Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pointa wa mitumba ni kesi pana sana. Katika mada hii nitazungunzia experience yangu ilala, kipindi nauza mitumba ilala pointa ni mteja mkubwa sana kwa sisi wafungua belo. Pointa hanunui nguo sehemu moja lakinj pia pointa hawq wako wa aina mbiliPOINTA
mnunuzi wa nguo nzuri katika duka la jumla ili akauze rejareja. Hawa wanaitwa pointa sababu wana sifa ya kuchagua kupita maelezo. Ni jina common sana kwa wauza mitumba hasa ilala boma na karume, sijajua masoko mengine wanajulikana vipi.
Pointa kama mfanyabiashara anatokea kama mteja kwa mtu anaefungua belo la mtumba. Pointa huchagua nguo kali kwa muuza mitumba, na kawaida ya pointa huchagua icon au huwa na identity yani anatengeneza wateja wake wa nguo za aina flani. Kama una uzoefu na vijana wanaouza nguo barabrani kwa kusimama au nje ya jengo la China plaza kuna vijana wengi sana pale wamepiga pasi nguo zao wanauza. Hii kazi hata Kontawa alishafanya na nikiri nilishawahi kumuona kipindi anajitafuta
Winga akiwa mzoefu anakuwa na askari wake kadhaa kituo karibu na anakofanyia kazi, likely ndio utaenda kumshitaki hapo. Kwahiyo ukifika na kesi nae utasikia "aah kumbe huyu".Hii Kazi sio rahisi
Hasara ongezea Winga wengi wanaogopa Askari wakikujua Wewe ni Askari wanaishi na Wewe kwa mashaka sana maana muda wowote kinanuka
Watu wanahudumia familia kwa kazi hiyo mkuu, vijana kariakoo wanapata hela sana kwa hizi ila wengi wanakuaga na tamaa na kuingiza utapeli humohumo.Uwinga kazi kama zilivo kazi nyengine
Mawinga wanalipa kodi?Na Mwalim M. A, Mkombozi (Kalaga baho)
Kanusho : Hakuna mgogoro wowote wa kimaslahi utakaojiyokeza kwenye darasa hili endelevu. Ushauri utatolewa bure kabisa na hakuna nia ya moja kwa moja ya kuumiza hisia ya mtu.
Asee niaje? Wazee mpo??
Ni vyema kwa kias chake kuendelea kumwaga nondo na kushea uzoefu katika mapambano kwa vijana wenzetu. Kuendelea kupeana maujanja na michongo ili tuendeshe gurudum la maisha. Ni katika harakati tu za kujikwamua na kujitegemea, juhudi za kuusaka utajiri badobado!.. Ofkoooz ni jambo linalotia moyo, na kupendeza sana!
Leo, kalaga baho ninazungumzia machache sana, japo mengi kwa kadiri ya uchache utakaofikirika. Yote yatahusu kona mbili tu yani 1. "Uwinga kariakoo", 2. "Pointa Ilala boma" na yote mawili yatabeba dhima ya kumsaidia kijana walau kuanza kuthubutu kufanya jambo.
Niliwahi kuzungumzia kuhusu mitumba- uzoefu wa ilala boma 2018-2021, na nina uzoefu wa uwinga kariakoo. Vyote kwa pamoja nitashea humuhumu.
1. WINGA
Winga ni mtu kati, dalali anayeuza kitu cha mwingine kwa bei juu ili apate chochote "ganji". Winga huwepo masoko yote makubwa yanayouza nguo, simu au bidhaa ambazo si chakula kilichopikwa. Hata chakula katika mfumo wa nafaka winga huwepo. Madalali hawa wanakabidhiwa mizigo wauze ili wapeleke hesabu.. wengine hupeleka wateja na kupewa ganji na muuza duka. Ni wazuri sana kwa wauzaji mana wachangamfu na wanauza kweli, wabaya kwa mteja mana huwa na bei juu sana. Huwa na sifa ya kubambikia wateja vitu vibovu. Mawinga ni wengi sna Kariakoo, Ilala, Manzese, Tandika,Mbagala na karume. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia mawinga wanatumia mitandao ya kufanya biashara zao. Wanaunda magroup wasap na kubust matangazo Instagram. Uwinga ni pesa, kazi na fursa kama zilivyo nyingine.
Shida ya mawinga
1. Ulevi na anasa, wengi huwa hawaon cha maana cha kufanyia pesa wanayopata. Ilala yote ile mawinga ni walevi walevi na vijana wasioleweka tu.
2. Dhulma na ujanja ujanja
Hakuna watu ambao hawafai kuaminiwa kama hawa jamaa. Mkiuza kitu mgawane hapohapo mana ukitoa kisogo umekwisha. Pia wajanja sana, huwez kutoa gepu hata kidogo mana waharibifu
3. Winga wanauza kila kitu kwa bei juu.
4. Ugumu ulipotiliza kukua kibiashara kama mfanyabiashara. Yani winga wote wanasafa kukuza biashara zao mana hawana uwezo wa kupeleka wateja dukan.. wanapoteza wateja kila leo kwa sabab ya kufika dukani tu
Uzuri wake
1. Exposure ya biashara, kujua bei na machimbo
2. Haihitaji mtaji, hupati hasara wala hulipi kodi.
3. Networking na kukua kiujuzi
Winga ana biashara gan mpka alipe kodi mkuu?Mawinga wanalipa kodi?
