Naomba kuelezwa ni nani Mwingine zaidi ya Dkt Tulia na David Kafulila amewahi kurejesha Chenji Serikalini?

Naomba kuelezwa ni nani Mwingine zaidi ya Dkt Tulia na David Kafulila amewahi kurejesha Chenji Serikalini?

2016?Leo hii imepita miaka mingapi?Kwa nini habari ya Kafulila(siyo wizara yake) na Tulia (na siyo bunge/utumishi wa bunge)zije nyakati hizi?It's very suspicious activity!??????????
Ulitaka z
2016?Leo hii imepita miaka mingapi?Kwa nini habari ya Kafulila(siyo wizara yake) na Tulia (na siyo bunge/utumishi wa bunge)zije nyakati hizi?It's very suspicious activity!??????????
Ulitaka zije lina habari hizi?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kuna watu ni WAZALENDO kwelikweli,ni wasafi sana, ni waaminifu waliopitiliza,ni wacha Mungu na wenye Hofu ya Mungu sana na wana uchungu mkubwa Sana na Maisha ya watanzania. Miongoni mwa watu hao basi ni hawa watu wawili ambao wamewahi ishitua Tanzania na kugusa mioyo ya mamilioni ya watanzania.

Ngoja niwape story bila kuwachosha kuelekea wikendi. Ilikuwa hivi Mheshimiwa Chuma Mwenyewe David Kafulila akiwa katibu Tawala Mkoa wa Songwe alipewa Billion Sita kujenga mpaka kumaliza ujenzi wa Makao makuu ya mkoa wa Songwe yanayopatikana katika kata ya Mlowo Eneo la Nselewa. Lakini Chuma kwa kutumia mfumo wa Force Akaunti katika ujenzi wa Makao makuu hiyo hakumaliza pesa hiyo.

Ambapo mpaka jengo linamalizika na kukamilika Chuma Kafulila akabakisha Chenji ya Karibu Billion Mbili.Siku hiyo anasoma taarifa hiyo mbele ya waziri mkuu mwaka 2020 Ofisi za makao makuu ya mkoa ,watu wote walibaki Midomo wazo na kustaajabu Uzalendo alio uonyesha CHuma Kafulila. Nakumbuka siku hiyo alisoma taarifa hiyo kwa umakini na utulivu wa hali ya juu sana. Na kwa bahati nzuri mimi mwenyewe nilikuwepo siku hiyo na nilikuwa karibu sana eneo la Tukio na nilikuwa nimesimama jirani na Mheshimiwa David Silinde ambaye siku hiyo alipewa nafasi ya kuzungumza pia. Nilikuwa jirani maana nilikuwa ni kiongozi wakati huo kwenye jumuiya ya vijana yaani UVCCM.

Siku hiyo nakumbuka wakati tunarejea majumbani Chuma Kafulila alikuwa ni gumzo sana tena sana midomoni mwa watu ,kwa namna alivyo onyesha uzalendo wa kipekee na uaminifu wa kiwango cha juu sana.

Mwingine ni Dada wa Taifa na Rais wa IPU na msomi Nguli wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini.huyu sina sababu ya kueleza mengi maana mnakumbuka Billion kadhaa alizorejesha serikalini baada ya kubana matumizi kule Bungeni.

Nimeamua niandike haya kueleza kuwa kuna watu ni waaminifu na wazalendo sana,ambao miongoni mwao ni hawa niliowataja hapa.

Jiulizeni ndugu zangu watanzania ni mara ngapi mmesikia kuwa mradi fulani Umepelekewa mamillioni kwa mamillioni ya pesa, lakini pesa zimekwisha na mradi haujafika hata nusu na hela haieleweki iliko kwenda? Mara ngapi mmesikia miradi kama vile ujenzi wa shule au kituo cha afya au barabara au usambazaji wa maji unakatu umekwama kukamilika kwa kuwa tu mapesa yaliyotolewa yameliwa na kuisha kabla hata mradi haujafika hata Nusu yake? Hamjaona haya wanapofanya ziara mawaziri wetu huko mikoani wakisikitika mpaka wanatamani kulia baada ya kukuta pesa zimeliwa? Hamjaona waziri mkuu wetu akiongea kwa uchungu na kwa huzuni na kuagiza ukaguzi na uchunguzi ufanyike kubaini waliotafuna pesa?

Lakini vyuma hivi Mheshimiwa Dkt Tulia pamoja na David Kafulila vilirejesha Chenji ya mamilioni kwa mamilioni,pesa ambazo wangeamua kuzichepusha kutunisha akaunti zao benki. Lakini kwa uzalendo wao wakasema hapana acha turejeshe pesa hizi ili zikajenge vituo vya afya ,shule, usambazaji wa maji safi na salama,umeme, barabara n.k.

