Nani yupo nyuma ya vuguvugu la kuvunja Muungano

Samia anayechukuliwa kuwa mwenyeji wa Omani upande wa Mama ni mwenyeji wa mikoa ya huku Pwani kwa upande wa Baba yake.

Asilimia 90 ya wazenji asili yao ni mikoa ya Pwani, Lindi, Tanga, Morogoro na Mtwara, vigumu sana kuwatenga na mababu zao waliopo huku.

Tunaishia kutukanana na kukejeliana lakini mwisho wa siku wote tunarudi kukaa kwenye viti kwani damu ni nzito kuliko maji.
 

Hakuna anayebisha kuwa kuna mahusiano ya damu, ndoa na biashara kati ya Wazanzibari na watu wa Bara. Hilo lilikuwepo kabla ya Muungano na litaendelea kuwepo hata kesho. Mombasa ilikuwa sehemu ya Zanzibar mpaka 1963 na ina mahusiano makubwa zaidi na Zanzibar .

Lakini usichanganye mahusiano ya wananchi na mjadala wa kisiasa kuhusu Muungano.

Wazanzibari wengi wanaouliza maswali kuhusu Muungano hawafanyi hivyo kwa sababu wanawachukia Waislamu wa Bara au Wakristo wa Bara. Wanauliza kuhusu historia na haki za kisiasa.

Je, mauaji na mateso baada ya Mapinduzi ya 1964 hayakutokea?

Je, malalamiko kuhusu mamlaka ya Zanzibar ndani ya Muungano hayajawahi kuwepo?

Je, uchaguzi wa Zanzibar wa 2015 haukufutwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, baada ya Mwislamu kikwete kuleta majeshi na kumlazimisha kufuta uchaguzi jambo lililosababisha mjadala mkubwa wa kisiasa Zanzibar?

Hayo ni maswali ya kisiasa yanayohitaji majibu ya kisiasa, si ya kidini.

Kusema kila anayekosoa Muungano anachukia watu wa Bara au anataka kuwafukuza watu wa pwani ni kukwepa hoja halisi.

Muungano ukitetewa au kukataliwa iwe kwa haki, usawa na ridhaa ya wananchi; si kwa vitisho wala kwa kugeuza kila mjadala kuwa wa dini.
 

Na zaidi Mombasa msijifanye hamjuwi kwani , Mombasa ilikuwa kama Pemba mpaka 1963. Hiyo haifanyi tuungane kwa kuvamiana , Tanganyika mna uhusiano zaidi na Kenya na Uganda kuliko Zanzibar mbona hamuungani ??
 
Ila aliyeunganisha muungano alitukosea mno watanganyika. Hivi kadude kazanzibar ni ka kuunganisha na Taifa kubwa kama Tanganyika kweli? Dah!
 
Akina maria sarungi,hilder Newton na huyo mpuuzi wa TLS matamshi yao ni Tanganyika Zanzibar Tanganyika Zanzibar,sijui wanadhani muungano ukivunjika hakuna waislam Tanganyika!
Huwa nakuheshimu ila Leo nimeona ka ujinga kako, mbona huwaongelei wale wawakilishi wa Zanzibar walio ongea ubaguzi hadharani tena wakapigiwa na makofi why hujawaongelea hao?
 
Ila aliyeunganisha muungano alitukosea mno watanganyika. Hivi kadude kazanzibar ni ka kuunganisha na Taifa kubwa kama Tanganyika kweli? Dah!
Elimu ndogo ya babu yenu Nyerere hiyo , aliona mtakuja kusema jinchi hili Tanganyika lenye kila kitu mumeshindwa na ka kinchi hicho Zanzibar ? Mngaliuona upofu wake
 
Hapana ni jamii mbili zenye asili moja lakini hiyo haiwafanyi wawe taifa moja. Ndio maana mpaka mkoloni anakuja aliwakuta kila mmoja anahimaya/dola yake
Wanyamwezi ni mkusanyiko wa makabila manne,wakimbu,wanyanyembe,wakonongo,wasumbwa na walikua na himaya tofauti,nao siyo taifa moja?
 
Hiyo ni kiki ya chadema kupandikiza chuki kwa wananchi ilimrad watu waingie barabarani, wapo pamoja na TEC ikiwaunga mkono kusambaza udini na ukanda kwakuwa raisi aliyekuwepo ni muislam na pia ni mzanzibar

Anaebisha na atunze hii comment, tuone kipindi kijacho cha mgalatia kama hizi agenda zitakuwepo
 
 
LABDA TUWE NA SEREKALI TATU,KILA MOJA INAKUSANYA MAPATO YAKE INAJIENDESHA,NA KUJIPANGIA INACHOKIHITAJI, MUUNGANO WETU USIMAME KWENYE MAJESHI YETU, BAJETI ZA MAJESHI ZITOKE KILA UPANDE KWA KIASI CHA UKUBWA WA TAIFA HUSIKA,KILA UPANDE UHUSIKE NA RASILIMALI ZAKE./ EBO WANAKERA,ENDAPO WANAJIONA WANAYAWWZA SANA KWA AKILI ZAO,KABLA YA KUUVUNJA KABISA TWENDE HATUA HII.
 
Kuna zama na ZAMU poleni sana watanganyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…