Nani alianzisha jina la "Daddy" kwa Viongozi wa Kiroho?

Nani alianzisha jina la "Daddy" kwa Viongozi wa Kiroho?

Naona imekuwa trend siku hizi kwa Nabii, Mtume, Mchungaji haswa hawa kwenye makanisa binafsi ya kiroho kuitwaa Daddy!

Dadii una mgeni...
Dadii tukuletee chai...
Dadii Mzee Fulani amekuja tayari...

Masanja anaitwa daddy
Myamba anaitwa daddy
Mwamposa anaitwa daddy
Malisa anaitwa daddy
Yule wa kivule aliewaagiza nywele za sehemu za siri na kuchat dadi akafungiwa na serikali anaitwa Daddy

Who else anaitwa Daddy?

Wadada ndio wanaongoza kuwaita hivi, wengine wake/wachumba za watu. Ndio Mahaba, Heshima, Upendo, Fashion au kweli ni Kiongozi wa Kiroho?

Akiwa nyumbani, "Baba Chaudele unaingia nifunge mlango😒"

Akiwa kanisani, "Karibu Daddy..pita na viatu😁" na goti linapigwa!

Siku njema!
Wala msimwite mtu yeyote ‘Baba’ hapa duniani, maana Baba yenu ni mmoja tu, aliye mbinguni. Wala msiitwe ‘Viongozi,’ maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiye Kristo. Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu. Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa.
Mathayo 23:9-12
 
Usiombe mkeo awe kwenye hayo makanisa hamna rangi utaacha ona

Kifup huyo dady atampumbusha mkeo na wewe utaitwa baba James siyo dady
 
Wala msimwite mtu yeyote ‘Baba’ hapa duniani, maana Baba yenu ni mmoja tu, aliye mbinguni. Wala msiitwe ‘Viongozi,’ maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiye Kristo. Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu. Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa.
Mathayo 23:9-12
Asante mkuu
 
Ndiyo, matumizi ya neno "Daddy" kwa baadhi ya viongozi wa makanisa ya kiroho na kipentekoste yameongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni. Mara nyingi hutumiwa na waumini kama jina la heshima linalomaanisha baba wa kiroho (spiritual father), sawa na jinsi wengine wanavyosema "Baba Askofu", "Baba Mtakatifu", au "Mzee wa Kiroho".
Kwani Kwa Kiitaliano, neno la kawaida la baba ni "padre".
Wakatoliki wanatumia neno Padre, badre ni Baba kwa kiitalano, kwa English father, kiswahili Baba.
 
Back
Top Bottom