezea Simba hasa ukizingatia wachezaji wenye viwango, uwezo na ambao uchezaji wao unavutia na wanakupa matokeo kama Moses Phiri wapo wanasugua benchi. Mimi naamini Robertinho bado ni kocha mzuri sana na siyo yeye anayemkumbatia Bocco, naamini anafuata amri anayopewa kutoka juu yanayombeba Bocco na yanayompiga pini Phiri. Simba isitegemee mafanikio yoyote ya ndani au nje kwa kumtumia Bocco katika zama hizi. Ni misimu mingapi Simba imekwama na kugotea Robo huko CAF kisa mapungufu ya hawa kina Bocco, kwa nini wahusika hawajifunzi?

Nadhani kuna watu pale kwenye uongozi ndani ya Simba hawana mapenzi ya dhati na timu. Wameshikilia dhamana ya kuwapa furaha wanasimba ila pia wamejiandaa kuitumia dhamana hiyo kuwaumiza kwa maksudi kabisa wanasimba kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.

Yanga wana timu ya kawaida mno msimu huu ila pamoja na hilo kwa ninachokiona kinaendelea pale Simba, Yanga watakuwa na mafanikio msimu huu kuizidi Simba.

Nawasilisha.
Hapo mwishoni ndio umeharibu kwamba yanga wana timu ya kawaida msimu huu? Au umetumia tafsida kuwasilisha hoja? Timu ya kawaida inapataje mafanikio? Na kama ni ivyo timu nyingine za kawaida zinashindwaje kuyapata ayo mafanikio? Kukiri ubora wa mwenzako sio dhambi wewe kubari tu ya kwamba yanga wanacho kikosi bora kuizidi simba ndo ukweli wala ahiitaji kuzungukazunguka, timu zote tumeziona uwanjani bwana, licha ya ivyo yanga wamesajili kiufundi na sio kimihemko wamewapiga simba gape kubwa sana kiufundi, Angalia ata maandalizi yenu ya pre season ni ya kuungaunga, wenzenu wakati wako Avic town wanapiga maandalizi ya kufa mtu nyie mko angani kwenye safari ya uturuki, na wengine mara dar wengine mara brazil utawezaje kushindana na mtu aliyejiimarisha kwa 100% kila idara?
 
NAUNGA MKONO HOJA.

UAJIULIZA ANAYEFANYA USAJILI WA MAWINGA ANAAKILI TIMAMU KWELI?????????

Mawinga. 2023
1. Peter Banda.
2. Jimyson Mwinuke.
3. KIBU Denis.
4.Said Ntibazonkiza.
5. CLOTUS Chama 10-11.
6. Aubin Kramo.
7. Essomba Onana.
8. Luis Miquesson.

Hili KOSA lilifanyika 2020.
Mawinga walikuwa kumi, ukiunganisha idadi Yao mchango WAO MAGOLi hayafiki hata 10.

1 Bernald Morison.
2. Perfect CHIKWENDE.
3. Hassan Dilunga.
4. Ibrahim Ajibu.10--⁷
5.peter Banda.
6.pape sackho
7. Dunkan Nyoni
8. Valentine Muhilu.
9. KIBU Denis.

UNAJIULIZA HUU USAJILI UNAFANYWA NA MTU MWENYE AKILI TIMAMU KWELI.
Kati ya Mashabiki wa Simba Wenye hoja nzito huwa ni wewe. Sijawahi kuacha kukuunga mkono kwenye hoja zako. Simba ya Sasa ina umbo la mnyama Simba dume kabisa kama jina lake. Mbele mpana nyuma mkondefu.
 
Hapo mwishoni ndio umeharibu kwamba yanga wana timu ya kawaida msimu huu? Au umetumia tafsida kuwasilisha hoja? Timu ya kawaida inapataje mafanikio? Na kama ni ivyo timu nyingine za kawaida zinashindwaje kuyapata ayo mafanikio? Kukiri ubora wa mwenzako sio dhambi wewe kubari tu ya kwamba yanga wanacho kikosi bora kuizidi simba ndo ukweli wala ahiitaji kuzungukazunguka, timu zote tumeziona uwanjani bwana, licha ya ivyo yanga wamesajili kiufundi na sio kimihemko wamewapiga simba gape kubwa sana kiufundi, Angalia ata maandalizi yenu ya pre season ni ya kuungaunga, wenzenu wakati wako Avic town wanapiga maandalizi ya kufa mtu nyie mko angani kwenye safari ya uturuki, na wengine mara dar wengine mara brazil utawezaje kushindana na mtu aliyejiimarisha kwa 100% kila idara?
Mna timu ya kawaida, hata nyie mnajua hilo ila mnaogopa kuonyesha hisia zenu mnadhani upande wa pili utatumia hilo kuwatania.

Pia Yanga nao hawajafanya preseason ya muda wa kutosha saaana kuizidi Simba. Wote ni wale wale tu.
 
