Nani ana akili kuliko wote JF?

Nani ana akili kuliko wote JF?

Wajameni nina swali.
Who is the smartest person on JF?
Yani genius, akili mingi, great thinker..kuliko wote.
Nataka nimjue kipanga wetu.
Maxence Melo na Mwenzake Mike Mushi kwani bila Juhudi zao, Akili zao na Ubunifu wao wa Kutukuka leo hii kusingekuwepo na hili Jukwaa ( Jamvi ) linalotupa Kiburi na Kutujenga Kifikra hadi Kimtazamo wengi Wetu.

Pongezi zangu nyingi sana tu Kwao.
 
Akili za kishule za kushindanisha wanafunzi Zina athiri mpaka uraiani ama kwenye maisha. Maisha sio mashindano Wala kufaulu mtihani. Set your goals to achieve or compet you vs you and not you vs me.
Mana huwezi shindanisha samaki na ndege kwa uwezo wa kupaa angani ama kuogelea majini.
Ama tumbili na mbuzi kukwea miti.
Namaanisha Kama Jana ulikuwa umepanga Basi angalau Leo uwe kwako ndio mashindano halisi hayo.
Kila mtu Ana namna alivyoumbwa hujasoma kuwa Kuna eight areas of human intelligence sema shuleni wanapima Aina mbili tu mkuu.
So zingine sita shule haizitambui.
Kumbuka huu mfumo wa shule ulianzishwaga ili kutengeneza vibarua wa kufanya kazi viwandani vya wajanja wachache na ndio hao hao waliosema work hard badala ya work smart,jiulize mbona mabaamedi na wafanyakazi wa viwandani wanaofanya kazi hawapumziki labda nusu saa tu ya kula Ila hawana mafanikio, so walitageti kuku brainwash na wakafanikiwa.
Pia wakaambiwa kuwa asiyefanya kazi na asile ili kila mtu akatafute kazi awafanyie. Mbona wazee na watt na disabled hawafanyi kazi Ila wanakula mkuu na je wagonjwa na wao wasile ama.

Elon musk akaanzisha shule yenye mfumo ambao sio huu uliozoea watt wake wote na wengine wajanja wachache wameanza kupeleka watt wao kwa shule yake.
Mana anadai hajasomea havard Ila anaajiri waliosomea havard.
Pia watu wanachanganya intelligence na elimu. Watu huwa hawajui tofauti ama elimu na akili kwa lugha rahisi.
Ndio Mana inatakiwa mtt asipimwe kwa mitihani.
Mana hapa mtaani hatushindani kuwa leo Nimekula samaki jirani akala dagaa Basi naye kesho ale samaki ili anijibu kuwa uwezo anao.
Ishi maisha yako unavyowaza na sio kuigaiga ama kushindana,Basi kashindane na bolt ronado Jordan Mayweather Warren bill gate Jack ma tata Benzos na Elon utakufa unashindana na hutoishi hata siku moja.
Mbn umeingiza mambo ya elimu hapa? Mi nimeulizia akili tu bwana.
 
Akili zipi unazungumzia,

-Unaweza kua na akili za Magari usiwe na akili za biashara
-ukawa na akili za kiimani usiwe na akili za mapenzi
-ukawa na akili za mpira usiwe na akili za electronics
Hizo wewe unaongelea maarifa.
Unaweza kuwa na maarifa ila huna akili.
Mimi naongelea akili sio maarifa.
 
Maxence Melo na Mwenzake Mike Mushi kwani bila Juhudi zao, Akili zao na Ubunifu wao wa Kutukuka leo hii kusingekuwepo na hili Jukwaa ( Jamvi ) linalotupa Kiburi na Kutujenga Kifikra hadi Kimtazamo wengi Wetu.

Pongezi zangu nyingi sana tu Kwao.
Hicho sio kigezo...Yeye anaweza kuwa njia tu, ila kumbe alipofungulia jf wakaja watu wenye akili kumzidi yeye.
 
Sijawahi kuwaza kwamba kuna member ambaye anaweza kuwa kipanga in general lakini natambua kwamba humu ndani kuna vichwa ni msaada mkubwa sana katika field zao so kwa upande fulani ni magenious lemme appreciate them:
Wa kwanza ni CHIEF MKWAWA huyu jamaa kwenye masuala ya Information technology yupo juu sana hakuna tatizo ambali hana solution nalo ni msaada mkubwa sana kwa watu

Kwenye field ya magari na vyombo vya usafiri kuna ndugu yangu Extrovert na jamaa yangu JITU LA MIRABA MINNE
Binafsi Pascal Mayalla Humble African @Da'vinci na yule jamaa kwenye jukwaa la international forum anayechambua Silaha huwa nawachukulia magenious kwa mtindo fulani hivi bila kusahau Mshana Jr na LIKUD..Halafu kuna mwamba anaitwa Nguruvi3 nae naweza kumuweka kama genious...@Scars nae naweza kumuweka kwenye list ingawa si muanzishaji wa thread sana ila michango yake nae imejaa nondo nikiendelea kuwakumbuka watu nitaupdate comment..Ila hata mimi ni genious lakini sio kwa jamii forums maana nikiri wazi jamiiforums imenifanya nijue vitu vingi sana yaan mada yoyote itakayoanzishwa sehemh nilipo basi ntakuja na nondo kali sana na hii yoe ni kutokana na Jf,kwenye vijiwe vya kahawa wananikubali kinoma lakini hii ni kutokana na mchangi wa jamiiforums,hata Melo nilishwahi kumwambia hii tulipokuwa tunachati facebook
 
Hicho sio kigezo...Yeye anaweza kuwa njia tu, ila kumbe alipofungulia jf wakaja watu wenye akili kumzidi yeye.
Mbona hao Watu wako hawakuja na Ugunduzi / Ubunifu wa Mtandao huu / kama huu wa JamiiForums?

Kwa mfano Wewe mwenyewe tu unabishana nami hapa kupitia Mtandao walioubuni Wao sasa Wewe na Wao nani ni 'Genius' hasa?
 
Back
Top Bottom