Belo la mtumba ni bei gani jumla na linakuwa na pieces ngapiDoKEZO
Kama utadhamin belo kwq mwanamke au mwanaume grade one jinzi bei ni elfu 8 kila moja. Kali hata 25 unauza, na skin jinz huwaga elfu 6. Kuna wengine Wanafungua belo grade 2 hawq jinz zao bei rahis sana ni kati ya elfu 3 hadi 5. Tisheti grade 1 ni elfu 5 zile kali kabis ambazo huuzwa na vijana China plaza. Nyingine elfu 3. Na uzuri wa pointa huwa na memory nzur mnoo kila nguo anakumbuka amenunua kias gan
Blauzi bei yake nj elfu tatu (shifoni), shati ni elfu 8 grade 1, grade 2 ni elf 4 mpak 5, bukta kali za ndani ni elf 4 mpaka 5, taulo elf 5 shuka ni katibya elf 9 mpaka 14 japo kunatokeaga King size zinauzwga mpaka 40+
Baadhi yao huitembeza nguo mtaa kwa mtaa, wengine hupiga pasi na kuweka dukani "GOLINI", wengjne huamua kuuza mtandaoni.. nk kama kuja njia nzuri ya wewe kufanya njia moja wapo ni vizuri. Wanaopata pesa nyingi ni wale wanaosimama kando ya barabara kubwa jioni kuwauzia watu wanaorudi makazin. Hawa kila stendi kubwa Daresalam hii utawqkuta huanza saa 9 i
jioni hadi sita usiku ,kasoro makumbusho sijawahi kuwaona (especialy hawa wa nguo).
Mnama, Mtu anatakiwa awe na biashara gani Mpaka alipe kodi?Winga ana biashara gan mpka alipe kodi mkuu?
Nenda kitumbini pale opposite na LAtra, utapata beli grade A na bei zake, zinaanzia laki 6 mpaka milioni kutegemea na nchi. Wakorea viatu vyao vidogo havina soko, ukipata beli la mkanada ama marekanni vitu vyao ni quality sana.Belo la mtumba ni bei gani jumla na linakuwa na pieces ngapi
Biashara rasmi lazima ilipe kodi, nadhani inafaham mchkato wa urasimishaji wa biashara. Eneo maalum, kusaijiliwa and so .. yani formalisation process. Winga anatokea kama kijana mdogo kibiashara chini ya machinga.. kama machinga ambae ana nafuu ya winga halipi kodi vipi winga?Mnama, Mtu anatakiwa awe na biashara gani Mpaka alipe kodi?
Yesss..... na katika pieces ungespecify belo za nguo gani au bidhaa ganiNenda kitumbini pale opposite na LAtra, utapata beli grade A na bei zake, zinaanzia laki 6 mpaka milioni kutegemea na nchi. Wakorea viatu vyao vidogo havina soko, ukipata beli la mkanada ama marekanni vitu vyao ni quality sana.
Biashara rasmi lazima ilipe kodi, nadhani inafaham mchkato wa urasimishaji wa biashara. Eneo maalum, kusaijiliwa and so .. yani formalisation process. Winga anatokea kama kijana mdogo kibiashara chini ya machinga.. kama machinga ambae ana nafuu ya winga halipi kodi vipi winga?
Kuna shughuli yoyote ya informal sector inayotakiwa kulipa kodi?
Wale jamaa wanaoenda na wafanyabiashara wa bongo china na kwenda kuwa wazungumzaji. Aisee ule mchongo kwa kijana ambaye bado mdogo kiasi asome kichina tu uwinga nje njeWa Alibaba sio?
Informal sector mkuu ni exceptional cases automatically. Au unajua rationality ya kuwqkimbiza wamachinga kipind tofauti na kile vha temporal law recognition cha magufuli mpaka wakaachwa?Acha utodoo[upuuzi].
Income Tax Act, 2005 , kifungu cha 4 kinasema "kila pato" yaani every income is subject to tax, sasa wewe unataka kubishana na sheria ya Nchi?
Winga ni kama dalali, ana hela nyingi kuliko machinga.
Simu ya 200,000/- dukani winga anaiposti anasema 250,000/- .
anaichukua anapata 50,000/- faida na kumpatia mwenye duka 200,000/-.
Mwenye duka akitoa kodi, pango, mishara , usafiri na service charg anapata faida ya 30,000/-[Mawinga walipe kodi]
hivi pamoja na uwepo wa AI bado kuna watu wanafanya kazi ya translation???Wale jamaa wanaoenda na wafanyabiashara wa bongo china na kwenda kuwa wazungumzaji. Aisee ule mchongo kwa kijana ambaye bado mdogo kiasi asome kichina tu uwinga nje nje
Naomba Exceptional ya section 4 ya ITA, 2004? short of which ni bla bla, lets talk law.Informal sector mkuu ni exceptional cases automatically. Au unajua rationality ya kuwqkimbiza wamachinga kipind tofauti na kile vha temporal law recognition cha magufuli mpaka wakaachwa?
Unajua kwa nn walipewa kitambulisho kwa kukilipia? Unajua kwa nn informal sector except urban farming mjini kinapelekewa moto na mamlaka kila leo? Mana hii unaisema ni sheria ambayo inataliwq itekelezwe na kila mhusika lakin formalisation lazima usajili biashara brela ili ulipe kodi kihalali. Je winga aksajili biashara gan?