Nani yuko kwenye nafasi nzuri ya kupiga hela kati ya Mhasibu na Afisa manunuzi?

Nani yuko kwenye nafasi nzuri ya kupiga hela kati ya Mhasibu na Afisa manunuzi?

Habari za jioni wadau!

Tukiwa watoto tulikuwa tunawaza kazi nzuri ni udakatari na sheria ila kwa kadri umri unavyosonga unagundua hata huko ni umasikini tu sana sana uibe dawa ila kutoboa sio rahisi.

Baada ya kutafakari muda mrefu nimeamua kubadilisha fani kabisa na hizo fani tajwa hapo juu nimeona kidogo huwezi kosa hela ya dagaa na bia mbili nje ya mshahara.

Sasa naomba mnisaidie kwa wizarani au taasisi za serikali kati ya hizo fani mbili ipi unaweza kula kwa urefu wa kamba kuliko nyingine iwe kwa deal halali au haramu.

Karibuni kwa uzoefu wenu.
Usicheze na kitu inaitwa manunuzi, huyo mhasibu mwenyewe akitaka printer ya ofcn kwake anamwambia mzee wa manunuzi amuagizie, akiagiza printer kama ni milion 1.5 anaweza akaweka na chake Cha juu ikawa yamkini Milion 1.8 na baadae mhasibu yule analipa, mtu wa biashara anachukua Ile laki 3 anampa mtu wa manunuzi anaenda kunywa biereeeeee[emoji23][emoji23]

Any way mtoa mada usiende kusomea wizi maana swali lako limelenga kinacho julikana
 
Nashukuru sana mkuu kwa mchango wako wa kiuweledi. Hawa wengine wananitisha wakati wao wanaendesha Harrier new model au Dualis kwa mishahara ya laki 7 inawezekana vipi? Wanafiki wakubwa.
 
Mama wa Biharusi tumempa jukumu la Kamati ya Maandalizi ya harusi ya binti yale kwenda kutafuta Kuku wa shughuli ya Mwanae kenda kutuletea Vikuku kama njiwa halafu bei ya Juu tukajua kapigwa kwa ule utuu uzima wake …kufuatilia kumbe kacheza dili na Muuzaji wapate kama elf 5 kwa kila vikuku bile vya sijui wiki nne tu

Unapambana kujibana ujenge kijumba chako pekee kwny uhai wako unamshirikisha Mkeo wa maisha lakin cha ajabu huyo huyo anashirikiana na mafundi kuiba
Huyo mama kiboko
 
Hao manunuzi ndio huwa wanapitisha hata tenda kwa kampuni fulani lijenge jengo au barabara, hapo watu wenye makampuni huwa wanahinga pesa ndefu kupata tenda..... Manunuzi wanapiga hela ila wanakuaga wachache sana, hata ukisomea hio kozi ni mziki kupata ajira yake.

Kwa wahasibu hawa ni kawaida sana kusikia wanafungwa jela wakipiga pesa kwa hio akili ya ziada inabidi itumike kupiga pesa, ila hawa jamaa wakipataga tundu hakunaga wa kuwafikia aisee, ni wanabutuaga sio mchezo..... kazi za uhasibu zipo nyingi kuzidi za manunuzi.

Ila kama unataka uzichape kisawasawa nenda kwenye siasa huko
 
Hao manunuzi ndio huwa wanapitisha hata tenda kwa kampuni fulani lijenge jengo au barabara, hapo ili uoate tenda ni kawaida kutoa rushwa hata ya milioni 100.

Manunuzi wanapiga hela ila wanakuaga wachache sana, hata ukusomea hio kozi ni mziki kupata ajira yake.

