Siasa za kweli na zenye manufaa kwa jamii na nchi zahitaji watu waliokomaa na wanaojua mahitaji ya jamii na nchi badala ya maigizo ya kukariri, kutafuta maisha na umaarufu.
Hata hivyo, tulitaka hao wanawake waliomalizia pesa zao kwenye kampeni, Magufuli amebana siasa za upinzani (mbunge mmoja tu), washindwe hata kumudu mahitaji ya kawaida katikati ya misukosuko ya kisiasa? Uamuzi wao ulikuwa wa kipekee kwao (afadhali lawama kuliko fedheha). Kwao ilikuwa mapambano ya kufa na kupona kwa maisha baada ya uchaguzi.
Halima alikuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda na alijiamini.
Tatizo kubwa kwa hao wanaume waliosaliti vyama vyao.
Ni watu wa kuwekwa kwenye kundi kama walivyo na kukaa nao kwa akili.