Nakereka sana kusikia na kuona Rais Samia akiitwa au kuandikwa Dr. Samia

Nakereka sana kusikia na kuona Rais Samia akiitwa au kuandikwa Dr. Samia

Mkuu, wakuu wa mihimili mingine ya dola, wote ni "PhD holders" kwa ili kufunika kombe CCM wameona naye pia wamtambulishe kupitia "prefix" hiyo ya udaktari wa falsafa.

Makamu wake pia ana jiwe hilo la kitaaluma, kwa jinsi unafiki na umbumbumbu ulivyotamalaki ndani ya CCM, wameona ni vyema naye aonekane pia apewe njia ya mkato na kuanza kutambulishwa kama sehemu ya "elites"

Honestly huwa sioni tofauti ya wenye PhD na wenye elimu ya darasa la 7 hapa nchini.
 
Tatizo wala siyo hilo. Naumia kuona jina la F4 failure linaanzia na doctor (PhD).

Mi nahisi tuanze na swali. Wewe unaelewa nini hasa kuhusu „ Doctor of Philosophy ( philosophy-love of wisdom)? Mana haya mateso Sio ya uchungu wa Elimu bali ni unazi wa kisiasa. Ungetumia bundle lako hata kuelewa why of hizo PhD za heshima baada ya kwanza kuelewa kuhusu maana mtu kupata „PhD“ yenyewe kwa research nk.
 
Hili linafanyika ili kuendelea kulinda heshima ya ngazi hii kubwa ya elimu.
Mtaje jina huyo Profesa tumfahamu.
  • Kwani wale waliomtunuku wao hawalijui hilo isipokuwa yeye?
  • Kwani ametunukiwa tu baada ya kuonekana anavaa mavazi virzuri na kupendeza au kuna kitu kikubwa ambacho wasomi waliobobea wameridhika nacho na hivyo kuamua kumtunuku PhD ya heshima?
  • Heshima hiyo anayoisema yeye, ni heshima ya aina gani sasa wakati wote wanaotunukiwa PhD hiyo wanatunukiwa PhD ya heshima?
 
Mimi wajibu wangu ni kutupia ka video ka Dr.😁😁😁
 
Unashangaa hili, je kuitwa raisi wa serikali ya awamu ya sita badala ya raisi wa sita wa serikali ya awamu ya tano! Hii ndio Tanzania. Kama aliyetunukiwa anapenda kuitwa hivyo machawa watafanyeje sasa?
Hakuna popote kwenye katiba awamu imetajwa.
 
KUNA WATU WAMEUMIA SANA NA WATAENDELEA KUUMIA KWA MIKUNJO YA ROHO ZAO KAMA BALBU ZA UTUMBO
 
Angalia hapa Sexless Ikulu imejiondoa kwenye hiyo dr.
IMG_20230119_135749.jpg
 
Daah! Unaona Sasa? Kumbe Dr inatajwa na kuandikwa na machawa tu
Ndiyo hiyo, nilianzisha uzi kuhusu hiyo honorable doctor wenye jf wakaukwapua uzi fasta!.

Heading ilikuwa...

"IKULU YAJIWEKA PEMBENI NA HONORABLE DOCTOR"
 
Heading ilikuwa...
"IKULU YAJIWEKA PEMBENI NA HONORABLE DOCTOR"
Ahaa! Mm nilibahatika kuona pia ulikuwa umeweka na tweet ya ikulu ikimtaja Samia kwa kuanza na mheshimiwa.
 
Kuna profesa mmoja (jina silikumbuki) ametoa ufafanuzi hivi karibuni kuwa mtu akipewa PhD ya heshima jina lake halipaswi kuanza na Dr. (Mfano Dr. Samia) badala yake liandikwe Samia (PhD hons).

Hili linafanyika ili kuendelea kulinda heshima ya ngazi hii kubwa ya elimu. Sasa kwann wanaccm wanainajisi elimu mchana kweupe? Ni kujipendekeza kunawapumbaza?

Tunawavunja moyo wale waliopo vyuoni wakiumiza vichwa na kukesha usiku kucha wakisoma ili kuifikia hatua ya kupata PhD.

Natoa onyo kwa wanaccm na machawa wote kuwa rais Samia hapaswi kuitwa Dr. Samia.

Nimemaliza.
Mbunge wa huko Tanga mh Rashid Shangazi amesema PhD zinauzwa kama njugu kwani yeye binafsi aliambiwa atoe US Dollar 1500 atunukiwe.

Shangazi amesema Dola 50 ni Usajili, Dola 550 Doctorate degree yenyewe, Dola 250 Joho na vitu vinginevyo Jumla kuu inafika Dollar 1500.

Mh Shangazi amesema ukiwa na US Dollar 1500 faster unakuwa Dr Rashid Shangazi.

Source Jambo TV
 
Back
Top Bottom