"Watanzania"
Zari ajirekebishe kujumuisha watanzania wote, kwasababu wanaomsema na kujibizana mtandaoni sio wawakilishi wa watanzania isipokuwa nafsi zao binafsi.
Na, anapowasema watoto wa watanzania kwa kuwafananisha na wa kwake, nadhani hayuko sahihi.
Naamini, kama watoto wake walisemwa vibaya pasipo wao (watoto) kuyasikia maneno hayo yenye ubaya, si busara kwake kuja kuwasema watoto wa watanzania wote...azingatie kuwa mashabiki wake wengi na wateja wa bidhaa anazotangaza hasa dippers za watoto walengwa ni watanzania na watoto wa Tanzania.
Ashauriwe, awe na "vituo" vya maneno na kifua cha kuyamudu maudhi ya mtandaoni. Kabla ya kujitokeza, atazame "jina" na umaarufu wake...kwa sababu hasara ya maneno yake anaweza asiione moja kwa moja, au kwa haraka.