Najuta kwa mara nyingine kuwa na mahusiano na mke wa mtu

Najuta kwa mara nyingine kuwa na mahusiano na mke wa mtu

1. Mkuu, kwa imani yangu inanieleza kuwa, usichopenda kufanyiwa basi usimfanyie mwenzio.

2. Leo utaona huyo mtu unammudu, mtu akishatambua uovu anaofanyiwa, yupo tayari kulipa, huwezi kujua anafahamiana na nani ama nani atamsaidia ili kulipa.

3. Kesi ya ugoni, utakachofanyiwa hakina tofauti na mwizi.

4. Utakuja kuharibu familia yako daima kwa tamaa hizi ambazo umezishikilia kwa mke wa mtu.

5. Unaweza ukasoma haya yooote na bado ukajipa imani kuwa hayawezi kukutokea, unajua nini? Ulizia wooote waliowahi kupatwa na madhara ya ugoni, wameshawahi kufkiria kuwa watakamatwa?

6. Umemuoa mke wako, mpende na kumheshimu sana. Heshimu mama yako mzazi, heshimu pia mke wako.
Hivi hata boyfriend akimfumania girlfriend nao tunaita ugoni ?
 
Braza wewe ni Sikio la Kufa, halisikii Dawa.

Kujuta kunakuja kwa kuacha kabisa hicho kitendo.

Take it from me. Majuto yake ni Makuu Mno... InFact: Hayaelezeki.

NDOA NA IHESHIMIWE NA WATU WOTE.
 
Kwamba mume wake ni mtu wa kitengo fulani ila unaweza kumhandle tu bila shida, ebu fanya kile unachoona kinafaa kwako
 
Mimi na michepuko Ni damu damu,
Ila kwenye Wake za watu mimi HAPANA[emoji3525]
 
Kamwe usijisifie kulala na Mke wa Mtu. Kuna madhara ama laana kubwa zitakuandama kabla ya kuja kufumaniwa.

Ikimbie zinaa.
 
Yoyoyoyooo[emoji849]Rudia tena - Unasema unammudu? unaonekana una uzoefu na wake za watu ila jihadhari ndugu, Kuna jamaa alijifanya mbabe kama mfano wako hiivyo hinvyo, ukweli mpaka sasa naandika hiki Jamaa ana kojoa usaha na amekata tamaa hajui anaponea wapi, Hosptl amemaliza anapata nafuu tu kidogo inarudia, mkewake nae amegundua kuwa mumewake shida nimke wamtu, [emoji125][emoji125][emoji125]
 
"Nimegundua mme wake pia ni mtu wa safari kama mimi tu na yupo kitengo fulani na nammudu vizuri kabisa, hivyo hawezi kuwa tishio kwangu hata kidogo."

Acha huu ubwege, ukijua hivi wenzio wanajua vile.

Sent from my COR-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Kwa mfano Kama Ni mke wangu nikigundua ,siwezi kukusamehe kabisa mke anauma,hakuna mtu atakuvumilia katika Hilo,siku mumewe akijua utakuwa umejichimbia kaburi
 
Ukitembea na mwanamke wa mtu unaweka Roho yako rehani huwezi jua mwenye Mali atakufanyia nini,hata uwe Kama Goliath huwezi kujua akili ya mtu inawaza nini,ukijiona mkora jua kuwa Kuna wakora zaidi yako,mke wa mtu simu.
 
Back
Top Bottom