Timu ya kawaida halafu inachukua vikombe vyote vya ndani! Inafika hatua ya fainali kombe la shirikisho Afrika!
Halafu unasema Yanga haijafanya pre season ya kutosha kuizidi simba!! Hivi hii kauli ina uhalisia kweli!!
 
Kuna dalili mbaya toka pre-season hadi jana kwenye Simba Day nimeshaaza kuziona zinazoashiria kuwa Simba inaenda kuwa na msimu mbaya sana.

1. Tukirudi nyuma mwishoni mwa msimu uliopita, kipa Aishi Manula aliumia na kwa sababu za kijinga kabisa Beno Kakolanya, kipa mwenye uwezo akawa anakaa benchi tena katika mechi kubwa na muhimu sana. Hili tumelizungumza sana na nadhani kuna uzi nilishawahi kuuleta. Cha ajabu zaidi, inaonyesha hakuna juhudi zilizokuwa zinafanyika kutafuta kipa mbadala ili kipindi cha usajili kikifika asajiliwe, matokeo yake tumekuja kuokota kipa wa KMC dakika za lala salama.

2. Pre-season baadhi ya wachezaji kucheleweshwa kupelekwa kambini bila sababu za msingi. Baadhi ya wachezaji wapya walikuwa wanazungushwa kwenye matukio hapo Dar wakati wenzao wako kambini na wengine kina Chama na Baleke walichelewa kupelekwa kambini bila sababu za kueleweka. Hapo hapo inasemekana kocha alienda kwenye kozi fupi kwao Brazil (na kama wiki moja kabla alikuwa huko huko Brazil). Kimsingi timu imefanya mazoezi ya pre-season ya pamoja ya labda wiki moja tu.

3. Kwanini timu imejaza mawinga na kuzembea kusajili kiungo mkabaji na beki wa kushoto mbadala wa Zimbwe? Msimu uliopita niliona Simba imefululiza kusajili wachezaji wafupi kwa mkupuo. Nilibaki najiuliza huyu anayefanya usajili ana nia gani, hili halioni au ni makusudi haya? Msimu huu tumebadili gia, tumejaza mawinga, unajiuliza nia ni nini? Ukiangalia mechi ya jana dhidi ya Power Dynamos, utaona shida ya toka msimu uliopita pale eneo la kati ipo pale pale na hili litaisumbua sana Simba. Kuna wakati nilishauri Israel Mwenda ajaribiwe beki wa kushoto na kweli Simba ikatembea na ushauri huo lakini ukiangalia zile mechi alizochezeshwa nafasi hiyo kama ile na Coastal Union bado hakuwa comfortable kucheza upande ule. Ni sawa kumtumia hivyo kwenye dharura ila kwenye dirisha la usajili kulikuwa na nafasi ya kusajili mtu ambaye anaweza kucheza hiyo nafasi kwa ufanisi.

4. Kuendelea kumkumbatia Bocco. Kama mpira ni burudani, mimi siburudiki nikimuona Bocco akiwa uwanjani anachezea Simba hasa ukizingatia wachezaji wenye viwango, uwezo na ambao uchezaji wao unavutia na wanakupa matokeo kama Moses Phiri wapo wanasugua benchi. Mimi naamini Robertinho bado ni kocha mzuri sana na siyo yeye anayemkumbatia Bocco, naamini anafuata amri anayopewa kutoka juu yanayombeba Bocco na yanayompiga pini Phiri. Simba isitegemee mafanikio yoyote ya ndani au nje kwa kumtumia Bocco katika zama hizi. Ni misimu mingapi Simba imekwama na kugotea Robo huko CAF kisa mapungufu ya hawa kina Bocco, kwa nini wahusika hawajifunzi?

Nadhani kuna watu pale kwenye uongozi ndani ya Simba hawana mapenzi ya dhati na timu. Wameshikilia dhamana ya kuwapa furaha wanasimba ila pia wamejiandaa kuitumia dhamana hiyo kuwaumiza kwa maksudi kabisa wanasimba kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.

Yanga wana timu ya kawaida mno msimu huu ila pamoja na hilo kwa ninachokiona kinaendelea pale Simba, Yanga watakuwa na mafanikio msimu huu kuizidi Simba.

Nawasilisha.
Wewe Ni Utopolo, na hatutarajii kuiombea Simba mema!

Vitu vingine havihitaji akili kung'amua.

Ujinga
 
Lengo la Yanga kubeba makombe yote ni kuhakikisha wachezaji wa Simba wanasahau kabisa test ya sherehe ya kombe lolote! Hii ni psychological torture mbaya kuliko zote Kwa mchezaji! Hata wachezaji walipwe mishahara mikubwa kiasi Gani bila kombe misimu mitatu mfululizo hawatakuwa na morali inside! Hebu muangalie Kibwana akipangwa anavyojituma mlinganishe morali na Mzee Kapombe!

