Namwombea msamaha Paul Makonda, ni damu changa iliyozikwa mapema

Mimi ninavyojua ni kuwa alikwenda kujaribu bahati yake Kigamboni kikaumana...sasa msamaha unaombwa kwa nani?. kwani angefanikiwa saa hii si angekuwa Mbunge.
 
Huyo anatakiwa akamatwe
Kwa kufoji chetu
Haiwezekani wengine wafukuzwe yeye abaki na wewe ndiye mwenyewe
 
Atoke hadharani yeye si ana mdomo yule na sio bubu,aseme alishiriki kukatisha uhai wa watu wangapi na nani alimtuma ndio mengine yatafuata.
 
Hili taifa halitegemei mtu mmoja au watu kumi, lina watu wengi wa kufanya kazi. Huyo
mtu wako mwambie akalime bustani.
 
Wapo wengi sana wanaofaa kuliko yeye.
 
Hii mbegu ilioza haikumea! Ilizongwa zongwa na malimwengu ya umaarufu ikakosea na kuharibu udongo ambao ulitakiwa irutibishwe nao. Kupitia mbolea ya kemikali iliyomwagwa na dude moja jina lake kwa kifupi JPM mbegu Hii ilibadilika na kuwa sumu kwenye udongo ule uliotakiwa kuwa nyumba yake. Mbegu hii iliendelea kuumiza viumbe hai walioishi udongoni kama Ben Saa nane (hiki kiumbe kiliuawa kabisa), Tundu lissu (Huyu alijeruhiwa kabisa). Mbegu hii;Makonda ina sumu kali inabidi iondolewa udongoni haraka ili kuacha mazao yaote vizuri. Makonda anatakiwa KUNYONGWA. Tunahitaji kuzitambua hizi sumu zinazoitwa mbegu!
 
Nenda ukawaombe msamaha wale ambao ndugu zao walinyimwa haki ya kuishi.

Makonda aliwanyima baadhi ya watu haki ya kuishi (USA government statement). Ni kauli ambayo haikuwahi kupingwa na mamlaka yoyote ya Tanzania.
 
Mpe kazi kwenye Company Yako ya kuuza nsenene Europe. Naamini kwa sifa hizo ulizo mpamba Nazo kwa kusaidiwa na michwezi wa John Joseph, atakusaidia kukuza mauzo ya biashara Yako.
 
Gwajiboi alitoa muongozo mbona siku ile ana mfuta DAB kwenye ulimwengu wa siasa alimuamuru aombe msamaha kisha ajiuzuru baada ya hapo arudi shule akatafute vyeti vyake kisha arudi atakua katakasika hakuna short cut
 
Mimi sio chawa ila natamani kumuona Tena katika majukumu ya kulitumikia taifa
Taifa gani labda aende huko kwenu Burundi, Watanzania Bwana, hivi hamzionei Huruma Roho za marehemu zilizopotea na madhira ambayo wananchi wameyapitia kutokana watu hawa?. tunahitaji kujenga Tanzania ya watu waliostarabika. yanayotokea kwenye uchaguzi wa Kenya yatufunze na kutuondoa kwenye hizi fikira duni tulizonazo. na hili siyo kwake tu bali hata viongozi wengine linawahusu, na kuwa unaweza kuwa kiongozi bora bila kufanya Dhulma kama viongozi wetu wengi wanavyofikiria au kujificha kwenye kivuli cha Uzalendo.
 
Katika hii dunia usijaribu kuwadhalilisha watu wenye umri mkubwa wanaoitwa wazee !! Fanya yote lakini usijaribu kuwadhalilisha wazee eti kwa sababu tu wewe unao uwezo wa kufanya hivyo !! Ukifanya ujue you gonna pay very big price !!
 
Ukiona threads kama hizi ujue soon kuna teuzi zitatolewa..stay tune watu wa kitengo huwa na namna nyingi za kutoa info.

#MaendeleoHayanaChama
Let them do what suits them lakini ukweli utabaki kuwa ukweli tu !! Kama alikuwa muovu atalipwa tu kwa maovu aliyoyatenda !
 
Mpaka umeamua kumwombea Msamaha hebu YASEME Matendo yote MABAYA aliyoyatenda MAKONDA yakiwemo ya Utekaji Uuaji Ubambikiaji Kesi Uboraji Fedha za Wahindi
Kujimilikisha Viwanja vya Wahindi Kunyang'Anya Magari mazuri ya Wafanyabiashara
Kudhalilisha Watu akiwemo Mzee Lowassa kuwataja kwa Uongo wauza Madawa Kumpiga Makofi Mzee Warioba n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…