Namtetea mtoto wa Simbachawene, askari wachunguzwe

Hao askari wanatakiwa washtakiwe kwa kumpiga picha bila idhini yake.
Mbona wakiwa wanapokea rushwa hawajipigi picha.
Sasa wamenipa warrant wa kuwapiga picha pindi nikiwapa buku mbili halafu narusha mtandaoni
Mimi nataka kudeal na police wanaokunywa pombe wakiwa kwenye unifomu na smg siku nikibahatika video nitaitupa hewani waone km ni mazuri
 
Hiyo ndio hoja ya msingi.
Wakienda mahakamani hakuna uthibitisho kuwa alikuwa amelewa maana , hakuchukuliwa vipimo.

Tumekumbwa na pepo baya la kuchukia wateuliwa na Familia zao, pasipo sababu ya msingi.
Na kuhisi kuwa wao ndio waliotusababishia umaskini.
 
Hii mada yako na ile ya wakili msomi Pascal Mayalla zimedhihirisha namna gani makosa ya Tort ni mageni kabisa Tanzania.

Kikubwa kinachoangaliwa kwenye makosa haya ni :-
1.Duty of care
2. Breach of that duty
3.Demage
Sasa huyu ndugu Simbachawene ambaye naye ni msomi wa sheria kutoka chuo kikuu huria kama ilivyo kwa wakili msomi Pascal Mayalla , je! ana duty of care kisheria kwa lijitu lizima ambalo limezidi miaka 18 na lina familia yake? Nadhani Simbachaweze ameamua kutokahadharani na kulaani kitendo hicho lajitu ka,a raia mwingine aliyekerwa na kitendo hicho cha kumdhoofisha afisaa akiwa anafanya kazi yake na tutambue kuwa bado simbachawene ni mwanafamilia wa taasisi hiyo kwani aliwahi kuwa waziri wake , hivyo kuna yale mahusiano ya kufaamiana kwaz kufanya kazi pamoja.

Kwangu mimi, kwa njia yoyote ile hutuwezi kumuunganisha Simbachawene kwenye ujinga alioufanya mtu huyu na sijawahi kusikia tort ya aina hiyo.

Tort kama ilivyo kwenye makosa ya jinai huwezi kuhukumiwa kwa kosa ambalo halipio kisheria (Nulla poena sine lege ), Kadhalika baba wa Jurisprudence duniani Salmond alifafanua vilevile kuwa Tort nayo ina makosa yake, hivyo sio kila kitu utakifananisha na tort na kukipeleka mahakamani. Hapa alitolea ufafanuzi na kulinganisha na matundu ya nyumba ya njiwa kuwa ili njiwa aingie kwenye tundu lake lazima hilo tundu liwe na ukubwa ambao njiwa anaweza kukaa ( PEGION HOLE PRINCIPLE)

According to Salmond, “Tort is a civil wrong for which the remedy is a common-law action for unliquidated damages, and which is not exclusively the breach of contract, or, the breach of trust, or, other merely equitable obligation.”
Hivyo kwa maoni yangum wanaharakati wanaoliongelea hili, wanaongea kufurahisha jukwaa tuu au kwa sababu kuna mtu mkubwa katajwa lakini ilkienda mahakamani kama Simbachaweze atakuwa jointed inapigwa P.O asubuhi na mapema, lakini Polisi wana nafasi kubwa ya kumshitaki huyo kijana aliyefanya kosa hilo ( in his individual capacity) kwa makosa ya jinai cum usalama barabarani na Tort ikiwezekana ijapokuwa kupata UNLIQUDATED DEMAGES kwa askari kwa makosa ya tort yanayotokea kutokana na majukumu yake ni ngumu sana na hii nilisoma kesi nyingi za kizungu za askari waliopata madhara ya Post-traumatic stress disorder (PTSD) pale ambapo wanaposhukulikia matukio ya kutisha kama ajali, mauji nk na kuishia kupata mishtuko inayowaletea madhara ya kiakili na kimwili, kuna debate kubwa sana kwenye sheria kuhusu injury wanazozipata watu lakini hazionekani kwa macho na ni mbaya zaidi kuliko pysical injuries

Avogadro. LLB hons OUT
 
Tulia. Baba yako akileta nyoko nyoko ata hamishwa babarani, apelekwe kuwa Askari magereza, huko Mpanda.
 
Inafedhehesha Sana mshua akiitwa hivyo mbele ya watu au mtu wa karibu wa bi mkubwa akitukanwa na mtoto mbele ya watu.
Huyo Askari angekua mhehe au mchaga Sasa hivi mawaziri wangekua wanapishana Muhimbili.
Labda useme Mhehe, ila si Mchagga.
 
Dah umenikumbushs ya Mtwara na yule askari mwenzao waliyemnyonga. Halafu eti leo wawe wadilifu
 
Sema watanzania wanatakiwa kupewa heshima na hao poliCCM sio kusema watoto wa viongozi?
Kwani hao watoto wa viongozi ni akina nani?
Acha uchawa wa kingese!!
 
Wamemrekodi clip nyingi nyingi tu kuanzia nje hadi ndani ya kituo, na wao wana makosa. Aligoma kuingia kituoni ikabidi wamfosi wakawa wanamsukuma ndio maana akawa anatukana pale ndani ya kituo na yeye anataka kulipwa kwa kudhalilishwa
Kwanin akatae amri halali au kibao cha tii sheria bila shuri hakukiona?
 
Kwahiyo ukisababisha ajari, wenye mali mkiamua kulipana ndiyo basi, askari wa usalama barabarani, hawana chao tena siyo, kwa mujibu wa sheria zetu?
 
Hebu kakae na babaako nyumbani muyaongee kifamilia, sio Kuja humu JF.
 
Labda mama awe aliishaondoka duniani, vinginevyo huyo huyo waziri ataenda kufuta kesi.

Ngoja tuone nguvu ya mbunyee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…