Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Mimi Makonda ni mdogo wangu kiumri na hata kiutumishi. Nilikuwepo wakati akihudumu kama mkuu wa mkoa wa Dar. Ni kijana shupavu asiyeyumba katika jambo analoliamini.
Makonda alisaidia sana Jiji la Dar kuwa salama alikimbizana Sana na wauza madawa pamoja na waliotelekeza watoto. Alilimudu Jiji kwelikweli alikuwa mbabe na wakati mwingine mnyenyekevu.
Hotuba zake zilikuwa za kiume kweli kweli mamlaka yake ilimfanya avuke mipaka na kuwa mtu wa amri na visasi Makonda akiamua kumsakama mtu alikuwa haangalii cheo chake au umaarufu wake wengi walikimbia Dar na kufunga biashara zao
Kwa sababu ya kumuogopa Makonda, maduka, mahoteli, yalifungwa Kwa kumkimbia Makonda, labda alijua atakuwa mkuu wa mkoa milele inasemekana hata viongozi wa juu yake hakuwa akiwapa heshima yao Kwa sababu tu alikuwa na mawasiliano ya Moja Kwa Moja na JPM.
Hicho ndio kinamgharimu Leo, walioshika madaraka ni wale alikuwa akiwadharau sana wakati ule wa mwendazake pamoja na yote Mimi naamini tayari amejifunza na tusimuache apotelee kusikojulikana umri wa Makonda bado ni mdogo Sana , mamlaka imsamehe na impe nafasi nyingine. Mimi na mwamini na nimemiss sana heka heka za Paulo, mamlaka imesamehe huyu mwamba asimame Tena awatumikie watanzania na abadilike
Mimi mganguzi namwombea msamaha Paulo Makonda, natamani kumuona Tena katika uongozi na majukumu ya kitaifa, bado ni mtoto na ni kijana, huenda Kuna makosa aliyafanya Kwa sababu ya mihemuko ya ujana.
Naamini amekuwa naiomba mamlaka imkumbuke bado ni mbegu changa tusimzike ila tumfufue na kumfunda Ili aendelee kuitumikia nchi yetu. Narudia Tena namwombea msamaha Paulo Makonda Kwa yote yaliyopelekea apotelee kusikojulikana
Mimi mganguzi kazi yangu ni kuganga Kila jeraha