Nani yupo nyuma ya vuguvugu la kuvunja Muungano

Nani yupo nyuma ya vuguvugu la kuvunja Muungano

Nina taka kuwa rais wa Zanzibar
Ninataka kumiliki ardhi Zanzibar
hayo ndio malengo yangu so muundo wa muungano umekuwa kikwazo kwangu.
Serikali tatu utazugharamia wewe?..muundo wa sasa wa muungano umekwaza wapi maisha yako ya kila siku?
 
Na

UISLAMU NI DINI YA HAKI.
Ninaomba hio haki tuilete hapa katika hii hoja.
Kama ambavyo ZANZIBAR ni nchi na ina rais wake na Tanganyika ipate rais wake ambaye mzazibari hataruhusiwa kugombea nafasi hio.
Then TUBAKI NA MUUNGANO, TANZANIA
Tanganyika haipo,muambiwe mara ngapi?
 
Unazungumzia makadirio wakati sensa ya 1958 ilisema waislam ni 66% na wakristo ndiyo walikua wachache wakizidiwa na waabudu dini za jadi
Kwenye andiko langu nimesema ukristo ulianza hubiriwa late 1800s na kwamba early 1900s walikua hawafik 20k,naona umeniunga mkono
Maana hata Nyerere alibatizwa sekondari baada ya kumsoma Julius Caesar na kuvutiwa nae akachukua hadi jina,sasa Nyerere alikua sekondari lini?

Kuna mambo mawili tofauti hapa ambayo yanahitaji kutenganishwa.

Kwanza, ni kweli kwamba Ukristo ulianza kuenea kwa nguvu Tanganyika mwishoni mwa karne ya 19 kupitia wamisionari. Pia ni kweli kwamba mwanzoni mwa miaka ya 1900 Wakristo walikuwa wachache ukilinganisha na idadi ya watu wote wa Tanganyika.

Lakini suala la sensa ya 1958 linahitaji ushahidi rasmi. Watu wengi hutaja takwimu za 66% Waislamu, lakini mara nyingi hawatoi ripoti rasmi ya sensa yenyewe. Wanahistoria wengi wanakubaliana kwamba kabla ya uhuru kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa bado wanafuata dini za jadi za Kiafrika, na ndiyo sababu takwimu hutofautiana sana kati ya vyanzo.

Pili, kuhusu Nyerere, ni sahihi kwamba alibatizwa akiwa kijana na akachukua jina "Julius". Lakini si sahihi kusema alibatizwa sekondari baada ya kusoma Julius Caesar.

Julius Nyerere alibatizwa katika Kanisa Katoliki tarehe 23 Desemba 1943 akiwa mwanafunzi wa Tabora Government School. Alikuwa na umri wa miaka takriban 21. Jina "Julius" alipewa wakati wa ubatizo kama ilivyokuwa kawaida kwa waongofu wengi wa Kikristo wakati huo.

Hakuna ushahidi wa kihistoria unaokubalika unaoonyesha kwamba alichagua jina Julius kwa sababu ya kusoma Julius Caesar. Hilo limekuwa simulizi linalosambazwa mara kwa mara lakini wanahistoria wengi hawajalithibitisha kwa nyaraka za kuaminika.

Kwa hiyo, kama hoja ni kwamba Ukristo ulikuwa umeenea kwa kiasi kikubwa Tanganyika kabla ya uhuru, hilo linaweza kujadiliwa kwa takwimu. Lakini kutumia hadithi ya Julius Caesar kuthibitisha hilo si ushahidi wa kihistoria.

Ukweli ni kwamba kabla ya ukoloni hakukuwa na jamii kubwa za Kikristo Tanganyika, na ukuaji mkubwa wa Ukristo ulitokea katika kipindi cha wamisionari wa Kijerumani na Waingereza. Hilo ni jambo ambalo wanahistoria wengi wanalikubali.
 
Mkwawa alikuwa mtawala wa wahehe huko. Taifa la wahehe na mataifa mengine kama Wanyamwezi, wasukuma, wayao n.k yalikuwepo.
Hapakuwa na taifa ka Tanganyika.

Mjerumani alipofika ndiye akaketa. Dhana ya hayo mataifa ni makabila ilhali yalikuwa mataifa.

Akayaunganisha, akachora mipaka huku Mkutano wa Berlin ambao kimsingi ulihuzuriwa na mataifa ya ulaya ya kikristo yakihusika kuunda mataifa mengi unayoyaona hivi leo ya Afrika. Ikiwemo Tanganyika.
Nikumbushe, Deutsch ostafrika haikuhusisha kenya na Uganda ukiachilia mbali Rwanda na Burundi?
Sikumbuki nani aliyeiita Tanganyika Tanganyika,lakini yeyote awae,alipata Hilo jina kwa 'watanganyika' wenyewe
 
Walioasisi na kuunda Tanganyika ni wakristo wa Kijerumani. Elewa historia vizuri

Kauli hiyo si sahihi kihistoria ikiwa inamaanisha kwamba "Wakristo wa Kijerumani waliiasisi na kuiunda Tanganyika."


