Una tatizo mpaka hapo huwezi ukawa unasimulia watu unalalia godoro gani ni ujinga kiwango cha lami huwezi akawa unajieleza kwa watu unamiliki vitu fulani na huna ni utoto1. Kunaepusha husda na uchawi miongoni mwa majirani na maadui wa familia. 2. Ni utamaduni tu uliojengeka tangu kale,hata wanyama mfano paka wana tabia za kuhama usiku 3. Kuepusha aibu, imagine mtaani ulikuwa unasimulia wewe huwezi kulalia godoro inchi 1 wakati unahama unahama na sandarusi iliyojazwa pamba.
Wengine eti wanaficha vifaa vyao vya uchawi.Lengo kubwa ni kuficha Siri za familia,magodoro yaliyochoka,fenicha zilizochakaa!!
Watu wanaficha vitendea kazi vyao ndio maana hawataki mvione😁😁 hii point ni nzito mno kumbe unatakiwa usikilizwe ww jukwaa ni lako mkuu hebu nipe point za kutosha kuhusu usemacho
Wajipange kujieleza wakaeleweka.😃 wanakuja utawajibu kuhusu usemalo
Hao wanaohama usiku ni wapuuzi tu kama wapuuzi wengine mkuu. Ni sawa na baadhi ya watu ukimpa mtu kitu kwa mkono wa kushoto anakuona mshirikina. Sasa kama mkono wa kushoto ni mkono wa laana kwanini Mungu aliamua kuitenganisha? Si angeweka tu mikono yote miwili mkono wa kulia?Habari wakuu,
Kuna jambo nimekuwa nikiliona mara kwa mara kwenye jamii yetu. Watu wengi huamini kwamba kuhama nyumba ni jambo linalopaswa kufanyika usiku, kiasi kwamba mtu akihama mchana huonekana kama amefanya kitu kisicho cha kawaida.
Binafsi najiuliza, hii dhana ilianzia wapi? Je, kuna sababu za msingi zinazofanya watu wahame usiku zaidi kuliko mchana, au ni mazoea tu yaliyojengeka kwenye jamii?
Kwa mtazamo wangu, kuhama ni kuhama tu, iwe mchana au usiku. Kila muda una faida na changamoto zake. Lakini bado wengi wanaonekana kuhusisha kuhama usiku na usiri, uchumi wa gharama, au hata imani fulani za kijamii.
Je, wewe unaonaje? Umewahi kuhama mchana au usiku? Unafikiri kwa nini watu wengi hupendelea kuhama usiku?
Karibuni kwa maoni na uzoefu wenu.
Sasa si waache watu wavione ili liwe fundisho kwa wengine mkuu?Watu wanaficha vitendea kazi vyao ndio maana hawataki mvione
Mkuu umewasimanga kwa uchungu mno wanakujaHao wanaohama usiku ni wapuuzi tu kama wapuuzi wengine mkuu. Ni sawa na baadhi ya watu ukimpa mtu kitu kwa mkono wa kushoto anakuona mshirikina. Sasa kama mkono wa kushoto ni mkono wa laana kwanini Mungu aliamua kuitenganisha? Si angeweka tu mikono yote miwili mkono wa kulia?
Mimi sijawahi kuhama usiku. Nahama mchana kweupe mkuu. Kuhama usiku ni uzezeta. Ni zaidi ya wauza duka mazezeta amabao hawauzi sindano au chumvi usiku. Watanzania wamejaa mawazo ya kishirikina na kilofa.
Mkiviona vinapoteza uboraSasa si waache watu wavione ili liwe fundisho kwa wengine mkuu?
Huo ndio ukweli mchungu bwasheeMakorokoro dah 😃 mkuu upunguza ukali wa kwanja lako