Nani ana akili kuliko wote JF?

Wajameni nina swali.
Who is the smartest person on JF?
Yani genius, akili mingi, great thinker..kuliko wote.
Nataka nimjue kipanga wetu.
Maxence Melo na Mwenzake Mike Mushi kwani bila Juhudi zao, Akili zao na Ubunifu wao wa Kutukuka leo hii kusingekuwepo na hili Jukwaa ( Jamvi ) linalotupa Kiburi na Kutujenga Kifikra hadi Kimtazamo wengi Wetu.

Pongezi zangu nyingi sana tu Kwao.
 
Mbn umeingiza mambo ya elimu hapa? Mi nimeulizia akili tu bwana.
 
Akili zipi unazungumzia,

-Unaweza kua na akili za Magari usiwe na akili za biashara
-ukawa na akili za kiimani usiwe na akili za mapenzi
-ukawa na akili za mpira usiwe na akili za electronics
Hizo wewe unaongelea maarifa.
Unaweza kuwa na maarifa ila huna akili.
Mimi naongelea akili sio maarifa.
 
Maxence Melo na Mwenzake Mike Mushi kwani bila Juhudi zao, Akili zao na Ubunifu wao wa Kutukuka leo hii kusingekuwepo na hili Jukwaa ( Jamvi ) linalotupa Kiburi na Kutujenga Kifikra hadi Kimtazamo wengi Wetu.

Pongezi zangu nyingi sana tu Kwao.
Hicho sio kigezo...Yeye anaweza kuwa njia tu, ila kumbe alipofungulia jf wakaja watu wenye akili kumzidi yeye.
 
Sijawahi kuwaza kwamba kuna member ambaye anaweza kuwa kipanga in general lakini natambua kwamba humu ndani kuna vichwa ni msaada mkubwa sana katika field zao so kwa upande fulani ni magenious lemme appreciate them:
Wa kwanza ni CHIEF MKWAWA huyu jamaa kwenye masuala ya Information technology yupo juu sana hakuna tatizo ambali hana solution nalo ni msaada mkubwa sana kwa watu

Kwenye field ya magari na vyombo vya usafiri kuna ndugu yangu Extrovert na jamaa yangu JITU LA MIRABA MINNE
Binafsi Pascal Mayalla Humble African @Da'vinci na yule jamaa kwenye jukwaa la international forum anayechambua Silaha huwa nawachukulia magenious kwa mtindo fulani hivi bila kusahau Mshana Jr na LIKUD..Halafu kuna mwamba anaitwa Nguruvi3 nae naweza kumuweka kama genious...@Scars nae naweza kumuweka kwenye list ingawa si muanzishaji wa thread sana ila michango yake nae imejaa nondo nikiendelea kuwakumbuka watu nitaupdate comment..Ila hata mimi ni genious lakini sio kwa jamii forums maana nikiri wazi jamiiforums imenifanya nijue vitu vingi sana yaan mada yoyote itakayoanzishwa sehemh nilipo basi ntakuja na nondo kali sana na hii yoe ni kutokana na Jf,kwenye vijiwe vya kahawa wananikubali kinoma lakini hii ni kutokana na mchangi wa jamiiforums,hata Melo nilishwahi kumwambia hii tulipokuwa tunachati facebook
 
Hicho sio kigezo...Yeye anaweza kuwa njia tu, ila kumbe alipofungulia jf wakaja watu wenye akili kumzidi yeye.
Mbona hao Watu wako hawakuja na Ugunduzi / Ubunifu wa Mtandao huu / kama huu wa JamiiForums?

Kwa mfano Wewe mwenyewe tu unabishana nami hapa kupitia Mtandao walioubuni Wao sasa Wewe na Wao nani ni 'Genius' hasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…