Kwa wahasibu hawa ni kawaida sana kusikia wanafungwa jela wakipiga pesa kwa hio akili ya ziada inabidi itumike kupiga pesa, ila haaa jamaa wakipataga tundu hakunaga wa kuwafikia..... kazi za uhasibu zipo nyingi kuzidi za manunuzi
Ahsante sana. Hii ndio michango ya kujenga
 
Mfano kununua nguzo ya umeme bei ya serikali laki 1. Mimi nikitafuta mtu akaniuzia elfu 40 hapo nimebakiwa na elfu 60.
Huo sio wizi bali ni ujanja tu.
Na is ijulikane kuwa ulinunua elfu 40 hiyo nguzo. Na wewe kwa kuficha hilo utakuja na risiti zinazo onesha ulinunua ngozi moja sh 100,000. Huo ni udanganyifu, jela itakuhusu ndugu yangu.
 
Habari za jioni wadau!

Tukiwa watoto tulikuwa tunawaza kazi nzuri ni udakatari na sheria ila kwa kadri umri unavyosonga unagundua hata huko ni umasikini tu sana sana uibe dawa ila kutoboa sio rahisi.

Baada ya kutafakari muda mrefu nimeamua kubadilisha fani kabisa na hizo fani tajwa hapo juu nimeona kidogo huwezi kosa hela ya dagaa na bia mbili nje ya mshahara.

Sasa naomba mnisaidie kwa wizarani au taasisi za serikali kati ya hizo fani mbili ipi unaweza kula kwa urefu wa kamba kuliko nyingine iwe kwa deal halali au haramu.

Karibuni kwa uzoefu wenu.
Naona unajiandaa kuwa ' fisadi', kazi kweli kweli.
 
Naona unajiandaa kuwa ' fisadi', kazi kweli kweli.
Mfano umeambiwa wapangie hawa wageni hoteli yenye thamani ya laki 5 kwa siku. Wewe ukaenda hotelini ukaongea vizuri wakakubali kwa laki 4. Hiyo laki moja uirudishe wapi kwa katibu mkuu au kwa mkuu wa idara?
 
..Irudishe kwa aliyekupa kazi.
 
Unanishauri niingie kwenye siasa?
kama unaweza hiyo ndio sehemu pekee utatoka mapema. si unaona steve nyerere leo tu kwa press conference ile ameshakuwa maarufu na chart yake inapanda regardless of what ameongea.muda si mrefu utasikia anatajwa kuteuliwa sehemu. mark my words.
 
Na bado tunashangaa kwanini kama Taifa / Nchi tunapiga hatua kila siku za kurudi nyuma ?

Ukweli ni kwamba kama Taifa kuanzia viongozi mpaka wananchi tume-lose the Plot..., Yaani utafikiri tupo kwenye nchi ya kupanga na sio nchi yetu....

Tunabomoa / chukua mbao za milango ili tujenge madirisha
 
Wengi mmemtukana mleta mada..ila kiukweli hili suala la upigaji chanzo ni viongozi wetu..wananchi wanaona viongozi wanayoyafanya wanaiba mali na kuuza rasilmali za nchi huku wakituletea ngonjera za uzalendo ambao wenyewe hawana..hivyo kila mtu sasa ni kutafuta chaka piga utakavyoweza.

Hii nchi ishaharibiwa kitambo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Habari za jioni wadau!

Tukiwa watoto tulikuwa tunawaza kazi nzuri ni udakatari na sheria ila kwa kadri umri unavyosonga unagundua hata huko ni umasikini tu sana sana uibe dawa ila kutoboa sio rahisi.

Baada ya kutafakari muda mrefu nimeamua kubadilisha fani kabisa na hizo fani tajwa hapo juu nimeona kidogo huwezi kosa hela ya dagaa na bia mbili nje ya mshahara.

Sasa naomba mnisaidie kwa wizarani au taasisi za serikali kati ya hizo fani mbili ipi unaweza kula kwa urefu wa kamba kuliko nyingine iwe kwa deal halali au haramu.

Karibuni kwa uzoefu wenu.
WaTz na wizi na rushwa! Hili ni janga, Mungu tusaidie!
 
Back
Top Bottom