Najivunia ushamba na ulimbukeni huu ulinipitia mbali

Najivunia ushamba na ulimbukeni huu ulinipitia mbali

Kila mtu anafanya kile kinachomfanya afurahi, huwezi kuita hobby za wenzako "ushamba" , ni kitu watu wanapenda kushare furaha na huzuni zao na jamii inayowazunguka na wala sio ushamba kama ulivyoiita mtoa hoja.

Labda ungesema tu hauna interest na kujitupia mtandaoni ila don't term others as washamba kisa wewe hufanyi.
Ni kweli kabisa.
 
Baadhi ya mambo ambayo yakizidi sana huwa nayaona ushamba na ulimbukeni. Haya mambo mimi yamenipita mbali kabisa.

1. Kujipost WhatsApp status
Hata kama nitafanya jambo gani, hata kama nimepata nini cha mafanikio huwezi kukikuta status. Mwaka jana nimegraduate taaluma mbili tofauti lakini huwezi kukuta status. Acha status hata graduation sikuhudhuria(Japo sio ushamba)
Sijui nimenunua gari kali najisikia aibu sana kujipost. Hata picha tu ya gari sina, na zile zilizotumiwa na Mjapani nilishazifuta.

Kuna mdogo wangu alikuwa anapenda kupiga picha na gari anajipost. Nikamkataza.

Yule baby alikuwa anapenda kujiselfie na mimi halafu anajipost. Nikamkata kistaarabu tu baby don't do that. Hata kesho nikifanya harusi nadhani hakutakuwa na status.

Naona wenzangu wanapost matokeo ya watoto wao yaliyotoka jana. Mimi A tupu za wakwangu siwezi kuzipost, naona ulimbukeni. Ahadi ya zawadi niliyompa akipata A zote nitampatia, nitamtia moyo aongeze bidii na kumpeleka vacation ya kisima.

2. Kutumia elimu na kazi yangu kujiona bora
Nina mavyeti mengi tu lakini sio bora kuliko wengine. Sio bora kuliko mlinzi na mfagizi pale ofisini. Wakati wengine wakipita bila hata kumsalimia mlinzi na kusaini daftari getini. Mimi lazima nimjulie hali nijitambulishe. Hata akisema basi nenda tu, namwambia hapana nitasaini hapa na kule kwa Mkurugenzi nitasaini. Maana ndio utaratibu.

Tukiwa shamba mimi sio bora kuliko kibarua. Kwa hiyo msosi wa shamba utakula wote.
Pole sana unahitaji msaada wa kisaikolojia tena wa haraka sana ndugu kwasababu una tatizo la msongo wa mawazo ulio pitiliza na ukizembea kupata ushauri wa kisaikolojia utaishia kujitoa uhai wako.
 
Mkuu wewe kama mimi tuu
Kuna wanangu niliomaliza nao Telecom pale Cive walikua watu wa ku show off status ila mii wala

Nulipo piga electrical south africa wala hakuna ndugu aliyekua anajua an ni mtu wa kimya kimya..

Juzi nimeenda dubai lakini cha ajabu sijapiga picha hata kidogo. Mpaka mdogo angu anashangaa huyu blaza vipi ila naona normol tuu..

Maisha ya mtandaoni kujianika mi ndo siwezi kabisa aiseee
Hii ni nature niliyonayo toka advance nilipo piga A ya phy na chem wala sikua mtu wa show off zaidi zaidi waliokuwa and anapost matokeo yangu ni wale ndgu wa karibu tuu..
Sio normal io hali uliyo nayo yani sio normal kabisa ni una matatizo ya akili mkuu apo inabidi upate matibabu ya kisaikolojia ili io trauma bond ikutoke kichwani na uanze kufurahia maisha halisi
 
Sio normal io hali uliyo nayo yani sio normal kabisa ni una matatizo ya akili mkuu apo inabidi upate matibabu ya kisaikolojia ili io trauma bond ikutoke kichwani na uanze kufurahia maisha halisi
What is trauma bond
 
Kuonesha onesha kila kitu au mafanikio ni moja ya mental illness...

1. Tunaenda shule ili tujifunze na mwisho wa siku tukipimwa kwa mitihani tufaulu tena tufaulu vyema. Sasa kama wajibu ni kufaulu, kwa nini unataka tujue umefaulu wakati hilo ndio lengo la mtahiniwa yeyote?

