Nakusudia kuishtaki Serikali (TCRA) kuzima Simcard za wateja wa mitandao

Mbona hamkulalamika usajili ulipoanza? Kwanini mwalalamika mwishoni?
 
Na uhakika utakuwa mmoja wa wale wa tuma kwenye namba hii 😆😆😆😆😆, huu ni ushamba. Unachotakiwa kufanya ni kuomba, hata Mimi ukifungua Kesi na Mimi nakufungulia kwa kuwaibia Watanzania kwa kutumia cm.
Hivi ikitokea zoez la kuzima sim likafanyika kama hivi na bado watu wakapokea ujumbe huo huo kwa No hizo hizo na serkali ikashindwa kuwakamata, utasemaje? Kuna haja ya kuwaelimisha wananchi pia kuhusu umakin kwa kila jambo. Uarifu huu ni matokeo ya elim ndogo mno kwa wahanga na uzembe pia. Nchi jiran tu kenya humwibii mtu kizembe hivi. Na wizi hubadilika na huenda ikaja mbinu mbaya zaid. Mpaka leo naamin mambo ya tuma humu si sehem ya sabab za mkazo wa usajiri huu. Basi tu maisha yamekuwa siasa na siasa imekuw maisha.
 
Kwani haya hayawei kufanyika leo? Hayawezi kuwa forged leo?
 
Vitambulisho vya zamani hizo data zilikua zipo kama hardcopy, vitambulisho vya taifa wanascan kwa machine zinaingia kwenye computer, huwezi chukua karatasi za zamani za fingerprints ukaziscan, fingerprint scanner zinahitaji kidole sio karatasi.

Tatizo ni technology tu, hizo data hawana katika format inayotakiwa ndiyo maana wameamua kutengeneza mfumo moja ambao ni standard sasa hivi ambao dunia nzima wanatumia, so nenda kafanye acha lawama.
 
Hivi idara ya uhamiaji wana hakiki au wana gonga muhuri tu. Hivi wana nyenzo gani wanatumia kutambua huyu ni mtanzania au siyo?

Kuhusu affidavity hata sasa zinatumika. By the way ni nyumba ngapi zina namba? 90% ya wakazi wa dar wanahama hama kila siku, hivi mtu anapo hama taarifa zake za makazi huko NIDA pia zinabadilika?

Mtoa mada yuko sahihi, serikali haijajipanga na inatumia resources vibaya. Information must be captured and stored once...
 
mie mpaka sasa nawachora mnavyohangaika na kusajili simcard! sina muda huo na hawatagunga!
 
Mchakato wa vitambulisho vya taifa ni muhimu kwa usalama wa nchi yetu, kwasasa kabla ya kutoa kitambulisho unafanyika uchunguzi tofauti na jinsi zinavyotolewa leseni za udereva na vile vya kupigia kura, wale wanaotiliwa shaka wanachunguzwa zaidi.

Ushauri.
NIDA hawatozi hela yoyote kwenye huduma yao, kwa uzoefu wangu serikalini, taasisi zinazotegemea ruzuku kwa 100% hua zinakumbana changamoto ya fedha na vitendea kazi kutokana na ukiritimba uliopo kwenye kupata fedha toka mfuko mkuu, serikali iwapatie fungu la kutosha tena kwa wakati na iwaongezee nguvu kazi.
 
Kigezo ni kimmoja kimataifa ni ID ya taifa.
Tokea uhuru jambo hilo ilipuuzwa.Japo Kenya ilikuwa inatoa ID.
ID inaweka msukumo wa kuwa na cheti cha kuzaliwa.
ID inatumika kupewa Passport, ajira, mikopo,kupiga kura,driving license, dhamana,bima,hati za mali,kufunga ndoa,kufungua account bank n.k
Takwimu zake ni kiunganisho cha mtu kutambuliwa kitaifa hadi kimataifa.
Serikali itaendelea kubeba lawama kwa kupuuza ID kwa muda mrefu bila sababu ya msingi.
Japo tunaambiwa ni zoezi endelevu ni ukweli usiopingika kuwa NIDA haina nyenzo,watu,fedha za kutosha.Ilitakiwa Marshall Plan.NIDA ina umuhimu hata kuliko kuhamisha makao makuu kwenda Dodoma.
Historia itawahukumu.
 
Mkuu nawe pia moyoni mwako umeamini kabisa kuwa ni kweli fingerprints zishachukuliwa sasa kuna hoja gani ya nguvu ktk suala la ukweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani tuwe wawazi kwenye kusajili line kwa kitambulisho cha taifa wamekurupuka sana wao walitakiwa wawawezeshe NIDA wawe kwenye kila makao makuu ya tarafa au kata ili iwe rahisi kwa kila mtu kufika ,kuna maeneo Tanzania hii mtu anatumia zaidi ya elfu 30 kufika wilayani
 
Kweli bwana zile pesa ambazo bwana yule alijengea uwanja wa ndege kwenye majaruba ya mpunga zilitosha kabisa kuwawezesha NIDA
 
Kwa hiyo National ID ndo itatumika kupiga kura?
Kama kulikuwa na makosa kwa nini Vitambulisho vya kupigia kura havijabadilishwa na uchaguzi Tayari umefika?
Huoni kuwa Rais wa Tanzania anachaguliwa na Warundi ndo maana ana tabia za kirundi, sasa ujuaji wangu uko wapi?
Hebu jibu swali langu, Kwanini Vitambulisho vya kupigia kura bado havijabadilishwa hata baada ya kugundua kulikuwa na makosa ya uhakiki? Na mwaka jana vimetumika tena kwenye local government elections?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…