Nani anatengeneza faida kubwa kati ya mzalishaji wa bidhaa na mtu wa kati?

Nani anatengeneza faida kubwa kati ya mzalishaji wa bidhaa na mtu wa kati?

Mzalishaji obviously ndie anaepiga pesa ndefu Kwa sababu yeye huuza products nyingi Kwa hao middle men.
For single product unit middle man anaweza kupata faida zaidi ya mzalishaji. Lakini Kwa sababu huyu middleman anachukua sehemu ndogo Tu ya manufactured product hawezi kumzidi mzalishaji ambao anapata faida ya product yote iliozalishwa.
Unalinganisha vipi? Ulinganishi wako sio sahihi, maana unachanganya na ukubwa wa mtaji. Weka wote wana mtaji sawa alafu jibu hilo swali.
 
Unalinganisha vipi? Ulinganishi wako sio sahihi, maana unachanganya na ukubwa wa mtaji. Weka wote wana mtaji sawa alafu jibu hilo swali.
Kuna uwezekano wa mzalishaji na middle man kuwa na mtaji Sawa?
Labda useme mkulima na middleman. Kwa Mimi mzalishaji ni Yule mwenye kiwanda. Labda unipe mfano wa mzalishaji anaezidiwa na middleman wake!
 
Mzalishaji ndie anaetengeneza faida kubwa maana ndie anaejua siri kubwa ambayo ni gharama za uzalishaji wa hiyo bidhaa

Mfano Mzalishaji Mo ndie anaejua siri kwamba Mo energy moja thamani yake ni shilingi 50 tu kuizalisha. Ila yeye ananuuzia middleman Mo energy moja kwa shilingi 450. Hivyo anapiga 400 kama faida kwa energy moja.

Huku middleman yeye anamuuzia mlaji wa mwisho mo energy moja kwa shilingi 600. Hivyo yeye anapata faida ya shilingi 150 kwa kila mo energy moja
Nimekuelewa sana
 
mzalishaji ndio mmiliki wa mfumo kwahiyo hakuna wakumpangia au kumkadiria kiwango cha pesa anachotakiwa kukipata ila mtu kati ni msaidizi tu ambae anamuunganisha mzalishaji na mlaji kwahiyo kiwango chake cha kipato kipo chini ya mzlishaji, kwa maana mzalishaji akiamua kuuchezesha mfumo na kubadili vigezo na masharti vya kumkandamiza mtu kati ili azidi kujiongezea ukwasi basi mtu kati anaathirika moja kwa moja.... kwa maana nyingine unaweza kusema kwamba mzalishaji ni mfanya biashara wakati huo huo mtu kati ni mfanya kazi.

kwahiyo kazi kwako mkuu kwenye kuchagua, kama unataka uwe mfanya kazi nenda na middleman ila kama unataka uwe mfanya biashara basi kuwa mzalishaji.
Alafu kumbe naweza nikawa mzalishaji at the same time nikawa mtu kati.. Kwa product hiyo hiyo ninayo zalisha .
 
Alafu kumbe naweza nikawa mzalishaji at the same time nikawa mtu kati.. Kwa product hiyo hiyo ninayo zalisha .
Kwa maana ya kupitia mfumo utakao utengeneza inawezekana ila kwa wewe mwenyewe ni ngumu kwa maana watu wengi wanapambana kutengeneza biashara ambazo haziwategemei wao ili ziweze kwenda.
 
Wakuu habari zenu

Naomba kuuliza kwenu watu wa biashara na uchumi

Hivi kati ya producers/manufacturer Na Middleman nani yupo good position ya kutengeneza faida kuliko mwenzake.

Mimi ni middle man kwenye biashara X nataka ku shift kuwa kama manufacturer
Mzalishaji wa viwanda au wakulima?

Mtu kati anatengeneza hela nyingi sana kwenye kilimo

Kwenye uzalisgaji viwanda wazalishaji wanapata hela nyingi sana maana wanatoa percent tu kwa wachuuzi au watu kati ,ila wao wanauza bodhaa nyingi sana
 
unashindana vipi? mtu anaye jipangia bei auze bei gani? product yake... Alafu anakuja kupangia muuza jumla mpka mlaji wa mwisho!
Hakuna mtu anaejipangia bei kubwa itakayozidi kiwango ambacho mzalishaji amepanga au anaexpect kama ndio bei ya mwisho

Pabda hizi bidhaa za mitaani


Mfano soda huwez panga bei yako, cement huwezi panga bei yako ,sukari huwez panga bei yako
 
Alafu kumbe naweza nikawa mzalishaji at the same time nikawa mtu kati.. Kwa product hiyo hiyo ninayo zalisha .
Ukiwa mzalishaji na muuzaji mwenyewe hufiki mbali sana , lazima watu kati wakusaidie

Huwez sambaza cement nchi nzima

Na hata ukiwa mzalishaji huwezi jipangia tu bei ambayo unataka maana washindani ni wengi

Labda uwe na bidhaa ambayo haipo popote
 
😹
Hata uwachukue wasambazaji wote wa Mo kwa pamoja hawawezi mzidi kwenye faida jumla kuliko yeye
Anakuuzia wewe upate asilimia fulani tu
Aki simamisha uzalishaji mwezi mmoja tuu ni kilio nchi nzima 😄
 
Back
Top Bottom