Upande wa mashabiki wa Simba , Yanga inabeba ndoo zote na kuhakikisha wanakuwa waropokaji na watukanaji grade one Dunia nzima! Bila kombe mshabiki huna cha kujivunia, unakuwa debe tupu haliachi kuvuma! Simba ni Debe Tupu fc linavuma! kolowizard mbumbumbu fc!

Kelele kibao ooh Mlete Phiri, hata wacheze Phiri hamsini uwanjani Simba itabaki kuwa timu mbovu, Haina mipango kama Yanga, Haina pesa kama Yanga, Haina uongozi kama Yanga ila pia Haina makombe kama Yanga, makombe ya Simba ni kuwa top ten CAF, kununua kibegi, kushindwa kiume na kujaza uwanja!
Umekaza fuvu mmmh

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Wewe Ni Utopolo, na hatutarajii kuiombea Simba mema!

Vitu vingine havihitaji akili kung'amua.

Ujinga

MPIRA haupo hivyo

Yeye AMETOA hoja zake na wewe mjini kwa Hoja.

Ukisema yeye UTOPOLO Au Ndunduka ni Majibu ya kitoto, hayafai kuwepo hapa Jamii Forum kwenye Great thinkers.

Hoja HUJIBUWA KWA HOJA.
 
Timu ya kawaida halafu inachukua vikombe vyote vya ndani! Inafika hatua ya fainali kombe la shirikisho Afrika!
Halafu unasema Yanga haijafanya pre season ya kutosha kuizidi simba!! Hivi hii kauli ina uhalisia kweli!!
Mmevuruga kikosi na upepo ulikuwa upande wenu ila kikosi cha sasa ni cha kawaida saana.

Suala la muda wa kutosha wa preseason lilikuwa muhimu zaidi kwa Yanga kuliko Simba maana mna benchi jipya na mna maingizo mengi kwenye kikosi cha kwanza. Kina Diarra na Aucho wamejiunga lini na wenzao? Bado wachezaji wapya waliosajiliwa.
 
Aisee Yanga iko imara sana. Mchezaji wa maana aliyeondoka kwenye kikosi ni Fiston Mayele tu. Bangala na Juma Shaban, hawakuwa hata na msimu mzuri. Kisinda ndiyo kabisaaa!!

Na ukija kwenye benchi la ufundi; ukumbuke kocha Gamondi amefundisha soka katika vilabu vikubwa Barani Afrika! Hivyo hata CV yake ni kubwa kuliko ile ya Profesa Nabi!

Usajili wa Yanga msimu huu umegusa maeneo muhimu tu. Viongozi hawakusajili kwa mihemko kama viongozi wenu.
 
Kuna mchezaji wa Simba aliyeachwa ambaye unadhani angetakiwa kubaki?
 
Benno Kakolanya hakutakiwa kuachwa! Hata Joash Onyango naye alikuwa ni msaada sana kwenye ligi ya ndani.

Kwa sasa mna mabeki wawili tu wa kati wa uhakika. Pembeni kushoto yuko Tshabalala peke yake!! Ukija upande wa Yanga, kila namba ina zaidi ya wachezaji wawili wa uhakika. Halafu tukichukua vikombe vyote mtalalamika kweli!!
 
Kwa hiyo kuachwa kwa wachezaji wawili ndiyo useme usajili wa mhemko, tena mmoja mlikuwa mnamsema sana kuwa ni mzee na hafai, leo hii unamlilia? Umemuona Malone? Halafu umecopy maneno yangu ila mimi niliyasema kwa angle tofauti.
 
Aisee Yanga iko imara sana. Mchezaji wa maana aliyeondoka kwenye kikosi ni Fiston Mayele tu. Bangala na Juma Shaban, hawakuwa hata na msimu mzuri. Kisinda ndiyo kabisaaa!!

Na ukija kwenye benchi la ufundi; ukumbuke kocha Gamondi amefundisha soka katika vilabu vikubwa Barani Afrika! Hivyo hata CV yake ni kubwa kuliko ile ya Profesa Nabi!

Usajili wa Yanga msimu huu umegusa maeneo muhimu tu. Viongozi hawakusajili kwa mihemko kama viongozi wenu.
Yanga tunabeba tena makombe 2024, wataanza kutuelewa ngao ya jamii.
 
MPIRA haupo hivyo

Yeye AMETOA hoja zake na wewe mjini kwa Hoja.

Ukisema yeye UTOPOLO Au Ndunduka ni Majibu ya kitoto, hayafai kuwepo hapa Jamii Forum kwenye Great thinkers.

Hoja HUJIBUWA KWA HOJA.
Ujinga kutoka kwa mjinga nao Ni hoja?

Wewe Ni mgeni humu. Utopolo wanajulikana siku zote.

Tutakaaa humu kujibu hoja za kijinga za kishabiki maandazi.

Na ww mjinga mmetumana wapuuzi nyie kila saaa Simba Simba , si mkajadili litimu lenu huko?

Kumbafu!
 
Back
Top Bottom