Ukweli wa kihistoria ni huu:


Tanganyika haikuanzishwa na wamisionari Wakristo.
Kabla ya Wajerumani kufika, kulikuwa tayari na falme, usultani, machifu na jamii mbalimbali katika eneo ambalo baadaye liliitwa Tanganyika. Mfano ni falme za Buganda (nje ya Tanganyika ya leo lakini jirani), jamii za Wachagga, Wanyamwezi, Wahaya, Wasukuma, n.k.


Jina na koloni la Tanganyika vilitokana na utawala wa kikoloni wa Kijerumani.
Kuanzia miaka ya 1880, Carl Peters na German East Africa Company walipata mikataba na kuanzisha ushawishi wa Ujerumani. Baadaye eneo hilo likawa sehemu ya German East Africa.


Tanganyika kama jina la kisiasa ilitokea baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.
Baada ya Ujerumani kushindwa mwaka 1918, eneo kubwa la German East Africa lilikabidhiwa kwa Uingereza chini ya mamlaka ya League of Nations na likaitwa Tanganyika Territory mwaka 1920.

Wamisionari Wakristo walikuwa sehemu ya mfumo wa kikoloni, lakini hawakuunda Tanganyika.
Wamisionari wa Kijerumani na baadaye Waingereza walieneza Ukristo, walijenga shule na hospitali, lakini hawakuwa waanzilishi wa nchi yenyewe. Utawala wa kikoloni uliendeshwa na serikali za Ujerumani na Uingereza.
 
Utakuaje rais wa nchi ambayo wewe siyo raia, unataka kuwa mkoloni?
Yes hii ni point niliyokuwa naitaka.
Ili kuwe na usawa inatakiwa neno ZANZIBAR IFUTWE kama ilivyofutwa TANGANYIKA na tubaki na neno TANZANIA ili tu share mambo kwa haki na usawa. Unaonaje?
 
Mkwawa alikuwa mtawala wa wahehe huko. Taifa la wahehe na mataifa mengine kama Wanyamwezi, wasukuma, wayao n.k yalikuwepo.
Hapakuwa na taifa ka Tanganyika.

Mjerumani alipofika ndiye akaketa. Dhana ya hayo mataifa ni makabila ilhali yalikuwa mataifa.

Akayaunganisha, akachora mipaka huku Mkutano wa Berlin ambao kimsingi ulihuzuriwa na mataifa ya ulaya ya kikristo yakihusika kuunda mataifa mengi unayoyaona hivi leo ya Afrika. Ikiwemo Tanganyika.

Kuna ukweli na kuna upotoshaji kidogo katika maelezo yako.

Ni kweli kwamba kabla ya ukoloni hakukuwa na nchi iitwayo "Tanganyika" kama taifa la kisasa. Kulikuwepo falme, usultani, himaya na jamii huru kama Wahehe wa Mkwawa, Wanyamwezi wa Mirambo, Wahaya, Wachagga, Wasukuma, Wanyakyusa, Wayao na wengine.

Lakini si sahihi kusema kwamba Mjerumani ndiye "aliunda Tanganyika" Alikuta watu, tawala, biashara, lugha na utambulisho tayari vipo.

Pia Mkutano wa Berlin Conference haukukaa na kuchora mipaka yote ya Tanganyika kama inavyoonekana leo. Mkutano huo uliweka kanuni za kugawana maeneo ya Afrika kati ya mataifa ya Ulaya. Mipaka mingi ilikuja kutokana na mikataba iliyofuata kati ya Ujerumani, Uingereza, Ubelgiji na Ureno katika miaka iliyofuata.

Jambo lingine muhimu ni kwamba "Tanganyika" yenyewe haikuwa jina la Kijerumani mwanzoni. Wajerumani waliita koloni lao German East Africa. Jina "Tanganyika Territory" lilianza kutumiwa rasmi na Waingereza baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mwaka 1920 walipopewa eneo hilo na League of Nations.
 
Tumetofautiana sana kwenye upeo(IQ) kwa mtu anayefikiria sawa sawa na kwa kina, hawezi kushindwa kuona chuki ya Samia juu ya Tanganyika, hajali chochote, ana kiburi cha hali ya juu sana.
Ni kama ana option B na C endapo chochote kitatokea.. nasikitika kuona vyombo vya usalama vinamuangalia tu.
Akimaliza mda wake ataiacha nchi kwenye makovu makubwa sana, huyu mtu sijui ana roho gani? Haogopi damu ya mtu.
 
Nikumbushe, Deutsch ostafrika haikuhusisha kenya na Uganda ukiachilia mbali Rwanda na Burundi?
Sikumbuki nani aliyeiita Tanganyika Tanganyika,lakini yeyote awae,alipata Hilo jina kwa 'watanganyika' wenyewe

Haijalishi jina lilitoka wapi. Ila muasisi wa Tanganyika alikuwa Mkoloni.

