Nani aliwachagua kuwa viongozi wa dunia? G7 ni viongozi wa nchi 7 tu si zaidi ya hapo

China anaongea Nini?. Makampuni ya kimarekani ndio yamejaa china. Trump alitaka kuyaondoa ayarudishe marekani China akawa mpole. Maana hayo ndio yameifanya china ikue kiuchumi.
Wamarekani wamepeleka mitaji China yes, lakini wachina pia wana intellectual na technical capability sawa au hata zaidi ya Marekani hasa kwenye emerging technologies kama AI na nyinginezo. Mi wala sina ushabiki wa nani zaidi au bora kati ya mmarekani na China. Ila sitaki pia tuaminishwe kwamba eti mtu akishakuwa na nguvu ya kiuchumi basi akupangie hata mambo yako ya jikoni.
 
Mbona habari yenyewe ya kuchonga?. Hakuna wa kuwadindia G7. China aendelee na BRICS aache maneno.
Hao G7 ndio wanataka kuidindia China sasa kwa taarifa yako.

Mojawapo ya agenda yao kwenye kikao chao cha mwaka huu pale Japan ilikuwa ni ku-agree new initiatives to fight Chinese economic coercion

Ijapokuwa hawakuitaja China direct lakini ilikuwa wazi waliilenga China.

Ukuzi wa China unawaumiza sana vichwa hao wanaojiita G7
 
Na inashangaza sana. Sijui nini kinawaaminisha hawa wanaojiita G7 kufikiri ni kosa nchi zingine kuinuka kiuchumi? Na hapa tustuke wabongo kudhani kwamba hayo malengo ya UN SDGs yana nia ya dhati ya kuziinua nchi hizi zetu kiuchumi.
 
Na inashangaza sana. Sijui nini kinawaaminisha hawa wanaojiita G7 kufikiri ni kosa nchi zingine kuinuka kiuchumi? Na hapa tustuke wabongo kudhani kwamba hayo malengo ya UN SDGs yana nia ya dhati ya kuziinua nchi hizi zetu kiuchumi.
Hao jamaa wanataka sera zao hasa Marekani ndo zifuatwe na mataifa yote

Kwa mfano Marekani akitaka taifa fulani liwekewe vikwazo vya kiuchumi basi mataifa yote duniani yakubaliane naye

Mchina anatumia coercion measures kama vile Marekani anavyotumia economic sanctions.

Ila akifanya Mchina wao hawataki wanasema anaharibu kimakusudi global chain supply na eti ni kinyume na terms za Shirika la Biashara Duniani, WTO (World Trade Organization)

Cheki mifano ya trade coercion zilizofanywa na China ambazo wao wanazipinga, ila angekuwa ni Mmarekani wote wangemsikiliza basha wao wangemuunga mkono

 
Mwelekeo wa kidunia wa Neo-colonialiasm.....
 
[emoji2956]
 
The bilderberg group
 
Nilishindwa kuwaelewa mwanzani ilikuwa G8, kwa maana kwamba ni umoja wa nchi zilizoendelea kiviwanda 8 wakiwemo Urusi. Ghafla Urusi wakatolewa ikabaki G7 sasa sijui viwanda vya Urusi vilikufa vyote ghafla[emoji3][emoji3]..
Sio tu viwanda ndo vitakuweka G7 vipo vitu vingine ikiwepo kujali humam rights ndio maana China hayupo humo , hayo mataifa yote yaangalie vzr yana mifumo mizur ya kisiasa , China na Urusi haina mifumo imara ya kisiasa
 
Kuna wanaoitwa "maskini jeuri". Wanajali heshima yao na hawako tayari kuiuza kwa gharama yoyote!! Watakuambia "potelea mbali na pesa yako". Watu kama mwalimu Nyerere, Robert Mugabe, Fideral Castro nk.
Una uhakika hao walikuwa masikini jeuri?
 
Na we mkuu hebu acha misihara bwana ulishaambiwa bosi hanuniwi we unakumbuka majuzi tu Biden acha g7 aliwaita Marais wa Africa amewakusanya kama vitoto vyake vya kuzaa na Kila raisi aliyeitwa pale katika amejaa kichwa. Ni nani rais hapa kwetu Africa na ni wa nchi gani ana ubavu huo? Kwenye msiba wa malkia wamepandishwa kwenye daldala utadhani sio hawa wanaongozwa na ving'ora na mikwara mingi huku kwetu.
Tusijaribu kudanganya watu historia inaonyesha kwamba kila aliyejaribu kuja kinyume na hawa jamaa wananchi wake walibeba gharama ya hiyo misimamo ila mwisho wa siku mtawala akibadilika lazima atawalegezea tu
 
Maisha yako ni bila teknolojia ya gari, ndege, simu na zingine ni sawasawa na bure...kama wangegundua hizo tech na wakakataa kuzitoa nje ili zikae kwa ajili ya wanannchi wao pekee...sisi huku Dunia ya tatu tungebaki kama kondoo.
 
Maisha yako ni bila teknolojia ya gari, ndege, simu na zingine ni sawasawa na bure...kama wangegundua hizo tech na wakakataa kuzitoa nje ili zikae kwa ajili ya wanannchi wao pekee...sisi huku Dunia ya tatu tungebaki kama kondoo.
Hivi unajiona kweli hicho ulichokisema? Ukiachilia mbali kwamba ugunduzi wao wa teknolojia hauna maana kama hawatatafuta masoko ya hizo tech nje ya mipaka yao, still you can bet kwamba kuna tech wanazo sisi hatuna na hatutakuja kuzipata (mfano tech za kwenda Mars, n.k) yet tunaishi maisha yetu na tunadunda. Utoshelevu wa mtu hautokani na material prosperity kama ulikuwa hujui. Na kuna maisha waliyaishi watu wa zama za kale na wakaishi miaka mingi sana kuliko utakayoishi wewe na kaiphone kako.
 
Baada ya Marekani inafuatiwa na China ndio taifa la pili kwa kuichangia UN na taasisi zake

UN regular budget 2023:

USA πŸ‡ΊπŸ‡Έ (22%),
China πŸ‡¨πŸ‡³ (15.25%),
Japan πŸ‡―πŸ‡΅ (8.03%)
Germany πŸ‡©πŸ‡ͺ (6.11%)
Tatizo vijana wanalishwa sana propaganda, na wanawaona US miungu watu!
China hata ifanye jema kiasi gani,watajifanya hawaoni!
 
That said sikukatishi tamaa usijitaftie connections zako na wamagharibi kama hiyo itakusaidia mkate wa mezani. Ila as for me (na nina uhakika na watanzania kama wote hivi) hatuweki matumaini ya maisha yetu kwa kudra za G7. Mungu katupa afya bure, akili bure na nguvu za mwili bure na tunavitumia hivyo kufanya kazi kwa bidii hili mkono uende kinywani, huku tukimshukuru moyoni kwa zawadi ya maisha haya. Hakuna nafasi ya kujipumbaza na ma G7 na magenge maslahi mengine kama hayo.
 
Reactions: Ame
Mrusi yuko kama jibwa KUBWA lisilo ng'ata hana faida kimataifa
Epuka kuropoka hovyo hovyo!Hawa ndio top ten wanaochangia UN!

  1. United States (27.89%)
  2. China (15.21%)
  3. Japan (8.56%)
  4. Germany (6.09%)
  5. United Kingdom (5.79%)
  6. France (5.61%)
  7. Italy (3.30%)
  8. Russian Federation (3.04%)
  9. Canada (2.73%)
  10. Republic of Korea (2.26%)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…