Abdul Nondo namkumbuka wakati akisoma political science pale mlimani akiwa na urafiki wa karibu na Emijidius Cornel kjana aliyekuwa anachukua shahada ya ualimu pale chuo kishiriki cha elimu cha Dar es salaam (DUCE )ila akiwa mwanaharakati wa kutetea haki za walimu wanaojitolea pamoja na mambo ya kijamii chuoni pale .
Nimeitoa historia kidogo kuhusu hawa vijana wawili sababu nilipata kuwajua wakati huo na ni wakati huo ndiyo nikamjua kiasi chake Abdul Nondo alikuwa kijana mwenye kuijua haki yake na kuiijua sheria kwa kina ,alismama kidete kumtetea EMIJIDIUS COENEL pale alipopelekwa wodi ya vichaa Muhimbili kwa kudai ana shida ya afya ya akili na chuo chake cha DUCE (DAR ES SALAAM UNIVERSTIY COLLEGE OF EDUCATION)
Japo zilikuwa hujuma juu ya harakati zake za kutetea haki za wanafunzi kwa baadhi ya mambo haswa ucheleweshaji wa boom ,kufelishwa na kutafuta walau supporting power kwa walimu waliokuwa wanajitolea katika shule mbalimbali katika wilaya ya TEMEKE haswa WAILES ,MIBURANI NA KEKO SECONDARIES .
Ni katika hayo machache niliouona mchango wa Abdul na pale waliposhirikiana na Emijidius kuwaleta viongozi wa kitaifa hasa wa chama cha mapinduzi katika hafla na utiaji moyo kwa wale walimu wanafunzi walikokuwa wanajitoleq katika shule mbalimbali ,mfano wa kiongozi aliyeawahi kuletwa kwa mialiko yao ni pamoja na KINANA ,HAMPHREY POLEPOLE lakini pia mbunge mstaafu wa jimbo la TEMEKE .
Ni katika hayo naweza kusema nimemuona NONDO alifanya nini kiasi cha kuweza kusema ni machache mno kulinganisha na mheshimiwa Tundu antipas Lissu sababu ya umri wake katika harakati ni mkubwa kiasi cha kuona kuwa kuwalinganisha ni kumkosea heshima mheshimiwa Antipus Lissu .
Hivyo itoshe kusema Tundu bado yuko juu kwa mengi zaidi japo kwasasa yupo nyuma ya nondo hivyo Abdul anaweza kuwa na nafasi ya kufanya mambo makubwa labda yanayoweza kumuweka juu ya Lissu wakati huu ambao hayupo .
Ahsante