Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 14,705
- 30,041
You can make a point bila kuwafokea watu hapa, ikiwa kwako ni sawa kuhama mchana it's okay homeboy,lakini haimaanishi wengine ni mazezeta kwasababu tuna sababu za msingi kabisaHao wanaohama usiku ni wapuuzi tu kama wapuuzi wengine mkuu. Ni sawa na baadhi ya watu ukimpa mtu kitu kwa mkono wa kushoto anakuona mshirikina. Sasa kama mkono wa kushoto ni mkono wa laana kwanini Mungu aliamua kuitenganisha? Si angeweka tu mikono yote miwili mkono wa kulia?
Mimi sijawahi kuhama usiku. Nahama mchana kweupe mkuu. Kuhama usiku ni uzezeta. Ni zaidi ya wauza duka mazezeta amabao hawauzi sindano au chumvi usiku. Watanzania wamejaa mawazo ya kishirikina na kilofa.
Sababu gani zinawafanya mhame usiku mkuu? Ni ushirikina au ni nini?You can make a point bila kuwafokea watu hapa, ikiwa kwako ni sawa kuhama mchana it's okay homeboy,lakini haimaanishi wengine ni mazezeta kwasababu tuna sababu za msingi kabisa
Kuwa humble siku zote
Kwani ukijenga ndio huwezi kujenga nyingine? Biandamu sio kobe.Ukijenga yako itakuwaje
Nyie ndio wale mnaonekana kama mnaenda kuchota maji kumbe ndio unasepa hivyooo ๐คฃ๐คฃMie nahama mapema maana sina vitu kabisa ๐ ๐
Nenda comment no 11 utanikutaSababu gani zinawafanya mhame usiku mkuu? Ni ushirikina au ni nini?
Wale jamaa wenye magari ya kubeba vitu Canter au Fuso wanapendelea kubeba mizigo kuanzia saa 12 jioni kuwakwepa wale wavaa nguo nyeupe.Sababu gani zinawafanya mhame usiku mkuu? Ni ushirikina au ni nini?
Yaan shwaa๐คฃNyie ndio wale mnaonekana kama mnaenda kuchota maji kumbe ndio unasepa hivyooo ๐คฃ๐คฃ
๐ชUmenikumbusha mwaka fulani mimi na mshkaji wangu tulikua tumepigika ile mbaya.
Mwenye nyumba akatutimua, katika pilika pilika tukapata sehemu ya kuhamia, ila changamoto ikawa hela ya kuhamishia vitu hakuna.
Baada ya kuwaza sana, tukafikia maamuzi magumu, tukakubaliana tutahama na daladala.
Usiku mida ya saa tano, tukaanza kusomba kitu kimoja kimoja, kutoka nyumbani mpaka stendi ya daladala.
Mfano wa umbali kutoka nyumbani mpaka stendi ni sawa na kutoka ubungo darajani mpaka kanisa la kakobe mlimani city.
Mnabeba kitu mnatembea weeeee mkichoka mnashusha kupumzika, mpkaa tunamaliza mzigo wote ni saa saba usiku.
Kwa mnaopajua bunju muda mwingi pamechangamka hata kama ni usiku sana.
Daladala imekuja tukamwambia tunalipia seat 6 kwa bei ya 500@ mabishano ya hapa na pale jamaa akasema tumpe 5000 tukakubali haooooo tukahama.
Tumefika sehemu tunapoenda tukashusha mzigo, ikawa kubeba kwa zamu, unabeba unapeleka ukirudi na mie nabeba mpaka mzigo wote ukaisha.
Hii stori tukiwaambiaga watu hawaamini.
Sawa mkuu.Nenda comment no 11 utanikuta
Kwani Canter haziruhusiwi kufanya kazi mchana mkuu?Wale jamaa wenye magari ya kubeba vitu Canter au Fuso wanapendelea kubeba mizigo kuanzia saa 12 jioni kuwakwepa wale wavaa nguo nyeupe.
๐๐ Chumba cha mtu unauliza nini? tena anaonekana jamaa niboda na niyamkataba analala nayo ndan.hawezi laza kwa walinzi wasje iibaHiki ni nini ๐ ๐
Jamani dah si angepangilia vizuri sasa๐๐ Chumba cha mtu unauliza nini? tena anaonekana jamaa niboda na niyamkataba analala nayo ndan.hawezi laza kwa walinzi wasje iiba
Mda wakupangilia geto msela utatoa wap unaamka kumi usiku kupeleka abiria stend kurud kulala sasita usiku mabassi ya mikoan yakikata.na. Geto la hvyo utapanga nin kieleweke๐๐Jamani dah si angepangilia vizuri sasa
Weekend basi ebooMda wakupangilia geto msela utatoa wap unaamka kumi usiku kupeleka abiria stend kurud kulala sasita usiku mabassi ya mikoan yakikata.na. Geto la hvyo utapanga nin kieleweke๐๐
Love and respect kwa watu wa mtaaNakumbuka mwaka flani enzi hizo bwana mdogo naanza maisha nilihama mchana maana sikuwahi kuwa na hii mentality ya kwamba kuhama inatakiwa kuwa usiku... Nilikua na vitu vichache tu, sasa ile natoa vitu ndani naenda kuvipakia nje ya geti kwenye guta, majirani ( wengi wao wamama) wakawa wanashangaa na kusikitika ninavyohama " jamaa uhamia wapi? Jamani kwa nini unahama lakini?"
Ikawa majirani wengi wako nje na watoto wao wameshika mikono kiunoni wananiangalia ninavyopakia vitu kwenye guta,,, kwa hiyo majirani wako nje wananishangaa, na kumbuka hiyo nyumba ipo karibu na barabarani... Mpaka dereva wa guta ameliwasha na nimepanda hapo nyuma, nyomi la kutosha mpaka madereva wa bodaboda wakaunga tera kushangaa wamepak pikipiki zao wanaimba"we charii kumbe unahama aisee"... Aisee nilijisikia vibaya siku ile, toka hapo ndo nikajua kwa nini watu wanahama usiku.