Namna ya shambulizi la Israel huko Isfahan-Iran inathibitisha Israel wamedhamiria na wanawaalika Iran kwa vita kamili.

Namna ya shambulizi la Israel huko Isfahan-Iran inathibitisha Israel wamedhamiria na wanawaalika Iran kwa vita kamili.

Mkuu waisrael, wamarekani, waingereza, wafaransa, wajerumani na dunia kwa ujumla hawatokuja kusahau hicho kipigo kilichosababisha Netanyahu na wahuni wenzake walale chini ya mahandaki, ili kukwepa shambulio lililoshindwa kuzuiliwa na nchi zaidi ya 8.
1. Marekani
2. Uingereza
3. Ufaransa
4. Ujerumani
5. Jordan
6. Iraq
7. Saudi Arabia
8. Israel yenyewe

Pamoja na nchi hizo kujaribu kuzuia makombora ya Iran, lakini wameshindwa. Sasa Iran hako kashambulio kakazuia yeye mwenyew bila msaada wa Marekani, Saudia wala ushuzi wa nchi yoyote. Kwa kujiamini na kuidharau Israel na washirika wake Iran kasimama yeye kama yeye. Yani ni mapambano ya nchi 8 dhidi ya nchi 1. Alaf kashambulio kao ndio kepesi namna ile, na watu wengi duniani hawajui hata kilichoendelea huko Iran. Ila shambulizi la Iran mpaka vijijini kwenu huko Chato walilifahamu kulaleki 😂😂😂
{}
 
Mwanajeshi wa jeshi bora duniani akidhibitiwa na kijana ambae hana kifaru, ndege ya kijeshi wala meli ya ya kivita.

Msaada wote wanaopewa na mabwana zao Marekani na Uingereza unashindwa kuwasaidia kupambana na vijana wasiokuwa na silaha 😂😂😂
images.png
 
Kuna kambi za jeshi la Marekani zinazojifanya zinapambana na kundi la Islamic State huko Syria. Zilijaribu kutoa ushirikiano wa kudhibiti makombora ya Iran yenye nguvu lakini wakashindwa.
{}
 
Yani kila anacho ongea America ni kweli? Kama ni kweli yule kondoo Netanyahu si angeanza kujisifia kwenye press conference na kuitishia Iran na show off zake za kubweka bweka.
images (19) (1).jpeg
 
Kila mtu wakiwemo viongozi wa Israel yenyewe wameona aibu kulizungumzia hili shambulio kutokana na kushindwa kufikia malengo.

Shambulio lililozuiliwa kiulani na Iran yenyewe bila madhara yoyote, unaweza kumfananishaje na lile lililoshindwa kuzuiwa na nchi zaidi ya 8 na likapiga target iliyokusudiwa!

Shambulio la Iran liliishtua na kushangaa dunia jinsi lilivyofanikiwa kupenya ngome za ulinzi za mataifa kama US, UK, France, Germany, Saudi Arabia, Jordan, Iraq, Syria na Israel yenyewe. Hili la Israel watu wengi duniani hawajui kama limetokea maana halikuleta madhara. Lakini pia limeivua nguo Israel kwa shambulio lake kuzuiwa na nchi moja tu (Iran) bila msaada wa US wala UK.
Malengo ya Israel katika hili shambilio lao ni yepi?
 
Acheni kujifariji hakuna shambulizi lolote lililo fanyika ndani ya Iran zaidi ya vidrone vilivyo tunguliwa mjini Isfahan.
asijaribu kujibu shambulizi kubwa, mzigo mkubwa utashushwa tehran mpaka iran iombe amani
 
Cool down.
inaonekana uko na stress sana. kila mtu ana stress zake sasa hizi zako naona unataka kuhamishia kwa watu wengine.

stress ni sehemu ya maisha, na kuichukulia positively inaweza kusaidia kutoboa.

usikate tamaa kirahisi.

cool down
images (1) (16).jpeg
 
Kama vidume pigeni tuone, Iran kapiga kambi mbili na kuua wamajeshi kadhaa wamefariki..Tarifa ya wali mliadai mmezui makombora 99% sasa mnasema 84%.

