gallow bird
JF-Expert Member
- Aug 10, 2024
- 14,889
- 18,593
Hiyo ni serikali moja,lakini rais wa Tanzania ana mamlaka Zanzibar,kuna ofisi za muungano na vyombo vyote vya ulinzi na usalama Zanzibar, Zanzibar ikivamiwa imevamiwa Tanzania,watakaopambana ni jwtzYes hii ni point niliyokuwa naitaka.
Ili kuwe na usawa inatakiwa neno ZANZIBAR IFUTWE kama ilivyofutwa TANGANYIKA na tubaki na neno TANZANIA ili tu share mambo kwa haki na usawa. Unaonaje?
Na akina kinjekitile ni mashujaa wa ruvuma,pwani na moro mashariki siyo wa TanganyikaSasa umenielewa vizuri.
Hao kina bushiri sijui Mkwawa walikuwa mashujaa wa wahehe sio watanganyika. Muwe mnaelewa mambo
Sensa ya 1958 ilipelekwa umoja wa mataifa,ijahifadhiwa
Serikali huru ya askari wa vita vya msalaba walipofanya sensa 1968 wakawapunguza waislam hadi 33% na kuwapandisha wakristo hadi 30+%,wakapeleka umoja wa mataifa
Kule wakaulizwa waislam wamekumbwa na janga gani lililowaua kwa 50%,wakajiona wajinga,tangu hapo kipengele cha dini kikatolewa kwenye sensa
Mchezo wa kudai wakristo ni 30-40% tz na waislam ni wachache, ndiyo uliochochea sheikh ponda na wenzake kutaka waislam wasishiriki sensa 2012 mpaka kiwekwe kipengele cha dini,cha ajabu miongoni mwa wapingaji walikua maaskofu
Alichagua jina Julius baada ya kuvutiwa na Julius Caesar baada ya kusoma kitabu cha 'merchants of Venice' ambacho baadae alikitafsiri kama 'mabepari wa Venice',acha ubishi wa kijinga jinga
Mbona una op sana kijana,hii ni irrelevant
Hili ndiyo nimesema
Kwamba wanyamwezi hawakuhesabu wahehe kuwa kabila?Haijalishi jina lilitoka wapi. Ila muasisi wa Tanganyika alikuwa Mkoloni.
Kabla ya ukoloni Wahehe, wasukuma, Wanyamwezi, Waha na jamii zingine zilijitambua kama himaya na sio kama kabila.
Wazungu ndio walikuja ku-label hizo himaya kama makabila.
Kuna ukweli na kuna upotoshaji kidogo katika maelezo yako.
Ni kweli kwamba kabla ya ukoloni hakukuwa na nchi iitwayo "Tanganyika" kama taifa la kisasa. Kulikuwepo falme, usultani, himaya na jamii huru kama Wahehe wa Mkwawa, Wanyamwezi wa Mirambo, Wahaya, Wachagga, Wasukuma, Wanyakyusa, Wayao na wengine.
Lakini si sahihi kusema kwamba Mjerumani ndiye "aliunda Tanganyika" Alikuta watu, tawala, biashara, lugha na utambulisho tayari vipo.
Pia Mkutano wa Berlin Conference haukukaa na kuchora mipaka yote ya Tanganyika kama inavyoonekana leo. Mkutano huo uliweka kanuni za kugawana maeneo ya Afrika kati ya mataifa ya Ulaya. Mipaka mingi ilikuja kutokana na mikataba iliyofuata kati ya Ujerumani, Uingereza, Ubelgiji na Ureno katika miaka iliyofuata.
Jambo lingine muhimu ni kwamba "Tanganyika" yenyewe haikuwa jina la Kijerumani mwanzoni. Wajerumani waliita koloni lao German East Africa. Jina "Tanganyika Territory" lilianza kutumiwa rasmi na Waingereza baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia mwaka 1920 walipopewa eneo hilo na League of Nations.
