1. Mkuu, kwa imani yangu inanieleza kuwa, usichopenda kufanyiwa basi usimfanyie mwenzio.
2. Leo utaona huyo mtu unammudu, mtu akishatambua uovu anaofanyiwa, yupo tayari kulipa, huwezi kujua anafahamiana na nani ama nani atamsaidia ili kulipa.
3. Kesi ya ugoni, utakachofanyiwa hakina tofauti na mwizi.
4. Utakuja kuharibu familia yako daima kwa tamaa hizi ambazo umezishikilia kwa mke wa mtu.
5. Unaweza ukasoma haya yooote na bado ukajipa imani kuwa hayawezi kukutokea, unajua nini? Ulizia wooote waliowahi kupatwa na madhara ya ugoni, wameshawahi kufkiria kuwa watakamatwa?
6. Umemuoa mke wako, mpende na kumheshimu sana. Heshimu mama yako mzazi, heshimu pia mke wako.