Nakusudia kuishtaki Serikali (TCRA) kuzima Simcard za wateja wa mitandao

Jitafakari ulicho andika!!
Kitambulisho cha NIDA ni mradi ulioanza kabla ya Magufuli kuwa raisi wa JMTZ.
Wala yeye sie alie agiza au kuidhinisha mradi huo.
Ni wapi nimeandika mradi id za NIDA umeanzishwa na Magufuli au mihemko yako?So far hata kama ulianzishwa na jk kwa sasa utekelezwaji ni mbovu.Hvi unajua sheria zinazobana watumiaji wa simu kujisajiri zimetaja vitambulisho vingi lakin serkali imekomaa na Nida wakifikiri watawabana wanaoikosoa serkali.Haya matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za nchi.Umeona jina la JPM umeweuka umeacha kusoma kilichoandikwa unakurupuka tu
 
Wewe unathibitisha kile kilichosemwa na mtoa mada kuwa watanzania ni wasahaulifu au hujui kuwa Magafuli alisha apa kuwa akiwa rais wananchi wa taifa hili "watalima kwa mano".

Anaposema wenye akili wameshausoma mchezo maana yake ni kwamba kampeni hii ya kuzima simu ni moja ya utekelezaji wa kiapo cha kuwalimisha watu kwa meno. Yaani inatafuta kila sababu ya kuwahenyesha na kuwayumbisha wananchi.
 
Mimi kwetu Mbeya lakin kitambulisho nimeandikia Dar na mwenyekiti aliyeko ni wa Dar.hivi unadhani wenyeviti wanawajua wote waliowagongea mihuli?Kama unadhani eti fingerprint ndio inayoweza kumkamatisha mtu basi endelea kujidanganya.Bado kuna watu kibao hawakuweka taarifa zote na sasa wana vitambulisho.Halafu kwa ujinga wa mtu eti anadhani kuhojiwa na wale uhamiaji inaweza kupelekea kujua waamiaji haramu?Si kweli kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani sasa inafanyikaje kuhusu kuhakiki uraia wa muombaji?
Mbona unacho pendekeza ndicho kinachofanyika toka ulipoanza mchakato wa NIDA mwanzo wa mradi?
Polisi uhamiaji wako everywhere tofauti na NIDA
 
Vipi passport ya kusafikiria ambayo inatolewa na uhamiaji leo ukienda kusajilia laini au kununulia laini mpya wanakataa ..


Nipe majibj..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
My Son drink water,
Nia ni kuhakikisha kila mtanzania 18+ ana kitambulisho cha uraia
Kwanini wasipige Kambi kwenye hospitla zote kuhakikisha kila anaezaliwa anapewa kitambulisho chake kwanza Cha taifa ndani ya wiki moja ili tusitengeneze kizazi kingine kitakachokuja kufikia miaka mpaka 18 Hana hata kitambulisho...


Ubaya hii nchi inaemdeshwa Kijinga Sana , kila kitu kinaenda peke yake na shaghala baghala ... Leo tuna passport ambazo ni electronic zikiwa na taarifa zote za mtanzania mpaka finger print lakini ukienda na hiyo document kufungulia account benk unaambiwa uwe na kitambulisho Cha NIDA (Mungu wangu )... Eti wanakwambia nida Ina fingerprint



Daaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Umepotosha kuwa mtu hakutakiwa kuwasilisha cheti cha kuzaliwa. Hata sasa hivi si kila Mtanzania ana cheti cha kuzaliwa.
 
Asante sana jamani mtanzania mwenzangu
 
Yes wanaweza
 

Mkuu pamoja na ukweli uliosema, makazi iwe mjini au kijijini sio taarifa ya kudumu. Umemuelewa vizuri sana mchangiaji - alichomaanisha sio kuwa vitambulisho hivo ni mbadala kitambulisho cha taifa bali ni kitambulisho halali kwa sababu ya kukidhi vigezo muhimu. Sijui kama itafikia wakati tuseme ili uwe na DL lazima uwe na kitambulisho cha taifa.

Mleta mada anazungumzia mifumo inayoshirikiana. Si sawa kuzuia anayetafuta hati ya kusafiria sawa na unavomzuia anayetaka kusajili namba ya simu huku akiwa na DL au voter ID ambavyo vyote vina biometric requirements.

Habari ya mambo madogo kuna na complex solutions!!
 
Wewe nawe hakuna ulichokiandika hapa ila ni kuthibitisha "maajabu" ya watanzania kama mtoa mada anavyopata tabu kutuelewa.

Unaposema kitambulisho cha mpiga kura hakikuhusisha uhakiki wa uraia maana yake ni sawa na kusem "anayestahili kupiga kura si lazima awe raia bali ni mtu yeyote anayejiandikisha". Je, katiba ndo inaelekeza hivyo? Je, kushindwa kufanya ukakiki wa uraia wa mpiga kura sio uzembe?

Je kutoa hati za kusafiria (passport) bila uhakiki wa raia sio maajabu? Au unataka kutuambia hakuna mtu asiye raia wa Tanzania mwenyekuweza kumiliki kitambulisho cha NIDA?

Aliyetoa mada hii ana akili kubwa kuliko zako.
 
Akili hizi ni chache siku hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona katumia hisia kuliko uhalisia.
 
Nchi zingine ukiweza kumiliki passport unaitumia kama kitambulisho lakini kwa Tanzania eti kitambulisho cha Taifa ni bora hata kuliko leseni ambayo ina Tin number ndani yake, tena Leseni ni kitambulisho bora zaidi ya hicho cha Taifa lakini haitumiki sasa kusajili line, kwa sasa kitambulisho cha kupigia kura, passport, leseni ni kama vitambulisho feki havithaminiwi tena, kwani haviwezi kusajili line nchini Tanzania ni Aibu kubwa wakati Nchi zingine wanavitumia na kama vitambulisho sahihi lakini kwa Tanzania kitambulisho cha kura kinadharauliwa wakati ndicho kilitumika kuwaingiza ccm ikulu. Wapiga kura wote walitumia hivyo vitambulisho kupigia kura na kama ni feki ina maana uchaguzi urudiwe upya kwani wapiga kura ni feki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…