Unajua haya mambo inafika kipindi inabidi tu tukae kimya
Ugaidi wa aina yoyote ile wala hauuhusiani na uislamu kwa namna yoyote ile,ila unahusiana ima na watu ambao ni waislamu kwa majina au watu ambao wamelishwa mafundisho ambayo sio sahihi juu ya uislamu
Mfano mzuri ni talibani,kuna mhanga mmoja alilishwa matango pori na alikuwa katika listi ya kujiripua lakini kwa uwezo wa Allah kuna mazingira yalitokea akaja kupata mafunzo sahihi ya dini ya kiislamu na kuona upotofu mkubwa ambao alilishwa na hao wapuuzi ambao wanapigana kwa mgongo wa uislamu
Na hayo alisema katika kongamano kubwa la mjadala katika waislamu na wakristo lililoenda kwa jina la DINI YA KIISAMU NI DINI YA MAGAIDI?
Sasa tuje ktk upande wa pili wa uelewa mbovu juu ya mabikra na unywaji wa pombe,,,kwa kawaida wanaume tunapenda wanawake,pombe,mali na kadhalika,,na hasa wanawake ndio ugonjwa wetu sana,kama kuna mwanaume anabisha hapa anyooshe kidole nimuone
Sasa Allah anatuambia wanadamu kuwa hawa wanawake ambao tunababaika nao hapa duniani sio lolote ukilinganisha na hao wa huko akhera,,tuepuke zinaa na tulinde tupu zetu isipokuwa kwa wake zetu ili tupate mwisho mwema
Watu wataofanya matendo mazuri na mizani ikawa mizito siku ya kiyama basi pamoja na mambo mengine watapata wanawake warembo ambao hawajawahi kuguswa kabla,hao hawana mzunguko wa hedhi hakika wametakasika sana,wana macho ya vikombe na uzuri usio na kifani,,,kwahiyo tuache ujinga wa kubabaika na wanawake wa dunia hii kwani kuna warembo huko akhera ambapo jicho halijapata kuona
Litakuja swali je hawa wanawake wa hapa duniani nao wataolewa na nani?
Hakika jibu ni kwamba wanawake wema wa duniani watabadilishwa maumbo yao lkn hao ni wanawake wema,watakuwa warembo na wenye kuvutia umri wao ni rika la mabinti,,mambo yetu yaleeee ya saa sita nadhan mmenipata!
Na huko peponi watu watakuwa umri wa ujana na hakuna kuzeeka,,,sasa just imagine kijana baro baro na mabinti warembo inakuwaje hapo,kwahiyo tunapewa hamasa kwamba tutende mema tukapate hayo ambayo tunayatamani hali yakiwa katika ubora na uzuri ulioje
Pombe ya duniani ina madhara mengi,kuna maradhi ndani yake,kuumwa na vichwa na kuamka hoi,,,lakini pombe ya peponi ni yenye radha nzur kwa wanywaji na isiyo na madhara kwa mtumiaji wala haitoi akili za watu,na kinywaji bora kabisa kwa watumiaji
Tunaambiwa hivyo ili tuache pombe ambayo ni haramu bali huko akhera tutakutana na kinywaji safi kabisa kwa watumiaji,kwahiyo tuache ujinga
Shukrani