Namwombea msamaha Paul Makonda, ni damu changa iliyozikwa mapema

Mimi sio chawa ila natamani kumuona Tena katika majukumu ya kulitumikia taifa
Yeye pekee nchi hii ndo mwenye uwezo wa kulitumikia taifa?

Kama ni ujana ndiyo uliokuwa unamsumbua mbona kuna vijana wadogo zaidi yale tena walipewa majukumu makubwa ya uwaziri na hawakufanya alichokifanya.
 

Kafufue hawa halafu uje! Angalia vizuri hapo Albert Bashite unamuona?
 
unaomba msamaha kwa ajili ya ben saa8 au risasi kwa tundulisu au kwa ajili ya kipi?
kati ya wajinga wasiostahili kuwepo kwenye utumishi wa umma bashite ni mmoja wapo. nafikiri hata maza ameliona hilo na siku akimrudisha ndio atajua kama ni liability kwake. kwasababu majority hawataki kusikia hicho kitu. sauti ya wengi iheshimiwe.
 
Sema ni "Madam" mmoja anamlinda huyu mwendawazimu alitakiwa kuwa eneo chafu sana kutokana na mambo machafu sana aliyoyafanya tena jambazi sabaya angeonekana ana nafuu! Ila siku zaja atakuwa ktk mikono ya watesi wake!
 
Hali ya usalama kwa Dar sio nzuri na raia wanaishi kwa mashaka mithili ya raia wa Ukraine waliopo kwenye vita vikali.

Makonda yupo serious na maisha ya wananchi wake ndio maana alipambana kukaboliana uhalifu wa kila namna.

Sasa ni wakati muafaka kumshawishi mama yetu Rais Samia amrejeshe Jembe mchapakazi Paul Makonda.
 
Watu wengine sijui wana akili gani, yaani mtu alishalaaniwa kwa kuwa kinara wa genge la mauaji la wasiojulikana na kuna watu amewaua na wengine amejeruhi wewe bado unamsifia tu muuaji kama huyo, hadi Marekani wamempiga marufuku kukanyaga ardhi yao..!!

Wewe ni mtu moja wa hovyo na mpumbavu wa kutupwa. Bure kabisa.
 
BullSh...
T!
 
Kwanini usianzie Kilimanjaro ukaandamana bwana General akafutiwa kesi na kuteuliwa ukuu wa wiraya Hai?[emoji848]
 
Buda huwa unahangaika sana na konda boy
 
Kiukweli Mama ni msikivu mno. Wananchi walimlilia Kamanda Muliro akamleta. Sasa hivi tukimlilia Makonda atamleta tu! Mama tunamuomba Makonda arudi kuwa RC wa Dar es Salaam! Sikia kilio chetu Mama!!
 
Kama lipo la kumkumbusha Samia, ni kuagiza serikali imfungulie makonda mashtaka ya jinai uhujumu uchumi nk, sawa na Sabaya.

Seikali imekuwa na kigugumizi katika hili hadi watu tunahisi mengine yasiyofaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…