Kabla ya ukoloni Wahehe, wasukuma, Wanyamwezi, Waha na jamii zingine zilijitambua kama himaya na sio kama kabila.

Wazungu ndio walikuja ku-label hizo himaya kama makabila.
 
Yes hii ni point niliyokuwa naitaka.
Ili kuwe na usawa inatakiwa neno ZANZIBAR IFUTWE kama ilivyofutwa TANGANYIKA na tubaki na neno TANZANIA ili tu share mambo kwa haki na usawa. Unaonaje?

Tatizo huu si muungano ni UVAMIZI kwa hivyo inakuwa haiwezekani
 
Tumetofautiana sana kwenye upeo(IQ) kwa mtu anayefikiria sawa sawa na kwa kina, hawezi kushindwa kuona chuki ya Samia juu ya Tanganyika, hajali chochote, ana kiburi cha hali ya juu sana.
Ni kama ana option B na C endapo chochote kitatokea.. nasikitika kuona vyombo vya usalama vinamuangalia tu.
Akimaliza mda wake ataiacha nchi kwenye makovu makubwa sana, huyu mtu sijui ana roho gani? Haogopi damu ya mtu.
Kwani yule aliyeivamia Zanzibar na kuuwa maelfu ya watu na kuiweka nchi yetu mateka wa Tanganyika alikuwa na roho gani ?? aliogopa damu ya mtu ??
 
Kuna mambo mawili tofauti hapa ambayo yanahitaji kutenganishwa.

Kwanza, ni kweli kwamba Ukristo ulianza kuenea kwa nguvu Tanganyika mwishoni mwa karne ya 19 kupitia wamisionari. Pia ni kweli kwamba mwanzoni mwa miaka ya 1900 Wakristo walikuwa wachache ukilinganisha na idadi ya watu wote wa Tanganyika.

Lakini suala la sensa ya 1958 linahitaji ushahidi rasmi. Watu wengi hutaja takwimu za 66% Waislamu, lakini mara nyingi hawatoi ripoti rasmi ya sensa yenyewe. Wanahistoria wengi wanakubaliana kwamba kabla ya uhuru kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa bado wanafuata dini za jadi za Kiafrika, na ndiyo sababu takwimu hutofautiana sana kati ya vyanzo.
Sensa ya 1958 ilipelekwa umoja wa mataifa,ijahifadhiwa
Serikali huru ya askari wa vita vya msalaba walipofanya sensa 1968 wakawapunguza waislam hadi 33% na kuwapandisha wakristo hadi 30+%,wakapeleka umoja wa mataifa
Kule wakaulizwa waislam wamekumbwa na janga gani lililowaua kwa 50%,wakajiona wajinga,tangu hapo kipengele cha dini kikatolewa kwenye sensa
Mchezo wa kudai wakristo ni 30-40% tz na waislam ni wachache, ndiyo uliochochea sheikh ponda na wenzake kutaka waislam wasishiriki sensa 2012 mpaka kiwekwe kipengele cha dini,cha ajabu miongoni mwa wapingaji walikua maaskofu
Pili, kuhusu Nyerere, ni sahihi kwamba alibatizwa akiwa kijana na akachukua jina "Julius". Lakini si sahihi kusema alibatizwa sekondari baada ya kusoma Julius Caesar.

Julius Nyerere alibatizwa katika Kanisa Katoliki tarehe 23 Desemba 1943 akiwa mwanafunzi wa Tabora Government School. Alikuwa na umri wa miaka takriban 21. Jina "Julius" alipewa wakati wa ubatizo kama ilivyokuwa kawaida kwa waongofu wengi wa Kikristo wakati huo.

Hakuna ushahidi wa kihistoria unaokubalika unaoonyesha kwamba alichagua jina Julius kwa sababu ya kusoma Julius Caesar. Hilo limekuwa simulizi linalosambazwa mara kwa mara lakini wanahistoria wengi hawajalithibitisha kwa nyaraka za kuaminika.
Alichagua jina Julius baada ya kuvutiwa na Julius Caesar baada ya kusoma kitabu cha 'merchants of Venice' ambacho baadae alikitafsiri kama 'mabepari wa Venice',acha ubishi wa kijinga jinga
Kwa hiyo, kama hoja ni kwamba Ukristo ulikuwa umeenea kwa kiasi kikubwa Tanganyika kabla ya uhuru, hilo linaweza kujadiliwa kwa takwimu. Lakini kutumia hadithi ya Julius Caesar kuthibitisha hilo si ushahidi wa kihistoria
Mbona una op sana kijana,hii ni irrelevant
.

Ukweli ni kwamba kabla ya ukoloni hakukuwa na jamii kubwa za Kikristo Tanganyika, na ukuaji mkubwa wa Ukristo ulitokea katika kipindi cha wamisionari wa Kijerumani na Waingereza. Hilo ni jambo ambalo wanahistoria wengi wanalikubali.
Hili ndiyo nimesema
 
Back
Top Bottom