Kwamba wanyamwezi hawakuhesabu wahehe kuwa kabila?
Kabila ni nini?
Wewe unanichosha tu na insha zako, askari wa vita vya msalaba walifuta kila kitu kuhusu sensa ya 1958 kama walivyofuta ukweli wa historia ya uhuruNdugu, madai makubwa yanahitaji ushahidi mkubwa.
Kama kweli kulikuwa na sensa ya 1958 iliyoonyesha Waislamu 66% na sensa ya 1967/1968 ikawaonyesha 33%, basi lazima kuwe na ripoti rasmi za sensa hizo na maelezo ya wataalamu wa takwimu kuhusu tofauti hiyo.
Tatizo ni kwamba hoja yako inaruka moja kwa moja kutoka "takwimu zimebadilika" hadi "kulikuwa na njama ya askari wa vita vya msalaba." Hilo ni hitimisho kubwa ambalo linahitaji ushahidi wa moja kwa moja.
Pia idadi ya dini inaweza kubadilika kutokana na sababu mbalimbali:
Mbinu tofauti za ukusanyaji wa takwimu.
Namna ya kuhesabu waumini wa dini za jadi.
Uhamaji wa watu.
Ukuaji wa shughuli za kimisionari na kidini.
Tofauti za ufafanuzi wa mtu kuhesabiwa katika dini gani.
Kuhusu madai kwamba Umoja wa Mataifa uliuliza "Waislamu wamekumbwa na janga gani lililowaua kwa 50%", hilo linahitaji kuonyeshwa kwa nyaraka rasmi. Ni wapi katika kumbukumbu za Umoja wa Mataifa kauli hiyo ipo? Bila nyaraka, inabaki kuwa simulizi, si ushahidi.
Ni kweli kwamba kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye sensa za Tanzania, na baadhi ya viongozi wa Kiislamu akiwemo Sheikh Ponda Issa Ponda waliwahi kutaka kipengele hicho kirudishwe. Pia ni kweli kwamba viongozi mbalimbali wa dini walikuwa na mitazamo tofauti kuhusu suala hilo.
Lakini kuthibitisha kwamba:
kunahitaji vielelezo vya nyaraka za sensa na kumbukumbu za UN, si simulizi pekee.
- Waislamu walikuwa 66% mwaka 1958,
- Wakapunguzwa makusudi hadi 33% mwaka 1967,
- Umoja wa Mataifa ukapinga rasmi takwimu hizo,
Kwa hiyo njia sahihi ya kihistoria ni kuleta ripoti halisi za sensa na nyaraka za UN ili madai hayo yajadiliwe kwa ushahidi badala ya hisia.
Hiyo ni serikali moja,lakini rais wa Tanzania ana mamlaka Zanzibar,kuna ofisi za muungano na vyombo vyote vya ulinzi na usalama Zanzibar, Zanzibar ikivamiwa imevamiwa Tanzania,watakaopambana ni jwtz
Na akina kinjekitile ni mashujaa wa ruvuma,pwani na moro mashariki siyo wa Tanganyika
Fikiri vizuri kijana
Kabila ni neno la kiarabu lilokopwa na kiswahili,hakuna kisiasa wala asiliHapana. Hawakuhesabu.
Ila ninyi shuleni kwenye mitaala ndio mmefundishwa hivyo.
Kabila kwa tafsiri ya asili? Au tafsiri ya kisiasa
Anayetaja Tanganyika ni mpumbavu,hata kama anakuvutia kiasi ganiDkt. Nasra amezungumza hayo leo Juni 15, 2026 wakati akichangia Bajeti Kuu ya Serikali ya Zanzibar kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambapo amechangia kuhusu Haki za Vijana wa Tanganyika kwenye nafasi ya Muungano.
