Nani aliwachagua kuwa viongozi wa dunia? G7 ni viongozi wa nchi 7 tu si zaidi ya hapo


Mbona habari yenyewe ya kuchonga?. Hakuna wa kuwadindia G7. China aendelee na BRICS aache maneno.
 

Wamesema lini? Usiongee mambo ya kufikirika. Mikopo yote inatoka huko. Huyo Ghana anakaribia kufilisika kutokana na Deni la nje, halafu ndio aje aongee Nini?.
 
Umaskini wa akili ni umaskini mbaya sana!! Hizi nchi zinazodaiwa ni tajiri, utajiri wao ni wa wizi na utapeli tu!! Umaskini wa Afrika kwa mfano si umaskini halisi!! Ni umaskini wa akili!! Tuna raslimali nyingi sana!!

Huo ndio ukweli, Bado uduni wa akili unatausumbua Africa, ila kulaumu nchi zilizoendelea ndio uduni wenyewe wa akili. Rushwa na ufisadi umejaa utamlaumu mzungu?
 

Hata china ana BRICS kila nchi ina kundi lake, lakini G7 ndio inasidia nchi nyingi hasa mikopo na nk
 

Sio kweli, Russia Russia aliondolewa mwaka 2014 baada ya kuivamia Ukraine na kuichukua Crimea.
 

Ujifungie utaishije?. Mikopo Nani atakupa. Maana nchi nyingi za Africa zinaishi kwa madeni kutoka G7.
 

Nakataa, Africa tunajinyonya wenyewe. Ufisadi ni mkubwa kwa Viongozi ila tumebaki kuwalaumu G7.
 
Sasa kuna mataifa gani mengine yenye nguvu kushinda hayo saba nguvu za kiuchumi na ushawishi
 
Aise, mbona hawamvamii sasa Mrusi kama huu ndiyo ukweli?

Hata kama mnapata good time ya hao ndugu tusiwe obsessed kiasi hichi cha kuwaabudu...Hata sisi wengine ndiyo wanaotufadhili lakini akili zetu hatuziazimii kwao, we know what is right and wrong
 
Nakataa, Africa tunajinyonya wenyewe. Ufisadi ni mkubwa kwa Viongozi ila tumebaki kuwalaumu G7.
Hapa nakubaliana na wewe...Lakini siyo kweli, Africa na dunia ikiamua G7 inaweza kufanya lolote...Hao wanatumia psychology kuaminisha watu kwamba wao ni super beings...
 
China anaongea Nini?. Makampuni ya kimarekani ndio yamejaa china. Trump alitaka kuyaondoa ayarudishe marekani China akawa mpole. Maana hayo ndio yameifanya china ikue kiuchumi.
 
Hapa nakubaliana na wewe...Lakini siyo kweli, Africa na dunia ikiamua G7 inaweza kufanya lolote...Hao wanatumia psychology kuaminisha watu kwamba wao ni super beings...

Sawa mkuu
 
Reactions: Ame
China anaongea Nini?. Makampuni ya kimarekani ndio yamejaa china. Trump alitaka kuyaondoa ayarudishe marekani China akawa mpole. Maana hayo ndio yameifanya china ikue kiuchumi.
Lakini kumbuka why yapo China? Cost of production ipo chini sana China, hivuo kuna comparative na competitive advantages za kupeleka hayo makampuni China, na kwa ilivyo hata wakiyahamisha lazima China itayatengeneza hybrids za hizo...So wote wawili wanaogopana japo wanatishiana nyau
 
China anaongea Nini?. Makampuni ya kimarekani ndio yamejaa china. Trump alitaka kuyaondoa ayarudishe marekani China akawa mpole. Maana hayo ndio yameifanya china ikue kiuchumi.
Makampuni kurudi US hayawezi gharama za uzalishaji, bidhaa zitashindwa kupambana sokoni
 
Hata wewe pia unachekesha kwa akili yako china, urusi, india na baadhi ya nchi kama south korea nk haziwezi kuingia hapo, huo ni mpango tu wakuendelea wa kujiona wAo ndio kila kitu.
 
Nikupe mfano kidogo, kijijini kanisani (hasa katoliki) tajiri akitoa hoja hata kama ni pumba watu wanamshangilia kwa kusema "ndio Mzee" hata kama ni kijana mdogo. Basi hayo mataifa ni tajiri, wanastahili "ndio Mzee".
 
Nakataa, Africa tunajinyonya wenyewe. Ufisadi ni mkubwa kwa Viongozi ila tumebaki kuwalaumu G7.
Hii mada imetuzidi ukubwa tujadili mada level yetu,bajet yetu kila mwaka matumizi ya kawaida pesa ni nyingi kuliko maendeleo bajeti za kufikirika,ujasili wa kujadili nchi ambazo zimeishapitisha bajeti zao hadi 2030 na pesa zipo mezani tunaupata wapi? Tujadili kutupiana majini,wanganga wajadi,kipindupindu,utapiamlo nk
 
Maendeleo yao yameletwa na Hard working, kuanzia Mapinduzi ya Kilimo na vinginevyo,

Taiwan wana dominate sana Soko la Electronic, ni rahisi kusema wamesaidiwa na Marekani kwa mvivu asietaka kusoma, ila ukisoma Historia baada ya vita vya pili vya Dunia jamaa walirudi shambani, wakafanya Reform ya Sheria watu wakapewa ardhi wakalima, kutokea kilimo viwanda vikaanza, viwanda vinavyohusiana na Kilimo kama vya Nguo na baadae kidogo kidogo waka Transform kwenda Electronics. Unaweza soma historia yao hapa


Indonesia hawa wametoka kivingine, mpaka 1998 Indonesia ni Uchumi mdogo mno ila sasa hivi wapo G20, hawaja Mcopy mtu wala kumfanya yoyote awe role model wao wameangalia dunia Inataka nini wakawapa wanachotaka, Indonesia sasa hivi ni Muuzaji mkubwa wa Nickel kwa ajili ya Battery, Anauza Kote west na China atakaefika dau anauza, Anauza Mchele, Kahawa, Mafuta, Gesi, Mawese, Rubber etc. Kifupi Indonesia ametoka kwa ku Supply raw materials.

China wanapigania Masoko yoyote yale Duniani sio ya Us na Ulaya tu, Soko kubwa la China ni Nchi za Sea, ikifuatiwa na Us halafu ndio Ulaya. Pia China yeye ndio ameforce waende waka invest kwake, ni mipango yao na Akili zao sio kwamba Usa wamemsaidia China bali mipango ya china ndio imemleta Usa pale.

Kifupi mkuu hao wa Asia ni hardworker kupita maelezo na wakipata njia ya kutokea wanafanya kazi kwa bidii hadi wanatoka, hawajakuwa matajiri kwa misaada ni cheap propaganda tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…