Nani wa kumfungia kiongozi wetu Speed Governor? Nchi itapigwa mnada hii

MKUU CCM NI SIKIO LA KUFA NA MBAYA ZAIDI HIZO PESA WANAWEKA MIFUKONI MWAO
 
Porojo zako hazina msingi wowote hata hivyo,

NCHI iko katika uelekeo sahihi sana
 
Sasa kwanini tukawakopee wezi Kwa unachokiita " Nia njema"?

Saizi Hadi mifumo ya control namba inaingiliwa na waizi!!

Kwanini tusiondoe kwanza waizi ndipo twende kukopa?
Hoja yako ni nzuri na tayari inafanyiwa kazi
 
Hakutakuwa na tangazo la zabuni ya kuuza nchi. Sio kwamba gazetii au international business portal zitatangaza kwamba kuna nchi inauzwa huku. NO

Mtakuja kushtuka tu heeeh kumbe mmeuzwa miaka mitatu iliyopita. Itakuwa mmechelewa sana, kwa sababu hayo mauzo hayatakuwa na fidia bali ni nchi kuendelea kuwa chini ya wanunuzi.

Nchi inaweza isiuzwe kwa mnunuzi mmoja, huyu anaweza kuuziwa madini yule bandari na bahari, yule mbuga za wanyama na wanyama. Kwa hiyo mtakuta sehemu zote zimeuzwa isipokuwa nyinyi tu ndio hamjauzwa. Sasa hamtakuwa na pakwenda.

Hii kidogo kidogo ndio mchakato wenyewe. Amini hivyo, na Sio kusubiri eti kutakuwa bango kuuubwa kila mahali kwamba nchi imeuzwa.

Hamtakuwa na mtu wa kumbana kwa sababu wauzaji wote muhimu wamepewa kinga kisheria.
 
Na ndiyo wakati huo huo watu wengine wataamua kuhamia Marekani, Burundi, Rwanda, Oman, nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…