Dkt. Nasra amesema ipo haja kuwepo kwa muundo mzuri wa Muungano ili Vijana wa Tanganyika na Zanzibar wafahamu nafasi zao kwenye masuala ya haki na usawa, huku akisisitiza Wazanzibar kudai haki zao sio jambo la kibaguzi.
βTunaambiwa kwamba labda Wazanzibar wakizungumza maswali ya Uzanzibar linaonekana ni swala la kibaguzi lakini si swala la kibaguzi kwa sababu Watanganyika wana nafasi yao katika Muungano na Wazanzibar wana nafasi yao kwenye Muungano ni kwa sababu ya foundation ya Muungano imekosekana ndio maana tunaona labda ajira hizi ni za wazawa na hizi sio za wazawa, tuseme tu Tanganyika inahitaji muundo unaoweleweka,β amesema Dkt. Nasra.
#MillardAyoUPDATES
SOMA VIZURI UONE NENO TANGANYIKA NA ZANZIBAR KUWA NA MIPAKA
TANZANIA KUWA NA MIPAKA
KizimkaziHamjambo!
Miezi ya hivi karibuni kumekuwa na kelele na kauli nyingi zenye mrengo wa kuuvunja muungano.
Nani yupo nyuma ya vuguvugu hilo?
Kina nani wanatarajiwa kuwa wanufaika baada ya muungano kuvunjika?
Nafahamu kuwa wahusika wakuu watakuwa miongoni mwa Wanasiasa hasa ambao majina yao hayapo na hayatajwi tajwi kwenye Media.
Na Wafanyabiashara. Wanaohitaji kuunda mfumo mwingine. Huku Muungano ukiwa kizuizi cha mfumo huo mpya.
Wananchi wao sio wanufaika wala sio wapata hasara. Muungano uwepo usiwepo kwao mambo ni yaleyale.
Swali linabaki ni kina nani?
Ijumaa Kareem
Bila Mkoloni hakuna Tanganyika mkuu.
Mkoloni hakukuta Tanganyika alikuta Dola nyingi katika jamii za kibantu na ile Dola ya sultani wa zanzibar
Bila Mkoloni hizo Dola za wanyamwezi, wahaya, wasukuma n.k. hata siku moja zisingeweza kuungana na kuunda taifa kubwa la Tanganyika. Hilo lisingewezekana kabisa.
Kwanza hizo himaya zilikuwa zinapigana zenyewe kwa zenyewe. Kama vile unavyoona urusi na Ukraine.
Katika kuunda Tanganyika ndio maana utaifa wa awali(wakoloni waliuita Ukabila) wakapiga vita ukabika(utaifa wa asili), kisha lugha ya kiswahili nayo ikawa nyenzo ya kuunganisha hizo himaya na kuzifanya zijione ni jamii na nchi moja huku kiasili sivyo.
Mkwawa alishajiisha umoja wa 'watanganyika' dhidi ya wakoloni,akitaka waungane tabora(isike) iringa(mkwawa) Tanga(abushiri na bwana heri) na watanganyika wengine dhidi ya wageniNdio wala sio uongo
Kinjektile hakuwahi kupigania vita ya watanganyika. Na wala hajui kama kuna taifa au nchi iliitwa tanganyika.
Yeye alikuwa anapigania taifa lake huko
Kabila ni neno la kiarabu lilokopwa na kiswahili,hakuna kisiasa wala asili
Unajua kuwa hakuna kabila la wanyamwezi wala wasukuma?..na humo palikua na himaya tofauti kwa watu walewale?
Wewe unanichosha tu na insha zako, askari wa vita vya msalaba walifuta kila kitu kuhusu sensa ya 1958 kama walivyofuta ukweli wa historia ya uhuru
Usinichoshe na pumphlet zako
Mkwawa alishajiisha umoja wa 'watanganyika' dhidi ya wakoloni,akitaka waungane tabora(isike) iringa(mkwawa) Tanga(abushiri na bwana heri) na watanganyika wengine dhidi ya wageni