Nakusudia kuishtaki Serikali (TCRA) kuzima Simcard za wateja wa mitandao

Na sio watanzania wote wenye driving license na sio wenye kadi ya mpiga kura hili la nida itawalazimu watu wengi waingie kwenye mfumo.hakuna kitu kinachotafutwa Bali ni mabadiliko ya dunia na maendeleo yake ndio yanatulazimisha iwe hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani haya hayawei kufanyika leo? Hayawezi kuwa forged leo?
Kama ni rahisi hivyo sasa analalamika nini, si aende aka-forge apate kitambulisho cha NIDA asajili SIM card yake?
 
kama hoja ni usahili wa idara ya uhamiaji,je passport zinaruhusiwa kutumika kwenye usajiri wa laini?
Mkuu tuliza kichwa rudia kusoma vizuri njoo uchangie.
Hapo kuna hoja kuu mbili nimezigusia. Nakupa kazi zitafute uje ujadili.
Nafikiri masomo ya lugha yoyote sehemu ya ufahamu (comprehension) ukiwa shule halikuwa tatizo kwako, unasoma kifungu au habari flani kisha unajibu kulingana na ulivyo ielewa hiyo habari.
 
Mbona unadabili gia angani?
Madai yako hasa ni kuhusu vitambulisho vya NIDA? Au vitambulisho vya mpiga kura?
Maelezo yako ya awali ni kuhusu kutokuwa na umuhimu wa vitambulisho vya NIDA, ukapewa umuhimu wake umekuja na hoja nyingine kabisa ambazo kiujumla tunaweza kusema ni maboresho ya daftari la mpiga kura.

Na huku sasa ndio vijana wanaita kuhamisha magoli baada ya kubanwa na kukosa hoja kwenye malamiko yako ya awali.

Sasa turudi kwenye malalamiko yako ya uboreshaji daftari la mpiga kura, nikimaanisha hayo yote ya kudhibiti udanganyifu kwenye vitambulisho vya mpiga kura, kimsingi nakubaliana na wewe, tena ongeza na madai ya tume huru ya uchaguzi.

Kwenye siasa tubaki na siasa ila kwenye mambo ya kitaaluma kama ya kiusalama tujenge hoja au kukosoa au kushauri kama tuna uelewa mpana wa jambo husika, au kama hiyo ndiyo taaluma yetu.
 
NIDA wangeachiwa zoezi la kuprint tu id kwanza hawana elimu ya utambuzi kujua yupi raia yupi sio,jukumu la taarifa wangeachiwa polisi na uhamiaji kwani wako nchi nzima wakusanye taarifa wanazituma NIDA
Kwani sasa inafanyikaje kuhusu kuhakiki uraia wa muombaji?
Mbona unacho pendekeza ndicho kinachofanyika toka ulipoanza mchakato wa NIDA mwanzo wa mradi?
 
Hakuna la maana kinachofanyika hakuna tofaut kupata voter id,ili kupata voter id unahitaji kutambuliwa na mkit mtaa au kijiji mbele ya mawakala wa vyama vya siasa.Hvyvyo kwa sasa usipokua na vyet vya kuzaliwa mwenyekiti atakuandikia barua utambulisho bas hvyo uhamiaji ni kugonga mhuri tu na maswali mepesi.Tangu jiwe aingie madarakani viongozi wa serkali wameacha kufikiri na kuheshimu sheria.Wanamuangalia jiwe kichwa chake kikoje na wamempatia kweli.Yeye anajiona amewaweza lakini kumbe wanamuona babu mwenye vituko hvyo ukitaka mali yake msifie tu
 
Si kweli, ndugu Yangu alipoteza voting ID akapewa mpya bila Fingerprints walichofanya ni ku retrieve tu data zake na kumpiga picha, fingerprints walikuwa nazo Tayari

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa mkuu hayo ya ndugu yako yanahusika vipi? Naongea hii ni kazi yangu najua fika fingerprint technology ilivyo na kwa nini wanachukua upya kwa mashine mpya, notice wanatumia machine zilezile kila kona. Voting ID haihitaji kurenew fingerprints kwa kua copy waliyonayo ni ya picha sio format inayotakiwa na hizi machine mpya. Ni ngumu kukuelezea ila we elewa fingerprint za sa hivi original format yake inayotunzwa kwenye computer sio kama picha, ingawa wanaweza kuprint ukaona picha, ina data nyingi zinazotumika kukuidentify unapoweka kidole kwenye machine. We bisha ila naishia hapa maana naongea kitu ambacho nina uhakika nacho 100% nimefanya kazi kwenye upande wa software ya kusoma fingerprints
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fingerprints za Leseni na Kura hazipo makini kama hizi za Nida.
Issue sio fingerprints tu bali taarifa zenye uhakika kwamba mtu akikutafuta kwa Nida atakupata bila wasiwasi, yaani watu wanaqeza kuwakamata hata ndugu zako uliowainguza kwenye Nida, yaani hadi mwenyekiti wako wa kijiji anajulikana. Haya nambie kwenye leseni au kwenye kura wanaweza kumfahamu ndugu yangu au mwenyekiti wangu wa kijiji?
Acha ujinga, watu tuna akili.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni wa kuonea Huruma kabisa, unashindwa kujibu hoja unakimbilia sympathy ya kulia lia eti nje ya nchi sijui kumefanya nini, hata Tanzania ni nje ya nchi Ukiwa nje ya Tanzania.
Jibu hoja kwa hoja juu ya ujinga wa viongozi wenu, ndo maana wakizidiwa hoja wanakimbilia kuua watu kikatili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maboresho gani bila kuchukua fingerprint tena, kwa hiyo mtakuja na scene ya kuboresha tena National ID, nyie watu kwa kuharibu pesa ya nchi hamjambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo Database ya voter's ID ime expire?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jitafakari ulicho andika!!
Kitambulisho cha NIDA ni mradi ulioanza kabla ya Magufuli kuwa raisi wa JMTZ.
Wala yeye sie alie agiza au kuidhinisha mradi huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…