Naitabiria Yanga mafanikio zaidi ya Simba msimu wa 2023-2024

Naitabiria Yanga mafanikio zaidi ya Simba msimu wa 2023-2024

Kwa hiyo kuachwa kwa wachezaji wawili ndiyo useme usajili wa mhemko, tena mmoja mlikuwa mnamsema sana kuwa ni mzee na hafai, leo hii unamlilia? Umemuona Malone? Halafu umecopy maneno yangu ila mimi niliyasema kwa angle tofauti.
Bwashee, hata mimi ni mdau wa michezo. Hivyo hiyo kitu ya kusema nimecopy maneno yako, inafikirisha sana. Labda kama sina uelewa wowote ule na mpira wa miguu.

Halafu mimi sina sababu ya kulilia wachezaji wenu mliowaacha. Wewe umeniuliza, na mimi nikakujibu. Nje ya hapo, ninawaombea tu njaa mshindwe pia kwenye huu msimu. Hakuna kingine.
 
Mmevuruga kikosi na upepo ulikuwa upande wenu ila kikosi cha sasa ni cha kawaida saana.

Suala la muda wa kutosha wa preseason lilikuwa muhimu zaidi kwa Yanga kuliko Simba maana mna benchi jipya na mna maingizo mengi kwenye kikosi cha kwanza. Kina Diarra na Aucho wamejiunga lini na wenzao? Bado wachezaji wapya waliosajiliwa.
Subilia Tanga ndio utajua kama ayo maingizo mengi mapya unayosema kikosi cha kwanza yameclick ama ayajaclick, pacome, zouzou, nzegeli na yao yao ndio wachezaji watatu wapya watakaoanza kikosini na awawezi kuharibu backbone ya timu ya first 11 kwa wachezaji 9 waliozoeana, ingekuwa nusu ya kikosi wote wanaoanza ni wapya apo ungekuwa na point ya kujadili
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwahiyo wakitaka kumgusa anageuka jiwe?
Yani pale kwenye kikosi lazima atokee tu mana kocha mwenyewe anapigwa zongo anatulia. Umuhimu wa Boko mda mwingine unaletwa na utaalamu wa wapemba wa wete
 
NAUNGA MKONO HOJA.

UAJIULIZA ANAYEFANYA USAJILI WA MAWINGA ANAAKILI TIMAMU KWELI?????????

Mawinga. 2023
1. Peter Banda.
2. Jimyson Mwinuke.
3. KIBU Denis.
4.Said Ntibazonkiza.
5. CLOTUS Chama 10-11.
6. Aubin Kramo.
7. Essomba Onana.
8. Luis Miquesson.

Hili KOSA lilifanyika 2020.
Mawinga walikuwa kumi, ukiunganisha idadi Yao mchango WAO MAGOLi hayafiki hata 10.

1 Bernald Morison.
2. Perfect CHIKWENDE.
3. Hassan Dilunga.
4. Ibrahim Ajibu.10--⁷
5.peter Banda.
6.pape sackho
7. Dunkan Nyoni
8. Valentine Muhilu.
9. KIBU Denis.
10. RALY BWALYA 8-10--11.

UNAJIULIZA HUU USAJILI UNAFANYWA NA MTU MWENYE AKILI TIMAMU KWELI.
We choko Kila post unaweka Hilo likomenti lako acha ufala Upinde wewe
 
Mbumbumbu akili itawakaa sawa

Sent using Jamii Forums mobile app
Za mida?
Ihefu hawajambo, yule kocha wao amehamia Mtibwa, atatusaidia kumfunga paka kengele Manungu.

Tunaongoza ligi🤣🤣, tuko AFL na Ahly kesho, tuko makundi klabu bingwa. Sasa utacheza na Azam, safari hii wamejidhatiti ukishinda ni draw.

Sisi tukimalizana na Ahly tutakuwa tumeshafikia quality tunayotaka, halafu tutakutana na wewe🤣🤣. Mshauri Gamondi afuge nywele, maana atajikuna kipara achubuke siku hiyo.
 
Bado hamjasema.. na mtasema

Bao 5 zinawashaaaa sana
 
Kuna dalili mbaya toka pre-season hadi jana kwenye Simba Day nimeshaaza kuziona zinazoashiria kuwa Simba inaenda kuwa na msimu mbaya sana.

1. Tukirudi nyuma mwishoni mwa msimu uliopita, kipa Aishi Manula aliumia na kwa sababu za kijinga kabisa Beno Kakolanya, kipa mwenye uwezo akawa anakaa benchi tena katika mechi kubwa na muhimu sana. Hili tumelizungumza sana na nadhani kuna uzi nilishawahi kuuleta. Cha ajabu zaidi, inaonyesha hakuna juhudi zilizokuwa zinafanyika kutafuta kipa mbadala ili kipindi cha usajili kikifika asajiliwe, matokeo yake tumekuja kuokota kipa wa KMC dakika za lala salama.