Dhumuni lenu👉 Wale wanaowaita taifa la Mungu wasikate tamaa ila deep inside hamna huo uwezo , syria na Gaza kote wamekubali ila Iran mnapitisha drones za kufukuza nzinge sio mashamba ya mahindi hao.
We ni mpumbavu watu wanapigwa vizuri tu saa hii huko
 
  • Kicheko
Reactions: 511
Tukio la Jana la Israel kushambulia kwa ndege nchini Iran kujibu shambulizi la drones la Iran lililotangulia ni la kiwango cha juu kuashiria vita kamili . Hili Shambulizi lilipangwa kwa mkakati kama vile jeshi lililoko vitani serious na sio kama michezo ya kidali poo anayojaribu kufanya Iran. Hili ni shambulizi la mkakati mpana ukilitizama kwa sababu

Moja, Kuna chenga ya kijeshi waliofanyiwa Iran, ''military deception''(MILDEC) na serikali ya Israel. Chenga ya kijeshi ni kitendo cha kumuaminisha kiuongo adui kwamba utafanya au hautafanya jambo fulani ili kumchanganya afanye namna itakavyokuwa na faida kwako, ni kama kumpoteza maboya. Baada ya shambulio la Iran serikali ya Israel ilikaa vikao vingi na taarifa za mwisho za vikao hivyo zilizotoka ziliashiria Israel hawatafanya shambulizi lolote ndani ya Iran hivi karibuni lakini muda mfupi tu wameshambulia. Hii ni tofauti na vile Iran ilivyofanya shambulizi la kupanga la droni na kulitekeleza kwa siku nzima ikiwapa Israel na washirika wake muda mrefu wa kutosha kujipanga kukabiliana nalo.

Mbili, wamepiga karibia katikati kabisa ya Iran na zaidi wamepiga eneo muhuimu na la kimkakatil la Iran kijeshi na kiulinzi. Isfahan ni eneo ambalo kuna miradi ya nuclear, kambi kubwa ya jeshi na viwanda vya uzalishaji silaha zikiwemo droni. Hili ni onyo kwa Iran kwamba wamedhamiria vita na wanaweza kufika na kupiga popote katika nchi hiyo yenye ukubwa wa eneo mara mbili ya Tanzania.

Tatu, Israel wamepiga nchi tatu kwa wakati mmoja kwa mkupuo. Katika siku moja wameshambulia Syria, Iraq na Iran kuwaonyesha wa-Iran kwamba wako tayari kwa lolote.
Sasa tutegemee majibu kutoka kwa Iran.

Nne, Israel imeonyesha kwamba inaweza kufanya maamuzi yake peke yake kama nchi huru bila kujali washirika wake wa Marekani na Ulaya linapokuja suala la ulinzi, vita na pride ya nchi yao. Pamoja na msimamo wa Marekani na Uingereza wa kwamba hawataiunga Israel katika mashambulizi ya Iran kwa sasa, Israel imeendelea mbele na kufanya mashambulizi yenyewe kama ilivyopanga na kuona inafaa bila kujali msimamo wa washirika wake.
Hauwezi kuitokomeza Hamas na Houth Iran ikiendelea kubaki na nguvu.

Sasa hawa Mazayuni wanataka wakate mzizi kwanza.

Hakuna namna likiibuka la Istael na Iran lazima Marekani na uingereza waingie wazimawazima. Na ndicho kinatafutwa.
 
Vyombo vya habari vya Iran vimesema vimeona milipuko mikubwa kwenye kambi za jeshi .Live.Lakini serikali ya Iran inasema hiyo milipuko ni kweli ilikuwepo ila ilikuwa milipuko ya mitambo ya Iran ya kurusha makombora ya kulipua hivyo vidrones vya Israel ha ha ha ha 😂

Vidrones vinajibiwa kwa milipuko mikubwa ardhini kwenye ardhi ya vituo vya jeshi la Iran😄 🤣 😂 😆 😄 🤣

Message sent
Endelea kujifariji.
 
Back
Top Bottom