Mwisho niseme tu kuwa mimi ni mzalendo na nimekuwa na tabia ya kutetea na kuwasemea wazalendo wote. Mimi sioni haya wala aibu kumtetea na kumsemea mzalendo bure kabisa pasipo malipo ya aina yoyote ile wala kupewa hata mia tano tu ya Vocha. Nataka Taifa liwe na utamaduni wa kuwaunga mkono wazalendo na wachapakazi wa Taifa letu ,tusiache wakachafuliwa na kushambuliwa na wabaya .ndio maana kuna watu awali wakasema mara nalipwa kwa uchawa ,wengine wakasema nalipwa na Mheshimiwa Dkt Tulia,wengine wakasema Nalipwa na Mwamba Mwenyewe Paul Makonda na sasa wengine wanasema nalipwa na Chuma Kafulila.ila hawasemi nalipwa shilingi ngapi na kwanini nilipwe na kila mtu na na kwa watu wote hao? Na hawasemi kwamba wao wanalipwa na nani kuchafua watu humu jukwaani na mitandaoni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kumbe hata huyo mama hajawahi kurejesha, nilitaka nimtetee lakini maadam wewe haumtambui kuwa amewahi kurejesha basi tuamini hivyo kuwa mama hajawahi kurejesha.
 
Bila shaka umekurupuka ukiwa na vitu fulani kichwani. Hivi umeelewa hoja lakini? Hoja ni kuwa walipewa pesa lakini wakabakisha na chenji na kumaliza kazi kwa ufanisi na ubora uleule unaotakiwa kwa pesa pungufu ya kiasi kilichoidhinishwa kwao.lakini kwa usimamizi mzuri pesa zinabaki na wakaziridisha serikalini badala ya kugawana wenyewe kwa manufaa yao binafsi.
Wewe huna akili kabisa, Kiongozi bora angefanya re-allocation kutekeleza miradi au changamoto zingine katika eneo lake. Kwa mfano katika Mkoa wa Songwe lazima kulikuwa na mahitaji mengine muhimu ya wananchi ambayo yalitakiwa yatekelezwe badala ya ya kurudisha fedha Hazina. Kwanini hakufanya?!
 
Acha kutukana matusi.unafahamu sheria za kiutumishi au unaropokatu hapo? Unafahamu kila kitu kinakwenda kwa utaratibu na maandishi ya vikao? Unafahamu kila kitu kinahitaji kupitia miongozo? Acha umbumbumbu wako hapa wewe.
 
Wewe huna akili kabisa, Kiongozi bora angefanya re-allocation kutekeleza miradi au changamoto zingine katika eneo lake. Kwa mfano katika Mkoa wa Songwe lazima kulikuwa na mahitaji mengine muhimu ya wananchi ambayo yalitakiwa yatekelezwe badala ya ya kurudisha fedha Hazina. Kwanini hakufanya?!
nadhani Kurejesha pesa Serikalini Haina maana huwezi kufanya reallocation baada ya approval
 
Mbona walisifiwa na kupewa makaratasi ya pongezi 2016?Hizi "rising from the deads" zenu zina nia gani kwa nyakati hizi?
Historia husimuliwa wakati wote,
Kama watu wamefanya mambo mazuri hata kama ni miaka 20 iliyopita yasemwe tu.
 
Historia husimuliwa wakati wote,
Kama watu wamefanya mambo mazuri hata kama ni miaka 20 iliyopita yasemwe tu.
Kuna kitu.Si bure.Wiki nzima?Kafulila hili,Kafulila mule!Na,ili kupoteza maboya,mmemchomekea na Tulia.You people!😂🙏
 
Hawezi akaelewa hilo maana ana msongo wa mawazo
Mimi bado naishi nyumbani mwa Baba yangu.Msongo wa mawazo bin sonona nitoe wapi?Ninyi mnatutapeli na nyuzi za kumsifia Kafulila.Mna agenda ambayo haina tofauti na ile ya kuchora kwenye mawe makubwa na madaraja mwaka ule..."CHAGUA MWIGULU.NI MZALENDO"..!Tofauti yenu ni nini hapo?
 
Shida iko wapi?
Kila mwanasiasa anaambition kubwa,
Ila kwa sasa tuzungumzie kwanza Uzalendo wa huyu 2mbili
 
Napenda mijadala kama hii, tujifunze kutambua vipaji vikiwa bado chini kabisa
 
Back
Top Bottom