2. Pre-season baadhi ya wachezaji kucheleweshwa kupelekwa kambini bila sababu za msingi. Baadhi ya wachezaji wapya walikuwa wanazungushwa kwenye matukio hapo Dar wakati wenzao wako kambini na wengine kina Chama na Baleke walichelewa kupelekwa kambini bila sababu za kueleweka. Hapo hapo inasemekana kocha alienda kwenye kozi fupi kwao Brazil (na kama wiki moja kabla alikuwa huko huko Brazil). Kimsingi timu imefanya mazoezi ya pre-season ya pamoja ya labda wiki moja tu.

3. Kwanini timu imejaza mawinga na kuzembea kusajili kiungo mkabaji na beki wa kushoto mbadala wa Zimbwe? Msimu uliopita niliona Simba imefululiza kusajili wachezaji wafupi kwa mkupuo. Nilibaki najiuliza huyu anayefanya usajili ana nia gani, hili halioni au ni makusudi haya? Msimu huu tumebadili gia, tumejaza mawinga, unajiuliza nia ni nini? Ukiangalia mechi ya jana dhidi ya Power Dynamos, utaona shida ya toka msimu uliopita pale eneo la kati ipo pale pale na hili litaisumbua sana Simba. Kuna wakati nilishauri Israel Mwenda ajaribiwe beki wa kushoto na kweli Simba ikatembea na ushauri huo lakini ukiangalia zile mechi alizochezeshwa nafasi hiyo kama ile na Coastal Union bado hakuwa comfortable kucheza upande ule. Ni sawa kumtumia hivyo kwenye dharura ila kwenye dirisha la usajili kulikuwa na nafasi ya kusajili mtu ambaye anaweza kucheza hiyo nafasi kwa ufanisi.

4. Kuendelea kumkumbatia Bocco. Kama mpira ni burudani, mimi siburudiki nikimuona Bocco akiwa uwanjani anachezea Simba hasa ukizingatia wachezaji wenye viwango, uwezo na ambao uchezaji wao unavutia na wanakupa matokeo kama Moses Phiri wapo wanasugua benchi. Mimi naamini Robertinho bado ni kocha mzuri sana na siyo yeye anayemkumbatia Bocco, naamini anafuata amri anayopewa kutoka juu yanayombeba Bocco na yanayompiga pini Phiri. Simba isitegemee mafanikio yoyote ya ndani au nje kwa kumtumia Bocco katika zama hizi. Ni misimu mingapi Simba imekwama na kugotea Robo huko CAF kisa mapungufu ya hawa kina Bocco, kwa nini wahusika hawajifunzi?

Nadhani kuna watu pale kwenye uongozi ndani ya Simba hawana mapenzi ya dhati na timu. Wameshikilia dhamana ya kuwapa furaha wanasimba ila pia wamejiandaa kuitumia dhamana hiyo kuwaumiza kwa maksudi kabisa wanasimba kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.

Yanga wana timu ya kawaida mno msimu huu ila pamoja na hilo kwa ninachokiona kinaendelea pale Simba, Yanga watakuwa na mafanikio msimu huu kuizidi Simba.

Nawasilisha.
Hakika ulichambua na kuijua mapema. Ukweli una tabia ya kujitetea.
 
Za mida?
Ihefu hawajambo, yule kocha wao amehamia Mtibwa, atatusaidia kumfunga paka kengele Manungu.

Tunaongoza ligi[emoji1787][emoji1787], tuko AFL na Ahly kesho, tuko makundi klabu bingwa. Sasa utacheza na Azam, safari hii wamejidhatiti ukishinda ni draw.

Sisi tukimalizana na Ahly tutakuwa tumeshafikia quality tunayotaka, halafu tutakutana na wewe[emoji1787][emoji1787]. Mshauri Gamondi afuge nywele, maana atajikuna kipara achubuke siku hiyo.
[emoji2772][emoji2772][emoji2772]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Ukishiba viazi usiropoke hovyo
 
Za mida?
Ihefu hawajambo, yule kocha wao amehamia Mtibwa, atatusaidia kumfunga paka kengele Manungu.

Tunaongoza ligi[emoji1787][emoji1787], tuko AFL na Ahly kesho, tuko makundi klabu bingwa. Sasa utacheza na Azam, safari hii wamejidhatiti ukishinda ni draw.

Sisi tukimalizana na Ahly tutakuwa tumeshafikia quality tunayotaka, halafu tutakutana na wewe[emoji1787][emoji1787]. Mshauri Gamondi afuge nywele, maana atajikuna kipara achubuke siku hiyo.
Madhara ya balimi
 
Back
Top Bottom