Najuta kuwekeza kwenye kiwanja na nyumba ya mwanamke

Mwanamke mwanajeshi pngwe mwanaume anaendesha bajaji, mwanaume islam, Yule dada anakula kitimoto, anapika pale pale, Kaka zangu tafuteni pesaaa, natamani niongee nao Ila nitaonekana naingilia Mambo yao, na wafatilia yaaani.
 
Umenikumbusha mbali. Kuna jamaa naye alikuwa na mke Mmachame Kila siku ugomvi jamaa anaamiwa aondoke nyumba yake. Mwamba katukanwa na kudharaulika sana ukizingatia wote wamechangia ujenzi . Walikuwa wamezaa mtoto mmoja, Jamaa akaona ni heri aondoke akaanze maisha upya.

Jamaa akaoa upya maisha yakaenda. Mwanamke aliyeona nyumba ndo Kila kitu, kaumwa Mwaka Jana amefariki. Jamaa kaudhulia msibani kiroho safi na heshima ya shada kapewa. Hii Dunia tunapita hakuna utakachoondoka nacho.

Neema tu ya Mungu tunapumua hatujui kesho yetu.
 
Mwanamke mwanajeshi pngwe mwanaume anaendesha bajaji, mwanaume islam, Yule dada anakula kitimoto, anapika pale pale, Kaka zangu tafuteni pesaaa, natamani niongee nao Ila nitaonekana naingilia Mambo yao, na wafatilia yaaani.
Huu ni unyanyasaji, kwa nini aliolewa sasa
 
Kataa ndoa , ndoa ni utapeli huu ni ujumbe wa kinabiii sna kwa kizazi hiki kiovu , hamsikii tu au mpaka mpate ishara ole wao kizazi hiki chenye kupenda ishara , na hamtapa ishara isipokuwa ishara ya Yona.
 
Wanawake wote huamini wanaume tunakufa mapema kabla yao
Ni majinga. Na ndiyo hayo yakiona unazeeka huku unanawiri yanashikwa na wivu yanaanza kuiwinda roho yako ili ufe kwa lazima.

NB;
Wengi wa wanawake wa hivi ni wembamba, slim thick, na wale wanene walio fake mwili, na wenye makalio ya kufake na kila kitu.

Wanawake wanene kiasi na wanene kabisa, wengi ni safi! Nawapenda sana.
 
Story yako haitofautiana na ya jamaa yangu mmoja. Yeye alijenga mwanzo mwisho nyumba kwenye kiwanja cha mkewe. Hakuchukua muda baada ya nyumba kukamilika na wao kuaamia vikaanza vitimbwi ndani, mara paaaap akapata ugeni mkubwa wa mashemeji zake jamaa.
Wakisisitiza jamaa ahame kwenye nyumba.

Jamaa aliondoka akiwa na begi lake tu, huku akiendelea kulipa mkopo wa benki alioingia kipindi anafanya ujenzi wa nyumba hiyo.

Wanakwetu karudi magetoni.
 
Mwanamme hupaswi kugombania mali na mwanamke. Kwanza mshukuru huyo mwanamke ana akili ya kujenga watoto wako wanakaa pazuri na hakuombi hela ya kodi.

Hupaswi kuwa inferior eti kisa mwanamke kakopa hela kajenga nyumba ndiyo maana anakunyanyapaa. Wewe timiza majukumu yako kama mwanamme, Na wala usiteteleke.

Kama akizidisha dharau na hakuheshimu, ondoka nenda kaanze upya. Hapo ujue ya kwamba hakutaki na hana mapenzi na wewe ila siyo kwa sababu anamiliki nyumba.

Ukiwa unapambana kivyako utakuwa na amani watoto wako wanalala pazuri na hela ambayo ingelipa kodi kwa ajili ya familia yako kuishi ifanyie maendeleo mdogo mdogo.

Hiyo nyumba ata akiuza watoto wako hawatakufa njaa na pia kama hajauza hiyo nyumba watarithi watoto wako.

Mwanamme hupaswi kugombea mali na mwanamke, ni mwiko. Cha mwanamke ni cha watoto wenu.
 
Huu upumbavu wa ndoa unasababisha wanaume wengi wanaishi kama wapangaji kwenye hii dunia yetu nzuri.
 
Katika mambo ambayo siwezi kufanya ni kuchangia mambo ya maendeleo na mwanamke.

Akinunua kiwanja, nawe nunua jenga.
Mwanamke akikuambia tuchangie pesa tununue kitu fulani. Kataa kwa herufi kubwa.

Mwanamke anakubali kuishi na wewe kwasababu unauwezo wa kumtimizia mahitaji yake si vingenevyo
 
Haya mambo uliyaandika ndiyo yanafanya ndoa za siku hizi kuwa ngumu sana.
Wazee wa zamani, mwanamke akizingua anaondoka na mabegi yake anawaacha watoto ila siku hizi wanaume kama mabinti.
Siwezi kuondoka nikaacha mali nianze upya.
 

Nataman kusikia kutoka kwake pia

Nikasimamia ujenzi nyumba ikasimama ingawa kuna vitu vilikuwa havijakamilika nikaanza kuingia gharama kumalizia nyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…