2. Tunanua gari/magari ili iturahisishie kwenye suala la uchukuzi badala ya kutegemea usafiri wa umma utumie usafiri wako binafsi. Umefanya uamuzi wa kutoka usafiri wa umma kwenda binafsi, unatujulisha sisi wengine ili iweje?
 
Kuonesha onesha kila kitu au mafanikio ni moja ya mental illness...

Tunaenda shule ili tujifunze na mwisho wa siku tukipimwa na mitihani tufaulu tena tufaulu vyema. Sasa kama wajibu ni kufaulu, kwa nini unataka tujue umefaulu wakati hilo ndio lengo la mtahiniwa yeyote?
Na ata mtu ambaye hana furaha na maisha yake kiasi cha kushindwa kuyafurahia uyo lazima anaelekea kua kichaa kwasababu ya msongo wa mawazo na ukitaka kujua kuwa anaenda kua kichaa ndio kama hivyo yeye anajidai hataki ku Post lakini anaumia kuona wengine wana post sasa kama hapendi kupost kuna haja gani ya yeye kuongelea mada izo si akae kimya ili iwe serious kabisa yuko nje ya mitandao
 
Nipate chance ya kutoka kijijini huku nifike viwanja Kama Mapacha niwe nakula nyama nisijipost ?
Wanakijiji wataniheshimu kwa kipi Sasa ? Je watumishi wenzangu watajuaje Mimi kuwa mbali na kunywa Sana ulanzi sio kuwa sivijui viwanja vikali huku town ?

Kiukweli Mimi ndizo sababu za kujipiga picha na kupost daily nikiwa mjini ili niwaumize wanakijiji na wafanyakazi wenzangu ndiyo maana uwa nikirudi nawaonaga wanavyoniangalia kwa jicho la husda na wivu.

Wakiniangalia hivyo alafu muda huo nimetoka town nabadilisha na mwendo nakuwa natembea Kama nadunda Kama nimemaliza kila kitu ,hapo changanya mkononi nimeshika na mikate yangu miwili kutoka town awee uwa wanakoma ๐Ÿ˜€
 
Baadhi ya mambo ambayo yakizidi sana huwa nayaona ushamba na ulimbukeni. Haya mambo mimi yamenipita mbali kabisa.

1. Kujipost WhatsApp status
Hata kama nitafanya jambo gani, hata kama nimepata nini cha mafanikio huwezi kukikuta status. Mwaka jana nimegraduate taaluma mbili tofauti lakini huwezi kukuta status. Acha status hata graduation sikuhudhuria(Japo sio ushamba)
Sijui nimenunua gari kali najisikia aibu sana kujipost. Hata picha tu ya gari sina, na zile zilizotumiwa na Mjapani nilishazifuta.

Kuna mdogo wangu alikuwa anapenda kupiga picha na gari anajipost. Nikamkataza.

Yule baby alikuwa anapenda kujiselfie na mimi halafu anajipost. Nikamkata kistaarabu tu baby don't do that. Hata kesho nikifanya harusi nadhani hakutakuwa na status.

Naona wenzangu wanapost matokeo ya watoto wao yaliyotoka jana. Mimi A tupu za wakwangu siwezi kuzipost, naona ulimbukeni. Ahadi ya zawadi niliyompa akipata A zote nitampatia, nitamtia moyo aongeze bidii na kumpeleka vacation ya kisima.

2. Kutumia elimu na kazi yangu kujiona bora
Nina mavyeti mengi tu lakini sio bora kuliko wengine. Sio bora kuliko mlinzi na mfagizi pale ofisini. Wakati wengine wakipita bila hata kumsalimia mlinzi na kusaini daftari getini. Mimi lazima nimjulie hali nijitambulishe. Hata akisema basi nenda tu, namwambia hapana nitasaini hapa na kule kwa Mkurugenzi nitasaini. Maana ndio utaratibu.

Tukiwa shamba mimi sio bora kuliko kibarua. Kwa hiyo msosi wa shamba utakula wote.
Ila Mh. OKW SUNZU BOBAN umegraduate nini isije kuwa umeilamba ile CPA original.
 
Back
Top Bottom