Nakusudia kuishtaki Serikali (TCRA) kuzima Simcard za wateja wa mitandao

Hili la NIDA ni upigaji wa pesa tu wameutengeneza kwa makusudi.
 
Mkuu kuna sababu gani ya kukusanya taarifa ambazo tayari unazo?. Nadhani hilo ndo swali la msingi la mleta mada.
 
My Son drink water,

Umesahau na passport, yaani mpaka hivi vidole vyangu vimeanza kufutika hizo alama kila siku wanaviramba, hata ukisafiri pia wanaramba vidole, I’m tired
Afadhali mkuu na wewe umeliona hilo, hili ni taifa la mambumbumbu kupindukia, majitu yapo tu hata kuhoji hayataki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si kweli, ndugu Yangu alipoteza voting ID akapewa mpya bila Fingerprints walichofanya ni ku retrieve tu data zake na kumpiga picha, fingerprints walikuwa nazo Tayari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwa na national ID ni jambo la muhimu. Tatizo NIDA inafanya kazi kimasikini sana na hawakujipanga kama serikali kwa jambo hili. Huwezi kusema Watanzania wote 18+ wawe na ID ndani ya muda mfupi huku hujawekeza vya kutosha kwenye rasilimali vifaa, ofisi na watu kwa ajili ya kazi hiyo. Ilitakiwa kila ofisi ya kijiji na mtaa pawe na kitengo cha NIDA kwa kazi hizi.
 
Pia sheria ya mawasiliano uvitambua vitambulisho vinne yaani unawezasajili kupitia driving license,passport,national id au kadi ya kura na hivi vyote vina fingerprint,labda wanna lengo nyuma ya pazia.Kupitia sheria hii wanaweza wakasthakiwa kama watafungia watu Simu.
 
Asante sana !!! Sasa mleta mada ajipime kama anatosha kujinasibu kuwa yeye kashaitafuta elimu na kuipata ama bado anazurula na kijiba rohoni kuitafuta elimu.
 
NIDA wangeachiwa zoezi la kuprint tu id kwanza hawana elimu ya utambuzi kujua yupi raia yupi sio,jukumu la taarifa wangeachiwa polisi na uhamiaji kwani wako nchi nzima wakusanye taarifa wanazituma NIDA
 
Hili ndio jibu sahihi kwa mtoa mada
 
NIDA wangeachiwa zoezi la kuprint tu id kwanza hawana elimu ya utambuzi kujua yupi raia yupi sio,jukumu la taarifa wangeachiwa polisi na uhamiaji kwani wako nchi nzima wakusanye taarifa wanazituma NIDA
Ukitaka kuchunguza kwa undani uraia wa watu wote itakuchukua milele. Kinachofanywa na NIDA ni sahihi kabisa, wanafanya 'quick screening' kama taarifa zako zinaviashiria vya udanganyifu ndipo wanafanya uchunguzi zaidi, hata ukienda kuomba passport uhamiaji utaratibu ni huohuo, hawapotezi muda na mtu ambaye taarifa zake hazioneshi shaka yeyote.
 
Ok' huenda kama taifa watawala wanahitaji information zetu zifahamike, tunafanya nn? Wapi? Na nani?. Tatizo ni hiyo deadline. Why? Kwann usingetafutwa mfumo endelevu urenew kwa mfumo huo wa vidole? Kwann tukimbizane na deadline? Line mpya zingeweka na mfumo wa vidole, mtu akipoteza mfumo wa vidole utumike kurenew, mtu akihitaji msaada basi aambiwe sajili kwa mfumo kwanza ndo usaidike, taratibu mpaka wote wanasajili. Sasa speed yote ya nini?
 
Hebu hii iweke vzr Mkuu

MTC | 101| [emoji769]
 
Utatekwa na kupotezwa ukifungua hiyo Kesi, Tuna Rais hatari sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hii nchi katika taasisi nyingi za serikaki na wizara zake zinaendeshwa na watu wajinga wajinga. Mambo bado yanaendeshwa kwa kutumia mifumo ya zamani sana.

Hakuna mawasiliano mazuri wala uhifadhi wa kumbukumbu wa pamoja (central system); na ndio maana kila siku mambo yale yale yanajirudia.

Ni aibu kwa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…